Mi jumamosi ilopita yamenikuta mbona.
Tena nlikua napost kitu JF, milango ya saa 2 usiku.
Nipo kwenye taxi nyuma, na kioo nimeshusha. Yani akili yote imehama imehamia dunia ya JF.
Mitaa ya Jang'ombe zenji, dereva ka slow down kwa sababu ya mkanganyano wa magari. Nashtukiza kwapuuuu.
Nlivovinjari mtt wa kike, tulivutiana simu na kibaka mpk simu ilitoa mlio wa kudata.
Gemu lilienda kimya kimya, mana nguvu zote nlizihamishia mikononi basi hata kuongea sikuweza.
Nashkuru nlishinda, mana by the time dereva anakaza mwendo kibaka katoka mbio.
Ndani ya gari tulikua watu wa4 hamna alojua mpk nliporudisha pumzi na kuwahadithia.
Yani ilikua kama kituko flan ivi.