JF members mnaokaa Kivule tujuane, tutatue matatizo yetu

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania kama kuna;

JF Members mnaokaa kata ya Kivule karibia na Kitunda huku Dar ninaomba tujuane hapa.

Nimeamua kuwaomba tuonane hapa kwa maana kwamba ndani ya mtaa na kata yetu hii kuna changamoto nyingi sana kuanzia suala zima la usafi wa mazingira, ubovu wa barabara, mimba za utotoni, wazazi kugoma kupeleka watoto shuleni pamoja na nyingine nyingi sana ambazo zinahitaji nguvu yetu ya pamoja kama wana Kivule katika kuzizatua.

UMOJA NA NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

OUR MOTTO:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

View attachment 1519606

PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
Kweli nina shamba langu maeneo ya hospitali mpya. Leta mwongozo
 
Back
Top Bottom