JF Exclusive: The Buzwagi Contract

"provided that the aggregate of such local Government rates and taxes charged shall not exceed United States Dollars Two Hundred Thousand (US$ 200,000) in any one calendar year"

Wakuu mimi sio mtaalamu wa haya mambo ya hazina, lakini naamini kuwa ninakielewa vizuri hi kipangele kuwa ni a big joke! Sio tu kwa sisi wananchi bali hata viongozi wenyewe wanaotuongoza ambao sidahni kuwa walikuwa wameuona huu mkataba!

Shukrani kwa wale wote walioshiriki kutuletea hii kitu ambayo kwa kweli ni sabuni ya roho!
 
Mzee mwenzangu, kama wenye mgodi wangejua kuwa viongozi wetu wanaweza kusema hapana, they could not have dared to come up with such an arrogant a clause! Halafu tukiambiwa kuwa huu ndio ulioboreshwa zaidi.. then I can only imagine.. hiyo mingine imeweka kiwango gani..
 
Mkjj hata mie najiuliza hili swali mara mia...

kama huu mkataba ndio umeboreshwa, je hiyo mingine ikoje?

kuna sources zangu zinajaribu kufuatilia mikataba mingine yote ya madini..... ccm sasa hivi imegawanyika mno na nina uhakika nitapata hata hiyo mingine yoote!

ni aibu tupu.... ndio maana bungeni hawakutaka kabisa kusikia upinzani kuhusu huu mkataba maana walijua utawaumbua big time..

kazi kweli iko mbele huko!
 
Ninaupitia mkataba huo huku nikiangalia sheria ya madini pia.. kuna mtu anastahili kufukuzwa kazi na kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi!
 
Kipengere cha 4.4 nacho kinatia kichefuchefu..

mhhhhh jamaa wameamua kufunga kila kitu.... hakuna kodi zaidi ya wanayotaka wao.... hakuna cha michango wala nini! zingine zinaendelea hapa chini
 
Sisomi tena mikataba yenu mnayoweka online, yaani imenitia aibu kweli. I tried to take mkataba huu kama basis ya kutokea yamenikuta ahahaa

Baada ya kusoma mkataba huu, nimeandika barua kuwa kuanzia this month I won't pay any rent if I spend more than 2 days out of my house. Also if in any calendar yr, I spend more than three weeks out of my house, then the rent can not exceed half of a normal calendar yr rent. ahahaha

Yaani karibu nifungwe ahahahahahha

Jamani don't use this mkataba kama basis ya chochote unless unadeal na wagonjwa wa akili. Du
 

kwi kwi kwi kwi kwi kwi inabidi tu nicheke ....
 
Sasa kifungu hiki kwanza kieleweke ili tuendelee kwa wale wanayoijua sheria yake.

'Expatriate Employee' means a person not normally resident in Tanzania and who is engaged under a contract subject to the grant of a resident Permit.
Hiki kipengele kina utata mkubwa hawa expatriates ambao wanaombewa misamaha ya PAYE hatuwataki Tanzania. Mbona nchi zilizoendelea wanawatoza kodi wageni wote sawa na raia tu. Sisi Tanzania tunawapa pesa nyingi halafu tunawasamehe kodi - Ujinga gani huu?
'Year of production' means, in relationto the Contract Area, the production from the Mine of a minimum of 20,000 ounces of gold contained inore or concetrate, as the case may be, during the applicable calendar year.
Yaani wasipopata hizo ounces 20,000 mwaka bado kutimia kweli nazi kara mavi sio bure. Sasa bei yake hizo ounces 20,000 ni sawa na $144,000,000 kwa bei ya $720 hivi sasa
Angalia utata hapo pamoja na kufuta kwa nazi Karamagi na hapo hapo ati kodi isichajiwe kutokana na production? Uliona wapi mambo kama haya?

Mwenye Special Mining Licence pamoja na the income Tax Act No. 11 of 2004 pia the Customs Tarrif Act No. 12 of 2006 atuwekee hapa tuendelee ku-enjoy huu muziki.

Bado naendelea kuusoma
 
Mwanakiji kama unao huo Mkataba naomba nitumie nami nitauweka ONLINE ili wengi zaidi wauone na kuu-download..
 
4.4 inaendelea hapa,... kumbuka ilivyoanza!

Take note of the word - NOT

4.5 itaendelea hapa chini ......
 
anayeutaka naomba e-mail yake then nitamtumia kesho,ninao ktk pdf format..niliupata leo asubuhi!
hata kama unawakilisha pata chombo chochote bure<pccb> NA Usalama utaupata bila usumbufu,
 
Good Job Waungwana!Kama wanavyosema Wataalamu humu, Kumkoma Nyani Giladi,Nasikia huko Dar kila Ofisi ilipata nakala ya "Thisday". Najua watu wengi wataingia JF kuona huu Wimbo wa Boys II Men.Aluta Continua.Mambo yote hapa hapa Mchana Kweupeeee!!
 
Nakuomba usome vipengere vifuatavyo ukiwa umekaa chini la sivyo unaweza kuanguka kwa hasira na kuumia kwa huzuni
 
kwi kwi ,natamani nimuone karamagi nimpomde jiwe kwenye paji la uso,
mwanakijiji kesho mtafute katibu wa wizara ya nishati aeleze empowerment fund ni nini, na mpaka sasa imewanufaisha wana wa watanzania wangapi?
sitaki kuamini wataalam na wanasheria wa nishati hawakuona uhujumu uchumi huu,
sitaki kuamini mwanasheria wa siku nyingi mhe. Ngeleja<naibu waziri> hakuona utumbo huu,
sitaki kuamini JK anaangushwa na watendaji wake,
simtaki karamagi
 
mhe. geeque kesho utaupata mkataba saa 4 kwa saa za zimbabwe,
 
Inaendelea chini bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…