Jifunze Kuushinda Woga/ Hofu

Jifunze Kuushinda Woga/ Hofu

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,483
Reaction score
167,064
Mambo vipi fellaz
Leo nimeona nije kivingine. Nakuja Na uhasishaji wa kusoma vitabu.
Eat that frog
Kitabu hiki ni kifupi Na kizuri sana, kimeandikwa kwa kiingereza rahisi kueleweka hata kwangu niliyesoma vidudu kota
Kitabu hiki ni kitabu hamasishi inspiration kitaenda kubadilisha kwa ujumla mtazamo wako wa kufukiri Na kutenda mambo mbalimbali
Kama unatakiwa Kula vyura wawili, anza Na Yule mbaya zaidi.
Watu tunaogopa vitu vigumu, ni hulka ya tuliyozaliwa nayo, tunapenda miserereko.
Wenzetu walioendelea wanawafunza watoto wao tangu wangali wadogo namna ya kuushinda uwoga/ hofu.
Wakristo wameambiwa Mara 365 kwenye Biblia kwamba usiogope. Hii ni sawa Na Kila siku asubuhi kwa mwaka mmoja kuna sauti ya upole inakuambia usiogope.
Usiogope magumu unayopitia, usiogope Hali ya uchumi iliyopo, usiogope kuanza jambo jema jipya, usiogope kuanguka, usiogope kuaibika Na Wala usiogope kuendelea kujivunza.
Jifunze kutumia muda wako vizuri, Jifunze kufanya tafakari kwa kina, Jifunze kuweka utulivu wa nafsi mwili Na akili, Jifunze kusamehe Na Jifunze kutenda wema.
Jifunze maarifa mapya ya biashara, afya, teknolojia , kilimo etc.
Jifunze kwenye kazi zako kuanza Na zile kazi ngumu zaidi ndipo uende kwenye nyepesi.
Wenu mtiifu, niliyeamua kurudi darasa la Kwanza kuunga mkono juhudi za mwalimu Matthew, maana anafanya kazi kweli kweli. Kulifundisha zuzumagic kama mimi kosoma, kuhesabu Na kuandika hadi nikaelewa, haikuwa kazi rahisi. Mtanikuta Sisimba nagonga kengele
 
Ukishasema neno vitabu, lazima watu waukimbie Uzi wako.
Watanzania tunataka story za kijipu uchungu cha lemutuz zee la miaka 18. Sijui baba yake alijisikiaje baada ya ile video?
Watanzania tu wavivu sana na ukitaka kutambua hilo mwambie kusoma. Mtu anaweza kukuuliza ofisi fulani iko wapi wakati hapi aliposimama ndipo ofisi ilipo isipokuwa hajasoma bango mbele au nyuma yake
 
Watanzania tu wavivu sana na ukitaka kutambua hilo mwambie kusoma. Mtu anaweza kukuuliza ofisi fulani iko wapi wakati hapi aliposimama ndipo ofisi ilipo isipokuwa hajasoma bango mbele au nyuma yake
Ukiwa na biashara yako usiitangaze kwa tangazo ambalo linamlazimu mnunuzi asome, utaanga hela zako za tangazo. Amini amini nakuambia Tanzania ndio nchi pekee duniani ambayo RAIA wake ni wavivu Wa kusoma hata tarehe ya kuekspaya bidhaa aliyoinunua
 
Thank you a million. Ngoja niingie mtandaoni. Naamini nitapata machache ambayo yataufanya mwaka huu kuwa shuhuda wa matendo makuu ya MUNGU.
 
Yan watanzania cc ni waoga sana..inafikia hatua mpaka konda wa dala dala anakwambia rudi nyuma hata kama nafasi hamna huwezi mwambia zaid ya kujisogeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom