Mtu-Pori
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 1,308
- 1,522
Niliwahi kununua LG G2 nikiamini ni international version, duka fulani Samora Avenue. Kwenye boksi imeandikwa namba/code ya int. version. Ndani kwenye simu baada ya kufika home, nagundua ni ya mtandao wa Verizon (USA) imekuwa unlocked. Kuna baadhi ya vitu ilikuwa haiwezi kufanya ikiwemo wireless tethering, hakuna support wala software updates. I was very disappointed. Sasa hivi simu nanunua kwenye mitandao ya simu au kw authorized dealers kama Huawei pale Mlimani City.