Jifunze kilimo cha nyanya

Wakuu nauliza hivi ni sahihi kulima nyanya (kupanda) wakati huu wa mvua?

Je ni changamoto zipi natakiwa kujiandaa kukabiliana nazo endapo nitalima msimu huu wa mvua za masika
 
Wakuu nimepatwa na changamoto ya majani ya nyanya kuungua na kunyauka, nimejaribu kuuliza ni ugonjwa gani wengine wanasema ukungu wengine joto la ardhi. Naombeni wataalamu mnisaidie kujua hiki ni nini na dawa yake
IMG_2353.JPG
IMG_2349.JPG
IMG_2350.JPG
 
Kwa hizo dawa ulizotaja maisha huwezi muangamiza tuta
Tumia dawa zinazoua adult flies wa tuta kama vile evisect,thunder,actara kisha piga na zinazoua lava ambazo ni hizo umetaja tuta ataisha shambani kwako,piga ya adult baada ya siku tatu piga ya lava tena baada ya siku tatu piga ya adult kisha baada ya siku tatu ya lava. Tuta utammaliza


Au tukia recharge-antario-biotrine pia mtiririko huo unammaliza.

Ukiweza weka na tuta traps
mkuu tuta traps ndio ipi iyo mana hawa wadudu wamenimalza
 
Kwa hizo dawa ulizotaja maisha huwezi muangamiza tuta
Tumia dawa zinazoua adult flies wa tuta kama vile evisect,thunder,actara kisha piga na zinazoua lava ambazo ni hizo umetaja tuta ataisha shambani kwako,piga ya adult baada ya siku tatu piga ya lava tena baada ya siku tatu piga ya adult kisha baada ya siku tatu ya lava. Tuta utammaliza


Au tukia recharge-antario-biotrine pia mtiririko huo unammaliza.

Ukiweza weka na tuta traps
 
Habari za asubuhi wadau.. Hop mmedamka salama. Baada ya jamaangu mmoja last week kunishawishi kulima nyanya baadaya ya kufika shambani kwangu na kuona eneo la wazi nikawiwa kuja kusaka maarifa kwenye hiki kisima cha maarifa jf, nilipo type nyanya kwenye search bar nikakutana na huu uzi, nimeusoma kwa siku tatu mfululizo kwa sababu muda wangu ni mchache wa kupeluzi, wote mlioshiriki huu mjadala niseme moja tu, MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA, horticulturist, yumbayumba na wengine wote asanteni sana, mimi niko Bukoba Manispaa, nimechagua kilimo kuwa mstakabari wa maisha yangu, vijisenti kidogo ambavyo nimekuwa nikipata kitaa nimekuwa nikiviwekeza kwenye ardhi kwa sababu nataka kuwa na himaya yenye mifungo aina tofauti na bustani za mbogamboga na matunda na nimebahatika kuwa na eneo la ukubwa wa ekari 2.5 mpaka sasa na liko jirani ya mto. Mwaka 2016 kwa ubia na wenzangu wawili tulianzisha project ya kilimo cha mbogamboga kwa kumuajiri bwana shamba wa makaratasi na mimea ikawa inafia kitaluni kabla ya kwenda shambani, na hakuwahi hata siku moja kutueleza kuwa kuna mbegu chotara, nafikiri hata yeye hakuwa analijua hilo, pamoja na ku invest kiasi cha mil 6 shambani ila hatukuwa na miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji zaidi ya kununua mashine na tanks, wakati tunahangaika na miche kwenye kitalu kikaja kiangazi kile cha 2016 kikakausha vyanzo vyote vya maji vya jirani na tukajikuta balance yote imetuishia na hatukuwa tena na pesa ya pembejeo na mbolea, ukawa mwisho wa project na kila mtu akaendelea na maisha yake, ikanibidi nianze kilimo cha mazao yasiyokuwa na usumbufu sana kwa kiwango kikubwa ili nitakapouza nipate mtaji wa drip irrigation na miundombinu mingine muhimu shambani kwangu, hivyo nimepanda viazi vitamu ekari moja na nusu na muhogo ekari moja, natarajia kuanza mavuno mwezi wa nane. Sasa pale shambani kuna eneo nusu ekari ambayo muhogo haukustawi vizuri na tangu juzi nimeanza kuung'oa kwa ajili ya NYANYA, natarajia mwezi huu shamba na na kitaru viwe tiyari na mwezi wa sita nihamishie miche shambani, japo kwa eneo hilo hilo ambalo kwa vipimo linaonyesha linaweza beba miche 6,000 nilitaka nitenge kwa ajili ya nyanya miche 3000, hoho miche 1500 na bilinganya 1500. Elimu niliyoipata humu nina imani itakuwa mwongozo bora katika kufanikisha harakati zangu pamoja na msaada wa ziada kwa wale ambao nimewafuata inbox. Asanteni sana wadau, Mungu abariki kazi ya mikono yetu wakulima. Mwenye ushauli naomba.
 
Jamani Bei ya Nyanya ikoje huko Masokoni? kwa maana Huku niliko (Tanga) Bei ni Maumivu, Creti linaenda mpaka elfu kumi (10) Na nikicheki shambani zianiva kwa fujo. Kichwa kimepata Moto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom