JF imenifanya niporwe simu!

JF imenifanya niporwe simu!

Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa barabara ya Kilwa.

Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote.

Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku milio ya honi ikiwa imepamba moto.

Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu.

Nilirudi kwenye gari huku nikiwa nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!.

Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
Mkuu,
Unyanidume wako ndio umekufanya uibiwe simu na sio JF. Au inawezekana hauna utaratibu wa kutoa fungu la kumi au Sadaka kwa Muumba wetu. Ugua pole na Mungu akujaalie Upate iPhoneTecno6.
 
Dah...........My God! pole sana Nyanidume, umenikumbusha machungu ya simu yangu Nokia N97 iliyoporwa Ubungo kwa namna hiyohiyo,pole sana mkuu
Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa barabara ya Kilwa.

Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote.

Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku milio ya honi ikiwa imepamba moto.

Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu.

Nilirudi kwenye gari huku nikiwa nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!.

Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
 
Last edited by a moderator:
Dah Natamani lile bandiko langu lingepitiwa na kila Mtanzania,ili hawa wezi wakose cha kupora........maskini Nyanidume R.IP Simu yetu
Pole sana mkuu huo uizi ni maarufu sana hapa Dar na wengi wamelizwa sana...bahati mbaya watu wengi huwa wagumu kujifunza...

Ruhazwe JR lile bandiko lako la onyo limepata muhanga wa kwanza...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Unyanidume wako ndio umekufanya uibiwe simu na sio JF. Au inawezekana hauna utaratibu wa kutoa fungu la kumi au Sadaka kwa Muumba wetu. Ugua pole na Mungu akujaalie Upate iPhoneTecno6.
Ahsante!
 
Dah...........My God! pole sana @Nyanidume, umenikumbusha machungu ya simu yangu Nokia N97 iliyoporwa Ubungo kwa namna hiyohiyo,pole sana mkuu
Kumbe na wewe yalikukuta kama mimi yaliyonikuta? hakika inauma sana!
 
Dah Natamani lile bandiko langu lingepitiwa na kila Mtanzania,ili hawa wezi wakose cha kupora........maskini Nyanidume R.IP Simu yetu
Mkuu bahati mbaya sikubahatika kuliona hilo bandiko!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu una moyo! Uliacha gari barabarani ukaanza kufukuzana na kibaka aliyekuibia simu?? Uliporudi kwenye gari ulikuta kila kitu salama???[emoji848][emoji848]
 
Back
Top Bottom