JF kuna upapasi

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Mitambo yangu inaniambia kuwa hapa JF kuna vidudu vya upelelezi na ukitumia spyterminator utaona ,mambo mambo na harakati ,sasa sijui kama imeshanunuliwa na usalama wa Taifa na kuanza kutumika upapasi.sijui wengine mnaosurf mna onaje ?
 
Last edited by a moderator:
Mitambo yangu inaniambia kuwa hapa JF kuna vidudu vya upelelezi na ukitumia spyterminator utaona ,mambo mambo na harakati ,sasa sijui kama imeshanunuliwa na usalama wa Taifa na kuanza kutumika upapasi.sijui wengine mnaosurf mna onaje ?
Utasema kila aina ya vitu mwaka huu... fainali mwakani!
 
Mitambo yangu inaniambia kuwa hapa JF kuna vidudu vya upelelezi na ukitumia spyterminator utaona ,mambo mambo na harakati ,sasa sijui kama imeshanunuliwa na usalama wa Taifa na kuanza kutumika upapasi.sijui wengine mnaosurf mna onaje ?

Nadhani kuna msemo usemao maneno yafananayo na (nimesahau) "kuku ukimchunguza sana hutamla". Kwani nani kakuambia hiki sio chombo cha Usalama wa Taifa tangu mwanzo?

Cha muhimu ni kwamba hiki chombo kinajenga taifa. Hata kama ni cha Usalama wa Taifa bado ni kizuri. Kama wanakitumia kuona kuna nini kwenye mashine yako, usijali sana. Au una mipango ya ajabu ajabu kwenye mashine yako?

Mie nadhani JK aliahidi kuanzisha website ya Watanzania. Kwani si hii? Wee unadhani habari moto moto tunazopata hapa zinaweza kupatikana bila msaada wa Usalama wa Taifa?

Usalama wa Taifa wanaweza kuwa wanajenga taifa kwa njia hii. Kuna mbaya gani?
 
usiogope usalama wa taifa wewe toa hoja watu wachangie, hapa jf tupo kujenga si kubomoa na pia hao usalama nao wanataka habari ili watambue yanaoendelea so usiogepe endelea kutoa maoni yako mzee,
 
Mie nadhani JK aliahidi kuanzisha website ya Watanzania. Kwani si hii?
Na siku JK akijua anayeendesha chombo hiki sijui itakuwaje... Mkuu Augustine, website ya JK aliyowaahidi watanzania hajaianzisha bado!

Ninachoelewa ni kuwa kuna watu walikuwa wakibonyeza "Thanks" inawapeleka kwenye page ambayo inaonesha hawana access na page hiyo... Mmojawapo anaweza kuwa Mwiba!

Njia rahisi ya kuondoa tatizo hilo ni ku-clear caches na cookies kwenye pc yako.

Hold CTRL+Click Refresh then utaona changes nyingi ambazo zimetokea JF.

Poleni ambao mmeathirika na changes hizi
 
Isije ikawa huyo Mwiba ndio jasusi, na ameanzisha thread hii kusikilizia upepo unaendaje !!
 
Iwe usalama isiwe usalama mie hainihusu, Ninachoijali sana ni elimu na habari nivipatavyo humu. Unajua kuna raha na ni sanaa ya aina yake kufanya mkutano gizani ambapo masikizana kwa sauti ila hamuonani and woote ni strangers na baada ya mkutano kila mmoja anasepa kivyake. Raha sana maana unaweza kusikia sauti inasema ujinga na nyingine inatema busara bila kutambua ni nani. Sana sana nawashukuru Mods wa JF kwa kuficha na kutunza heshima zetu kwani tungejuana huko mtaani kwa nicks zetu nadhani mibuyu itang'oka 2010... I mean vigogo vilaza wataenda na mafuriko...
Invisible kula tano
 
upapasi wot does it mean? kiswahili kinakua.

duh! kweli wa-St. Mary's International School tupo wengi............hadi na wewe Senior hujui maana ya UPAPASI...........ngoja tumcheki Prof. Amandina Lihamba awe anatupa kozi ya kiswahili hapa.........Au vipi JEFF?
 
msiogope,toa michango wadau!! Nothing good comes easy.Hivi kuna wesite nyingine zaidi ya hii ya kutoa maoni yetu? Mimi naisubiri saana kwa hamu website ya president
 
Kwa kuwa hakuna nia mbaya na nchi yetu naamini wale watu safi ndani ya usalama wanaichukulia JF kama sio tishio lolote kwao.Kazi ipo kwa wale wenye ajenda za kujirutubisha wenyewe!Inshallah tutafika tu.
Mungu ibariki tanzania
 
Nadhani kuna msemo usemao maneno yafananayo na (nimesahau) "kuku ukimchunguza sana hutamla". Kwani nani kakuambia hiki sio chombo cha Usalama wa Taifa tangu mwanzo?

Cha muhimu ni kwamba hiki chombo kinajenga taifa. Hata kama ni cha Usalama wa Taifa bado ni kizuri. Kama wanakitumia kuona kuna nini kwenye mashine yako, usijali sana. Au una mipango ya ajabu ajabu kwenye mashine yako?

Mie nadhani JK aliahidi kuanzisha website ya Watanzania. Kwani si hii? Wee unadhani habari moto moto tunazopata hapa zinaweza kupatikana bila msaada wa Usalama wa Taifa?

Usalama wa Taifa wanaweza kuwa wanajenga taifa kwa njia hii. Kuna mbaya gani?

Naona mdau wa JF anaogopa sana kutoa hoja zake. JF hakuna upapasi wala upaparazi, we toa tu hoja zako.
 
afadhali upapasi uwepo.
Itasaidia coz here we dare talk openly.
Labda mambo kadhaa yatakuwa sorted....
tusiogope jameni
 
Hakuna anaeogopa hapa .na kwa vile nina asili ya Pemba naamini kabisa haki inadaiwa na kuhakikishwa kuwa inapatika kwa bei yeyote ile,kukubali kukaliwa kimabavu bila ya faida ni hasara kwa vizazi vijavyo na kurudishwa utumwa chini ya mkoloni mweusi.
Tulidai Uhuru ili kujikomboa na kuondokana na tabu za wakoloni weupe ,tuliamini kuwa sasa tutakula matunda ya uhuru lakini tuzipatazo ni sijui ni hasara au ni faida ,lakini majibwa yanafaidika sana yanapofugwa japo hutumika kuwinda ,ila yanapoachiwa na kuwa koko ,uhuru walio nao ni kupigana wenyewe kwa wenyewe na kuuwana ndio ukawakuta wengine hawana mikia wengine hawana macho. Tunaendelea kurapu ,nilikuwa nauliza tu ila naona majawabu yamekuwa mengi.

Nilitegemea nitaambiwa wapo au hawapo ,kwisha, sasa iliyotokea ni kubabaishana ,ninavyofahamu web huweza kutumika kuwanasa au kuwachunguza wengine ,na mwenye webu atakuwa na taarifa au atakuwa anatumiwa kuruhusu kukiz za upepelezi kuwekwa kwenye webu yake ,ndio maana yake.
 
Hilo lisikushangaze hao jamaa mnaowaita usalama wa taifa, ambao mimi nafikiri wakati mwingine tungewaita usalama wa tabaka tawala wapo kila mahari kwani kazi yao ni kukusanya habari kila mahari na kuwapelekea mabwana wao ambao ni tabaka tawala. JF ni moja ya chombo ambacho kadili yangu kinatoa elimu, kuburudisha na kuhabarisha watu. Lakini upande mwingine ni tishio kwa tabaka tawala kwa sababu habari nyingine wanazopata wanaJF pengine ni siri ya tabaka hilo na hivyo kadili yao hayo huweza kuhatarisha usalama wa taifa au tabaka hilo. Hivyo kifupi ndugu yangu usiwaogope hao jamaa kwani wapo kila mahari. kama upo ofisini jua wapo pia, huwa wanafuatilia sana hii mitandao. kuna mwalimu wangu pale Mlimani alizoea kututania kwamba katika kila watu 10 kuna mtu mmoja wa usalama. usiwajari na usiwaogope, hao jamaa kama kweli wangekuwa wanamsaada sana kwa nchi iliyo maskini sana, mafisadi wasingekuwa wameifilisi nchi kiasi hiki kwani habari za maovu hayo zingewafikia wahusika, ukweli ni kwamba hao jamaa hapa TZ wanachofanya ni kulinda maslahi ya tabaka tawala na sio taifa. Kuna website fulani pia huwa zinafuatiliwa sana. Tembea nchi zote utakuta hayo habari ndio hiyo mzee!!!
 
Kila neno linaloandikwa lazima lithibitishwe. Lazima sababu itolewe. Isiwe kama shushushu anapotafuta maadui wa Serkali anapoingia bar,na kuanza kusema"JK ni fisadi,hafai kuongoza nchi.''Halafu anngoja kusikia nani ataafikiana naye,halafu anamkamata,amempata mbaya wa Serikali. Ndiyo mambo yanayotokea hapa JF. Inawezekana kuna upapasi katika JF.
 
Na siku JK akijua anayeendesha chombo hiki sijui itakuwaje... Mkuu Augustine, website ya JK aliyowaahidi watanzania hajaianzisha bado!

Ninachoelewa ni kuwa kuna watu walikuwa wakibonyeza "Thanks" inawapeleka kwenye page ambayo inaonesha hawana access na page hiyo... Mmojawapo anaweza kuwa Mwiba!

Njia rahisi ya kuondoa tatizo hilo ni ku-clear caches na cookies kwenye pc yako.

Hold CTRL+Click Refresh then utaona changes nyingi ambazo zimetokea JF.

Poleni ambao mmeathirika na changes hizi

Website ya wananchi ipo siku nyingi tu.....ila sijui kama imeshawahi kutangazwa kuwa ipo na inafanya kazi

Website ya Wananchi.JPG - Click on the picture to be taken to the website
 
nimetuma sana maoni lakini hakuna hata siku moja waliyorespond hata receipt ya post.
pili kama hawayatilii maanani maoni yetu humu sidhani itasaidia kwa mtu kujipendekeza kupost maoni yake ktk web hiyo.
tatu ni kwamba kama web ya state house haipo up to date unategemea uendeshaji wake upo makini kweli? nahisi ilikuwa zimamoto
 
Back
Top Bottom