Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

wanafungua ndio lakini ni kosa kisheria na ukikamatwa fine milioni 10.

jaribu kuwasiliana na TCRA kama watakusaidia.
hivi wanaweza kugungua endapo unatumia sm uliyobadilisha imei waliyoifungia?
 
Asante kwa uelewesho wako murua kaka, nimekuuliza hivyo sababu hii iphone yangu nilinunua kwa mtu inafanya kazi fresh kabisa ila kuna baadhi ya vitu ipo tofaut kabisa na iphone zote nilizo wahi kutumia, kwanza hii simu nikiwa imezimwa nikichomeka chaja inaleta kibox cha chaja na inaendelea kuonesha inachaji kitu ambacho sijawahi kukiona kwenye iphone huwa najua iphone ukiichomeka kwenye chaja inawaka yenyewe automatic! Pili hii simu upande wa mwanga brightness hakuna sehem ya kufunga usijiongeze automatic! Tatu hii simu tangia niwe nayo namba za simu hazionekani sababu namba zangu zote naziwekaga kwenye icloud
801467fe34c313c17f8ec4ce932283af.jpg
6b325e0f6a20085fbd4dc076d3f2eef5.jpg

Kama still unatatizo ni pm nione namna gani naweza kukusaidia..
 
Wakuu mimi nina Lg F160L ya Kikorea. Ina antenna kama radio nilitaka kujua ina kazi gani.
 
habari natumia Y100-T00 simu imejaa kichina balaa!! hauwezi kuangalia USsD kabsa. nawezaje kusolve hii kitu. hata kuweka vocha uwezi kabsaa
 
Nitajuaje kama Samsung niliyonunua Ni nzuri kwa Matumizi Ya Kitanzania
 
Nitajuaje kama Samsung niliyonunua Ni nzuri kwa Matumizi Ya Kitanzania
inatakiwa iwe ni international version, google samsung fulani international version. mfano galaxy s7 international version ukishaijua angalia ya kwako kama model ni moja. kuangalia ya kwako nenda setting then about
 
noma sana me nna kitu cha note one
shv-s160e
napata tabu kudadeq
kwanza msg zangu mwisho text 80 na zaid ya hapo ni mms
version hata kit kat sifiki na no update
nimesaka rom ila sijapata kitu na walio juu zaidi yangu wameniambia nisijaribu kwa phone hii ntaiua kabsa
odin haitumiki wala sammobile hakuna roms za hii simu

NATAMANI KUITUPA
 
Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na ndugu yangu mmoja mitaa ya Aggrey tukitafuta simu aina ya galaxy Note 4 mpya, huwezi kuamini tulizunguka maduka yanaweza kufika hata 100 lakini hatukupata hata note 4 moja ambayo ni ya kimataifa (Africa pia) zote zilikuwa ni simu ambazo wamezitoa kwenye mitandao ya simu ya Kimarekani, Korea na China pamoja na nchi nyengine kubwa kubwa. Simu hizi nyingi zilikuwa zimelokiwa na jamaa wamezi unlock na pia ni mbaya kwa matumizi yetu ya kitanzania, leo hii nimeona niandike thread hii kuelezea madhara ya hizi simu na pia tuelezane njia za kupunguza hayo madhara kwa wenye nazo.

Hupati updates, warranty wala support yoyote
Unaponunua simu hizi usitegemee kupata updates badala yake ukitaka update inabidi udownload manual, vile vile hata kama simu ni mpya ikiharibika inabidi urudishe ilipotoka. mfano una galaxy s7 ya kikorea ukiwapelekea samsung Tanzania hawatakutengenezea sababu haiwahusu. Hata mwenye duka akikwambia anakupa warranty ni muongo tu labda airudishe alipoitoa kama atakua tayari.

Zinasumbua ussd
Umeshanunua simu ukaona ukiuliza salio *102# inakubali lakini mpesa, tigopesa na vyengine vinakataa? ukiona hivyo ujue tayari upo mkumbo huu umeuziwa simu za kikorea na wenzie
connection-problem-invalid-mmi-code.png


Muda wote zinaandika 4g au kutoshika kabisa 3g
Watu wengi hufikiri simu zao zina 4g kumbe hazina, mitandao mingi ya kimarekani na baadhi ya nchi wanaitwa hspa+ kama 4g kitu ambacho sio sahihi, hivyo simu hizo zikija hapa kwetu huandika 4g hata kama mtandao ni wa 3g, ukiona simu yako ipo hivi ujue umeshauziwa hizi simu, pia kuna mitandao kama T-mobile band yao ni 1700mhz hivyo simu zao zinaweza zisishike kabisa 3g huku kwetu

Simu za CDMA na band tofauti
Pia simu hizi zipo za CDMA zinaweza kuja Tanzania zisishike kabisa network ukapata pengine 4g tu, na hio 4g inaweza iwe ni band ambazo hazikubali kwetu, mtandao pekee wa Tanzania wenye band za kichina china ni smart band 2300mhz hivyo ukiwa na simu ya namna hii angalia mtandao wa smart.

Zinakuja bila google play store
Nchi kama China playstore kwao sio maarufu, hivyo simu zao zikija huku kwetu zinasumbua unakuta haina playstore wala app yoyote ya google hivyo kuanza kukuhangaisha kuweka hizo app sometime inabidi hadi uflash simu

SMA charachter sio 160
Kikawaida sms moja huwa na herufi 160 (pamoja na space na namba) lakini simu hizi huwa na herufi chini ya 160 hivyo utakatwa hela nyingi zaidi pamoja na kuharibu mfumo mzima wa kutumiwa mfano mtu akituma msg ya 160 kwako itakuwa kama msg 2. kwa wale wanaotuma msg ni muhimu hii.
jw-ucEQB3dwV42Bl8OMBJR51HbdW-0rLyJoJvOsrr2IP_b2-LlhJd0Cx-qaW0JqM_54=h900

mfano hii ina charachter 70 tu hivyo msg ya 160 itahesabika kama sms 3

Dialer ya kikorea au kichina
Pia inaweza tokea dialer (ya kupigia simu) ikawa mfumo wa kikorea
main-qimg-6a4e834ec4324839357802e8b65ec023


Support ndogo ya developers
Pia simu hizi huwa na custom rom chache au usipate kabisa, njia za kuroot wakati mwengine zinakuwa ngumu, nyengine zinalokiwa bootloader etc kama wewe ni power user simu hizi zinakuwa pasua kichwa.

Hayo ni baadhi ya madhara ya simu za kikorea, kama kuna mengine nimeyasahau mutaniambia.

Namna ya kujua kama simu ni ya kikorea au international
Kusema simu inaitwa lg g2 au galaxy s5 haitoshi kila simu inakuwa na model zake, simu moja kama galaxy s5 inaweza kuwa na model tofauti tofauti hata 10, hivyo kujua simu yako fanya hivi

-Nenda setting halafu about utaona model number ya simu
Tap-on-device-name-under-settings.jpg

Ukiipata hio model number angalia online ni ya wapi, site kama gsmarena kwenye specs za simu hueka model na maeneo zinapotoka unatakiwa uwe na model international, au just google simu yako na neno international version kwa mbele, mfano galaxy s5 international version utapata model ya international kama huna hio ujue kuna uwezekano kupata madhara ya hapo juu

-Njia nyengine ni kuregister na warranty ya samsung sema njia hii ni kwa simu mpya zilizotoka chini ya miaka miwili iliopita.. utaandika neno REG*imei# halafu tuma kwenda 15685 utajibiwa, badili neno imei na imei halisi ya simu

jinsi ya kupunguza madhara ya simu za kichina

1.Badili app husika
Mfano dialer ina maneno ya kikorea nenda playstore install dialer nyengine tumia

2. Badili rom
Unaweza ukaeka custom rom kama cyanogen hii itasolve matatizo mengi tu

3. Mods mbali mbali
Kuna simu zinakubali kubadili bands zake na kueka bands za nchi yako, kuna mods za bootloader kwa wale ambao rom za international zinakataa etc

Una tatizo la simu za Kikorea? Usisite kulitaja hapo chini.
Aiseee mim nilinunua simu Nina Samsung note 1 lakin Huduma za TIGOPESA na MPESA inagoma kabisa na ni mpya sijui unanisadiaje
 
Hizi simu mara nyingi zinakuwa refurbished phones na ndio zinapatakina kwa bei nafuu sokoni thats why wafanyabiashara wengi wa dar wakienda china wanapenda kununua.the only way ya kupata simu mpya kabisa ni kwenda kwa authorised samsung dealer ambapo mara nyingi bei zao huwa juu
 
Aiseee mim nilinunua simu Nina Samsung note 1 lakin Huduma za TIGOPESA na MPESA inagoma kabisa na ni mpya sijui unanisadiaje
kwa issue kama ussd solution ni kubadili firmware nzima, model yake ni ipi?
 
Yangu inaandika phone not allowed [HASHTAG]#mm6[/HASHTAG] ysn network haisomi kabisa mwanzo ilianza inakubali line zote badae nilivyo kua na line ya 4g kwa voda ikawa inasoma dar tu mwisho wa siku zote zikagoma ikabaki kusupport halotel tu sasaiv hata hyo halotel haisom but nikiweka na kuwasha data nakula internet bt network za simu wala sms za kawaida haxikubali yan
ishalambwa hiyo na tcra mkuu
 
Chief thanks kwa uzi matata kma huu.kuna wengine hatujui kuhusu izi cm nakumbuka nlinunua s2 uki instal app nying ina freez balaa nadhan kutokujua mamb kma haya mana wengne ni vilaza sna kwne mamb ya cm.na vip unaznzungumziaje hiz cm kabila la tecno
88cbf5f08f210edeae58c5d765b6f9ec.jpg
 
Chief thanks kwa uzi matata kma huu.kuna wengine hatujui kuhusu izi cm nakumbuka nlinunua s2 uki instal app nying ina freez balaa nadhan kutokujua mamb kma haya mana wengne ni ****** sna kwne mamb ya cm.na vip unaznzungumziaje hiz cm kabila la tecno
88cbf5f08f210edeae58c5d765b6f9ec.jpg
mimi huwa sishauri kabisa simu za mediatek, sababu zina matatizo mengi tu,
 
mimi huwa sishauri kabisa simu za mediatek, sababu zina matatizo mengi tu,
Ni kweli mm mwenyewe ni fundi na ninajua mtk zinamatatizo mengi sana lakini najiuliza mbona makampuni makubwa kama sumsung htc nk nayo yameanza kuitumia mtk katika simu zao.
 
Ni kweli mm mwenyewe ni fundi na ninajua mtk zinamatatizo mengi sana lakini najiuliza mbona makampuni makubwa kama sumsung htc nk nayo yameanza kuitumia mtk katika simu zao.
lengo la kampuni ni kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza faida, kabla ya mediatek samsung walikuwa wanatumia soc za spreadtrum kwenye simu zao za bei rahisi, walikuwa na uwezo wa kueka exynos lakini hawaeki sababu wanataka faida kubwa
 
Back
Top Bottom