Jifunze kilimo cha nyanya

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,074
2,000
NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa, kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji.


Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na kusahau kujadili kuhusu HASARA zisababishwazo na kilimo cha zao hili.

Kiukweli NYANYA inaweza ikakutoa ukafanikiwa ki maisha ila inaweza vile vile ikakupa hasara kubwa ukajuta kufanya kilimo cha zao hili.

Andaa matuta vizuri lakini naomba nikwaMbie ndugu msomaji kila aina ya Tuta ina mahala pake na ardhi yake maalum hivyo ni bora kuichunguza ardhi yako vizuri maana kwa udongo wa kichanga ukiweka matuta ni dhahiri udongo utapelekwa na maji...kipindi cha kumwagilia.

Zingatia nafasi katika upandaji wa zao hili la nyanya nafasi inayopendekezwa ni cm50 kutoka mche hadi mche mwingine. Usipande zao hili pasipo kufuata kanuni ya nafasi ya cm50 maana zao hili lina majani na ukipanda kwa kubananisha sana utasababisha joto kuzidi, vile vile matawi yakigusana kutoka mche mmoja kwenda mche mwingine unaweza kusababisha miche iambukizane magonjwa.
Kwa kawaida zao hili huchukua siku 72 hadi 120 kupanda hadi kuanza kuvuna. Zao la nyanya ni zao linalofyonza sana rutuba hivyo hakikisha ardhi unaiboresha kwa kuiweka mbole mara kwa mara...kwa mbolea za dukani Urea, dap, N.p.k, can na nyinginezo hakikisha unafuata maelekezo ya mtaalaam kabla ya kutumia hizo mbolea...mbolea ya Samadi au za mifugo hakikisha mbolea hizo ziwe zimekauka kabisa ziwe kama unga au kavu maana mbolea za mifugo zikiwa mbichi zitasababisha miche kuungua, na inaweza kudumaa pia.

Nyanya inashambuliwa sana na wadudu ambao hupelekea zao hili kupata magonjwa hivyo kabla hujapanda zao hili hakikisha unaanda shamba na kupiga dawa za wadudu pamoja na dawa za magonjwa za ukungu. Ni vigumu sana kutibu nyanya pindi utakapoanza kuona dalili kwenye mche ulioathiriwa na magonjwa. Hivyo kipindi chote cha uhai wa nyanya ni lazima kuzingatia matumizi ya dawa.
Endapo utagundua baadhi ya miche imepata maambukizi muone mtaalam wa madawa akushauri ukishindwa kuutibu ni bora ukaung'oa uo mche maana nayo huambukizana magonjwa kama tunavyoambukizana binaadam.
Uhai wa nyanya unategemea Maji, Mbolea na Dawa japo baadhi ya wataalam hushauri kuongeza na busta...ila ndani ya baadhi ya hizi booster kuna kemikali inayozuru afya zetu...kama utaamua kutumia booster yoyote weka akilini kuwa ndani ya booster kuna kemikali. Hivyo kwa ushauri wangu ni bora mkulima ukatumia mbolea asilia, na maji....dawa usitumie mara kwa mara.
Tumia dawa wakati wa kuandaa shamba.
Tumia dawa kukinga magonjwa ya ukungu.
Tumia dawa kuangamiza wadudu waharibifu.
Tumia dawa kutibu miche iliyoathirika.
Ila dawa isitimike kwa kiwango kikubwa...na hakikisha unafata maelekezo ya dawa yaliyopo kwenye kibandiko.
Kama utaihudumia miche ya nyanya vizuri kwa kuweka mbole pindi inapohitajika, kumwagia maji japo kwa wiki mara tatu...na hakikisha siku za kumwagia unamwagia asubuhi na jioni...Nyanya inaweza kuanza kutoa Vitumba (maua) ndani ya wiki ya 5 hadi ya 6 tuu tokea ulipoipanda.
Unapopuliza madawa kuwa makini sana maana kipindi ambacho nyanya imeanza kutoa maua ni kipindi ambacho nyanya inahitaji uangalizi wa hali ya juu wanaita (INTENSIVE CARE)...kuna baadhi ya dawa ni marufuku kabisa kugusa maua hayo kwani hukausha kabisa hayo maua....
Zao hili lina faida sana ukinunua mbegu kutoka kwa wauzaji makini unaweza kupata zaidi ya kilo 5 kwa kila mche japo zipo mbegu zinazo zaa hadi kilo 12 na kuendelea na zipo pia mbegu ambazo ukianza kuvuna na ukiihidumia vizuri unaweza kuvuna zaidi ya miezi 6 hadi mwaka.
Hasara kwenye kilimo cha nyanya mara nyingi husababishwa na uzembe....nasema ni uzembe kwasabu wengi tumejikuta tunakimbilia kilimo kwakuwa jirani amenunua pikipiki kwaajiri ya kilimo...na watu wengi husifia faida waliyopata pasipo kueleza na hasara walizopata....hivyo ukipiga dawa isiyosahihi upo uwezekano wa kuikosa miche yote.

Ukiweka mbolea vibaya upo uwezekano wa kuiunguza miche yote.

Usipo mwagia maji unaweza kuipoteza miche yote.
Usipo weka dawa kwa wakati unaweza kupoteza miche yote, hivyo ni jukumu letu wakulima kuzingatia uwekaji sahihi wa mbolea...kuzingatia uwekaji wa maji si lazima umwagie maji mengi eti ili kesho usimwagie mwagia majo kiasi cha kutosha ila usimwagie maji hadi matope yatapakae huku na huko, nyanya haihitaji maji kwa muda mrefu, itaoza. Weka dawa kwa wakati.hapo utashinda na utapata faida ya uhakika.

Nimeona nichangie mawazo yangu juu ya kilimo hiki cha nyanya. Nakaribisha maoni

Mungu akubariki sana.

Mimi ni mkulima wa nyanya na mpunga kijiji cha Mbigili, Dumila mkoani Morogoro. Wakulima wenzangu wa nyanya, tubadilishe uzoefu wa kilimo hiki kuhusu mbegu, mbolea, magonjwa, madawa na masoko.

Karibuni sana!
Hongereni wakulima wa nyanya, nimeona first page mambo ya mbegu naomba nichangie.

Ukulima nyanya hybrid/chotara au unalima za kawaida/opv, tambua huduma zake ni sawa, yaani kiasi cha dawa, mbolea, maji, muda wa palizi, vibarua, shamba kama la kukodi bei ni ile ile tofauti iliyopo kati ya kutumia mbegu chotara na mbegu ya kawaida ni mosi bei mbegu chotara ghali kuliko za kawaida na pili mavuno mbegu chotara ina mavuno mengi sana kuliko za kawaida na other advantage chotara inauvumilivu wa magonjwa kuliko za kawaida.

Huwa iko hivi kulima nyanya ya faida kwa asilimia Mia moja za mavuno basi asilimia 10 inatoka kwenye mbegu na asilimia 90 inatoka kwenye huduma. Hivyo unapoona mbegu chotara ghali ukanunua za kawaida tambua umeshajiandaa kupata hasara sababu huduma ni the same.

Tuondoke kwenye kulinganishiana maeneo yaani alielima pakubwa ndiyo mkulima, la! tuje kwenye kulima eneo ambalo unaweza kuhudumia vyema na unapata mavuno bora basi utafanikiwa.

Kama unalima let's say jarrah rz unapata crate 1000 kwa ekari (ndio uzao wake) na mwingine analima rio grand akapata crate 200 kwa ekari na muda Huo Huo uduma sawa sawa kote basi alielima jarrah atapata faida hata kama nyanya itauzwa elf 10 kwa crate na alielima rio grand atapata hasara hata crate likiuzwa elfu 40.
Habari

Vipi umepima udongo wa kwenye green house?

Muhimu upime haswa kujua kuhusu magonjwa haswa ya mnyauko bacteria au fungus hii itakuepusha na hasara kubwa sana ya baadae, ili kama kuna matatizo basi ujue utatumia system gani ya kilimo kama utasia direct kwenye udongo au kama utatumia mifuko na udongo wa kutibu.

Ukiwa na udongo usio na matatizo yoyote na ukipata mbegu bora unaweza vuna nyanya kwa miezi sita mpaka nane kwa hapa tunapoenda bei ya nyanya itashuka from mwezi wa nne mpaka wa tisa hivi na wewe ukisia sasa hivi utaanza kuvuna from mwezi wa tano ukiitunza vyema mpaka November au December means wakati bei inapanda na wewe ndio utakua umemaliza kuvuna kama vipi tazama soko kwanza la nyanya, hoho au tango sababu ukiweka tango ni miezi mitatu atleast mpaka kuisha hivyo baada ya kutoa tango unaweza sasa ukaweka nyanya. Tazama soko kabla hujaweka kitu sema pia unalimia mkoa gani wenyeji watakupa details zaidi za uliko pia, mimi niko Arusha kipindi hiki watu wanaandaa mashamba ya nyanya za miradi, huwa zinavuruga soko sana.

Mbegu bora

Tango:

Mydas -rijk zwaan
Massa - rijk zwaan

Tango ya green house lazima iwe parthenocapic yaani isiyohitaji uchavushaji sababu kwenye green house hakuna nyuki ukipanda variety ya tofauti na hizo hapo juu utakua umeotesha maua tu.

Nyanya
Tylka - syngenta
Monteazul -rijk zwaan
Victory -east west seed
Anna f1 etc

Nyanya lazima iwe nyanya ndefu (indeterminate) kwa mavuno ya muda mrefu.

Hoho

Red jet
Pasirella
Ilanga (rijk zwaan)
Balton pia wanazo za rangi
Syngenta pia wanazo

Inabidi ulime za rangi ili usiwe na mzigo sawa na wanaolima nnje
Njia za kulima ni sababu ya unyeshaji sasa bila mfereji au matuta utatumia njia gani ya unyeshaji?

Mfereji pima mfeje hadi mfereji cm 140 mpaka 150 upandaji nyanya hadi nyanya cm 50 na mstari hadi mstari ni cm 150 (ikiwa umepanda mistari miwili kwenye mfereji au mmoja yote inahesabika kama mstari mmoja)

Matuta upana wa tuta ni mita moja na mfereji kati ya tuta moja mpaka lingine ni sm 50.

Juu ya tuta nyanya unaweka sm 50 mche hadi mche na kwenye tuta ukiweka mistari miwili weka sm 75 kati yake au sm 50 ukipanda zigzag juu ya tuta.
 

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,074
2,000

Hapo mkulima kapatwa mche umenawiri umeanza kuonyesha manufaa, wadudu waharibifu wamefanya yao. Hakuna jinsi ni kuung'oa tuu huku bado ukiwa unauhitaji mche wako, unaweza ukalia.
 
  • Thanks
Reactions: cpt

Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,074
2,000
Mkulima amepatwa hapo....wadudu....wadudu wanaweza wakakuliza...fangas imeushambulia huo mmea...umeshambilia mirija ya maji...mmea hauwezi kupitisha maji...
 

Michh

Member
Jan 7, 2015
26
45
NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa....kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji

Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na kusahau kujadili kuhusu HASARA zisababishwazo na kilimo cha zao hili.


Kiukweli NYANYA inaweza ikakutoa ukafanikiwa ki maisha ila inaweza vile vile ikakupa hasara kubwa ukajuta kufanya kilimo cha zao hili.

Andaa matuta vizuri lakini naomba nikwaMbie ndugu msomaji kila aina ya Tuta ina mahala pake na ardhi yake maalum hivyo ni bora kuichunguza ardhi yako vizuri maana kwa udongo wa kichanga ukiweka matuta ni dhahiri udongo utapelekwa na maji...kipindi cha kumwagilia.


Zingatia nafasi katika upandaji wa zao hili la nyanya nafasi inayopendekezwa ni cm50 kutoka mche hadi mche mwingine .... usipande zao hili pasipo kufuata kanuni ya nafasi ya cm50 maana zao hili lina majani na ukipanda kwa kubananisha sana utasababisha joto kuzidi, vile vile matawi yakigusana kutoka mche mmoja kwenda mche mwingine unaweza kusababisha miche iambukizane magonjwa.

Kwa kawaida zao hili huchukua siku 72 hadi 120 kupanda hadi kuanza kuvuna...
Zao la nyanya ni zao linalofyonza sana rutuba hivyo hakikisha ardhi unaiboresha kwa kuiweka mbole mara kwa mara...kwa mbolea za dukani Urea, dap, N.p.k, can na nyinginezo hakikisha unafuata maelekezo ya mtaalaam kabla ya kutumia hizo mbolea...mbolea ya Samadi au za mifugo hakikisha mbolea hizo ziwe zimekauka kabisa ziwe kama unga au kavu maana mbolea za mifugo zikiwa mbichi zitasababisha miche kuungua...na inaweza kudumaa pia.

Nyanya inashambuliwa sana na wadudu ambao hupelekea zao hili kupata magonjwa hivyo kabla hujapanda zao hili hakikisha unaanda shamba na kupiga dawa za wadudu pamoja na dawa za magonjwa za ukungu. Ni vigumu sana kutibu nyanya pindi utakapoanza kuona dalili kwenye mche ulioathiriwa na magonjwa. Hivyo kipindi chote cha uhai wa nyanya ni lazima kuzingatia matumizi ya dawa.

Endapo utagundua baadhi ya miche imepata maambukizi muone mtaalam wa madawa akushauri ukishindwa kuutibu ni bora ukaung'oa uo mche maana nayo huambukizana magonjwa kama tunavyoambukizana binaadam.

Uhai wa nyanya unategemea Maji, Mbolea na Dawa japo baadhi ya wataalam hushauri kuongeza na busta...ila ndani ya baadhi ya hizi booster kuna kemikali inayozuru afya zetu...kama utaamua kutumia booster yoyote weka akilini kuwa ndani ya booster kuna kemikali...
Hivyo kwa ushauri wangu...ni bora mkulima ukatumia mbolea asilia, na maji....dawa usitumie mara kwa mara...
Tumia dawa wakati wa kuandaa shamba...
Tumia dawa kukinga magonjwa ya ukungu...
Tumia dawa kuangamiza wadudu waharibifu...
Tumia dawa kutibu miche iliyoathirika...
Ila dawa isitimike kwa kiwango kikubwa...na hakikisha unafata maelekezo ya dawa yaliyopo kwenye kibandiko.

Kama utaihudumia miche ya nyanya vizuri kwa kuweka mbole pindi inapohitajika, kumwagia maji japo kwa wiki mara tatu...na hakikisha siku za kumwagia unamwagia asubuhi na jioni...Nyanya inaweza kuanza kutoa Vitumba (maua) ndani ya wiki ya 5 hadi ya 6 tuu tokea ulipoipanda.

Unapopuliza madawa kuwa makini sana maana kipindi ambacho nyanya imeanza kutoa maua ni kipindi ambacho nyanya inahitaji uangalizi wa hali ya juu wanaita (INTENSIVE CARE)...kuna baadhi ya dawa ni marufuku kabisa kugusa maua hayo kwani hukausha kabisa hayo maua....

Zao hili lina faida sana ukinunua mbegu kutoka kwa wauzaji makini unaweza kupata zaidi ya kilo 5 kwa kila mche japo zipo mbegu zinazo zaa hadi kilo 12 na kuendelea...na zipo pia mbegu ambazo ukianza kuvuna na ukiihidumia vizuri unaweza kuvuna zaidi ya miezi 6 hadi mwaka.

Hasara kwenye kilimo cha nyanya mara nyingi husababishwa na uzembe....nasema ni uzembe kwasabu wengi tumejikuta tunakimbilia kilimo kwakuwa jirani amenunua pikipiki kwaajiri ya kilimo...na watu wengi husifia faida waliyopata pasipo kueleza na hasara walizopata....hivyo ukipiga dawa isiyosahihi upo uwezekano wa kuikosa miche yote....
Ukiweka mbolea vibaya upo uwezekano wa kuiunguza miche yote...
Usipo mwagia maji unaweza kuipoteza miche yote...
Usipo weka dawa kwa wakati unaweza kupoteza miche yote...hivyo ni jukumu letu wakulima kuzingatia uwekaji sahihi wa mbolea...kuzingatia uwekaji wa maji si lazima umwagie maji mengi eti ili kesho usimwagie mwagia majo kiasi cha kutosha ila usimwagie maji hadi matope yatapakae huku na huko...nyanya haihitaji maji kwa muda mrefu...itaoza....
Weka dawa kwa wakati...hapo utashinda na utapata faida ya uhakika....
Nimeona nichangie mawazo yangu juu ya kilimo hiki cha nyanya .....nakaribisha maoni
MuNgU akubariki sana.


Mungu akubariki!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom