JF imenifanya niporwe simu!

JF imenifanya niporwe simu!

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
2,411
Reaction score
1,153
Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa barabara ya Kilwa.

Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote.

Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku milio ya honi ikiwa imepamba moto.

Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu.

Nilirudi kwenye gari huku nikiwa nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!.

Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
 
Pole sana mdau.
Sijui tupitishe kampeni tukuchangie jamani. Nahofia kukumiss hapa
 
Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa.....

mkuu mbona kichwa cha habari akiendani na ulichokiandika ndani...?!!!
 
....barabara ya Kilwa. Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile...
 
....barabara ya Kilwa. Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile...

Masikini ya Mungu, wameshakwapua na hii kabla hujamaliza kuandika, pole sana bwana.
 
...simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote. Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku....
 
...milio ya honi ikiwa imepamba moto. Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu. Nilirudi kwenye gari huku nikiwa....
 
...nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!. Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
 
Pole sana mkuu huo uizi ni maarufu sana hapa Dar na wengi wamelizwa sana...bahati mbaya watu wengi huwa wagumu kujifunza...

Ruhazwe JR lile bandiko lako la onyo limepata muhanga wa kwanza...
 
Last edited by a moderator:
Hahaha! Mburula kweli wewe.
Ulipaki gari barabarani na unasema ulikuwa kwenye daladala. Ama wewe profeshenale nindereva wa ma3?

Cc watu8
...nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!. Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom