JF EXCLUSIVE: DOWANS vs TANESCO, the saga continues!

Mkuu Salute. At least I can now appreciate what JK meant when he said the country has no competent poeple in contract laws. It seems that you are very conversant with these issues. I, among many here, are ignorant of all the references you have made here, which, they make a lot of sense. What i want to know from you learned brother is that in such a situation, what is the way out for Tanesco and tanzania as a country in this case?

Mkuu I don't agree with what President Kikwete said, if he really said that. We have very competent lawyers in our country. The problem is we don't use them. Tuna maprofesa wazuri tuu on contractual issues. Tofauti na watu wanavyofikria, the issue does not lie with the agreement between Dowans and Tanesco. Issue iko kwenye sheria yetu ya arbitration. Inasema kuwa uamuzi wowote utakaotolewa na Tribunal utakuwa wa mwisho. Hii ina maana hautatenguliwa na mahakama yoyote ile.

Sasa wakati Tanesco wanaingia kwenye mkataba na Dowans, what they did was to copy and paste the clause from our arbitration Act to the effect that the arbitral award should be final and binding. Kama sheria yetu ingekuwa updated kwa kuondoa neno "final", then wasingeweza kukubaliana kuwa the award should be final.

On what is the way out for Tanesco and Tanzania as a country in this case, the answer is simple: there is no a way out. We have to pay Dowans the amount awarded by the Tribunal. The more we delay making the payment, the more it will cost us. Imagine kwa hii kesi tuu Tanesco imeamriwa kulipa dola milioni 5 kama security ili kuhairisha kesi mpaka Decemba 2011. Bado hujaweka gharama za kumwajiri mwanasheria ya Uingereza kuwakilisha Tanesco mahakamani. Where will Tanesco get this money wakati hawana hata umeme wa kuuza?
 
dawa ni ubabe,kisheria hatuwezi,kama mkuu wetu wa nchi yupo tayari tuitaifishe kibabe na kuvunja mahusiano na hiyo mahakama full stop!
@MTAZAMO, nakubalina na wewe kabisa.Tukienda kwa mtindo wa kufuata sheria tutadumbukia kuzimu. Hapa solution ni kufanya 'street law' kwamba hatulipi hata cent moja, na kama ni kutaifaisha mali za TANESCO zilizoko Uingereza na sisi tufanye hivyo hivyo hapa - jino kwa jino, liwalo na liwe. Inabidi tujilipue na kuwa maskini jeuri vingenevyo tutakamuliwa damu!

Wakuu huwezi kufanya ubabe kwenye hili suala. This is an international issue. Tanzania tume sign mikataba ya kimataifa na kukubali kuwa tutaheshimu hukumu ambazo zimepitishwa na mahakama za nje. Kama hatutaki then tujiondoe kwenye hiyo mikataba kwanza. Na ukisema uende kibabe, Tanzania is ina assets abroad? Thats is exactly what Dowans wants to do. Kwa vile tayari tumeshaleta ubabe nyumbani, Dowans wants to execute our assets abroad. Kama tunao ubabe basi tuhamishe assets zote na kuzirudisha nyumbani.

FJM kumbuka atakayetaifisha mali zetu ni Dowans na wala sio serikali ya Uingereza. Serikali ya Uingereza haihusiki hapa. After all sisi ndio tulichemsha wenyewe tuliposaini mkataba. Kwa nini leo tusilipe?

IKO kisheria sana tungepata Mtaalam wa Lugha za kisheria atutafunie sisi wabeba zege maana shule zenyewe tumesoma St CCM, Chuo tumefundishwa na waadhiri walofail, wale wazuri wooote wako kwenye Siasa...

Mkuu pitia post ya Pasco namba 21 hapo juu ameelezea vizuri na kwa kifupi.
 
Coach Parcells, kwa kifupi,
1. Baada ya ICC kuitioza Tanesco walipe zile US$65m plus interest ambazo zinaitwa tozo za Dowans.
2. Tozo hiyo inapaswa isajiliwe na Mahakama Kuu hapa nchini ili iweze kuwa enforceble by lacal laws, yaani Tanesco wawajibike/kulazimishwa kulipa.
3. Kabla mahakama kuu haijatoa uamuzi wa kuisajili tozo hiyo, tayari kuna kesi nyingine 4 zimefunguliwa mahakama kuu kupinga kulipwa kwa tozo hiyo.
4. Hivyo uamuzi wa mahakama kuu kuisajili tozo hiyo unaweza kuchelewa mpaka Desemba 2011 au zaidi ili kuzosikiliza pingamizi hizo.
5. Ili mshitaki Dowans asizidi kupoteza haki zake, ameipandisha Tanesco kwenye mahakama ya Uingereza, akiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kukazia hukumu ya ICC, kwa kuiomba itoe kibali cha kuzishika mali za Tanesco zilizoko Uingereza au Jumuiya ya Ulaya ili mali hizo zitumike kama dhamana/security ya kuishinikiza Tanesco kulipo tozo husika.
6. Hiyo mahakama hiyo ya Uingereza imeitaka Tanesco kulipa Dola Milioni 5 zitumike kama security kusubiri uamuzi wa Mahakama kuu ya Tanzania kuisajili tozo ya Dowans.
7. Mahakama hiyo imeridia msimao wa mkataba ule ambao kwa ridhaa yao wenyewe waliamua uamuzi wa ICC ndio wa mwisho na haukutakiwa kupingwa wala kucheleweshwa.

My Take.
Wana bodi wenzangu, hii ni issue ya kisheria na sio kisiasa, nawashauri tupunguze kidogo politics kwenye masuala ya kisheria. Niliwahi kusisitiza, ule mkataba ni mkataba bomu, Tanesco walijifunga na hawana pa kutokea dawa ni kulipa tuu!.

Ila pia naungana na hoja za Tanesco kuwa wao hawalipi kwa vile aliyewaingiza kwenye mtego huo ni serikali, hivyo ni jukumu la serikali kulipa na sio Tanesco.

Nyerere angekuwa ni rais wa nchi hii, tungevunja uhusiano na ICC, tusingelipa chochote!, mitambo tungetaifisha!, hao wawekezaji wa ulaya wangefungasha virago vyao na kwenda makwao wakatengeneze dhahabu na gesi zao huko viwandani kwao. Wachina wangetuletea teknolojia ya kuichimba dhahabu yetu, gesi yetu na mafuta yetu huku faida asilimia 100%, ikibaki ni mali yetu, kuliko sasa wanavyochimba hawa maharamia kwa jina la waweklezaji, wakikomba asilimia 98% huku wakituachia asilimia 2% eti ndio royality!.

Lakini kwa vile siye yeye,
waliopo wanaheshimu utawala wa sheria, wawekezaji ndio tunawanyenyekea na kuwalamba miguu, amini nawaambieni, Tozo tutalipa, tena sio Tanesco, bali serikali kwa kodi zetu!.

Mkuu Pasco: Napingana na wewe kwa nguvu zote kuhusu hapo nilipo-highlight na red. Serikali hii katu haina utawala wa sheria na mifano ambayo ipo ni mingi sana, nawe unafahamu fika. Hili suala la Dowans kwa kuwa linahusu ulipwaji wa pesa na kuna watu fulani humu nchini ni beneficiary, basi ndiyo kunaletwa hii ya kusema kwa kuwa utawala huu unafuata sheria, basi ni sharti tozo hiyo ikalipwa.

Kwa mambo mengine hatusikii kuletwa hiki kitu "utawala wa sheria". Serikali hii imekuwa ikikaidi hukumu za mahakama zake zenyewe hapa nchini zilizowekwa kikatiba na wala haijali, na wala akina Pasco hatujawasikia wakisema. Mfano ni kesi ya Valambia. Lakini kwa hukumu za mahakama za nje hata kama ni za binafsi kama vile hiyo ICC (isichanganywe hapa na ile ICC ya The Hague) basi serikali inakuwa na uchu mkubwa sana wa kulipa, na kuandaa wapambe chungu nzima kuipigia debe kwamba lazima utawala wa sheria ufuatwe.

Suala la pili ni serikali kutowachukulia hatua wale waliotufikisha hapo kwani wanajulikana -- akina Karamagi & co. Dola 65m ni nyingi sana kwa serikali kuingizwa mkenge na watu wachache. Jee, Pasco, kwa nini usiipigie debe suala hili kwamba serikali hii yenye kufuata 'utawala wa sheria' ni lazima iwafikishe mahakamani wachache hawa kwa kuliingzia taifa hasara?

Nawasilisha.
 
Kwa mara ya kwanza tanesco wameanza kuonyesha seriousness katika kutetea haki za wa-tz............................tatizo is this not a case of catching the plane after it had departed..??????

Nimefurahishwa na hoja za Mr. White.....................................kimsingi waendelee to the Courrt of Appeal in UK.........................sidhani kwenye mazingira ya tanesco v. dowans suala hili now is final and binding........................ukiangalia hoja za kimsingi za kuwa wanasiasa wakiongozwa na fisadi lowassa ..........they are above the procurement act........hoja ya kisheria ambayo pekee ilipaswa kumwongoza jaji mhusika kuona ya kuona the matter is still defeasible.............
 
Wakuu huwezi kufanya ubabe kwenye hili suala. This is an international issue. Tanzania tume sign mikataba ya kimataifa na kukubali kuwa tutaheshimu hukumu ambazo zimepitishwa na mahakama za nje. Kama hatutaki then tujiondoe kwenye hiyo mikataba kwanza. Na ukisema uende kibabe, Tanzania is ina assets abroad? Thats is exactly what Dowans wants to do. Kwa vile tayari tumeshaleta ubabe nyumbani, Dowans wants to execute our assets abroad. Kama tunao ubabe basi tuhamishe assets zote na kuzirudisha nyumbani.

FJM kumbuka atakayetaifisha mali zetu ni Dowans na wala sio serikali ya Uingereza. Serikali ya Uingereza haihusiki hapa. After all sisi ndio tulichemsha wenyewe tuliposaini mkataba. Kwa nini leo tusilipe?

kubwa hapa ni kuwa mahakama ya uk haijasema tulipe ila inataka tuweke rehani dola milioni 5 na uamuzi wao una utata na waweza kutenguliwa na UK court of appeal au House of the Lords..........................................so it is not yet over until it is truly over.........
 
Mkuu Pasco: Napingana na wewe kwa nguvu zote kuhusu hapo nilipo-highlight na red. Serikali hii katu haina utawala wa sheria na mifano ambayo ipo ni mingi sana, nawe unafahamu fika. Hili suala la Dowans kwa kuwa linahusu ulipwaji wa pesa na kuna watu fulani humu nchini ni beneficiary, basi ndiyo kunaletwa hii ya kusema kwa kuwa utawala huu unafuata sheria, basi ni sharti tozo hiyo ikalipwa.

Kwa mambo mengine hatusikii kuletwa hiki kitu "utawala wa sheria". Serikali hii imekuwa ikikaidi hukumu za mahakama zake zenyewe hapa nchini zilizowekwa kikatiba na wala haijali, na wala akina Pasco hatujawasikia wakisema. Mfano ni kesi ya Valambia. Lakini kwa hukumu za mahakama za nje hata kama ni za binafsi kama vile hiyo ICC (isichanganywe hapa na ile ICC ya The Hague) basi serikali inakuwa na uchu mkubwa sana wa kulipa, na kuandaa wapambe chungu nzima kuipigia debe kwamba lazima utawala wa sheria ufuatwe.

Suala la pili ni serikali kutowachukulia hatua wale waliotufikisha hapo kwani wanajulikana -- akina Karamagi & co. Dola 65m ni nyingi sana kwa serikali kuingizwa mkenge na watu wachache. Jee, Pasco, kwa nini usiipigie debe suala hili kwamba serikali hii yenye kufuata 'utawala wa sheria' ni lazima iwafikishe mahakamani wachache hawa kwa kuliingzia taifa hasara?

Nawasilisha.

Tawlingojea jibu lako Pasco kwa huyu Mandevu. Usiingie mitini kiulaini hivyo! serikali hii haifuati sheria zake hata kidogo.
 
kubwa hapa ni kuwa mahakama ya uk haijasema tulipe ila inataka tuweke rehani dola milioni 5 na uamuzi wao una utata na waweza kutenguliwa na UK court of appeal au House of the Lords..........................................so it is not yet over until it is truly over.........

Una maana uamuzi wa kulipa dola milioni tano kama sercurity ya kuhairisha kesi? If so, then Tanesco wanaweza kukata rufaa kwenye mahakama za Uingerezeza. Lakini mahakama za UK haziwezi kutengua uamuzi uliotolewa na ICC Tribunal. Pia for update, there is no longer the House of Lords. Siku hizi inaitwa Supreme Court. House of Lords imebakia kuwa sehemu ya bunge tuu.
 
Not necessarily, especially given the kind of legal language aka legalese applied here. The statements provided appear to be open to interpretation. That being said, you'll need to clarify as to the particular context(s) these statements allude to (according to you), and your own understanding of their legal meanings and/or consequences.

I am not a Lawyer Dude, I am a rare peasant!
 
FJM kumbuka atakayetaifisha mali zetu ni Dowans na wala sio serikali ya Uingereza. Serikali ya Uingereza haihusiki hapa. After all sisi ndio tulichemsha wenyewe tuliposaini mkataba. Kwa nini leo tusilipe?
.

Mkuu EMT, kwenye red; Hivi nani anamiliki Dowans? Ni Al-Adawi? au Symbion? Kama sikosei mwaka huu huu kuliwahi tolea amri na mahakama yetu kuwa Dowans wafanye maamuzi i.e kuuza mitambo (correct me if I am wrong) bila idhini ya mahakama. Hii ina nguvu yoyote?

Kwa ujumla Richmond/Dowans ni jinamizi ambalo kwangu naamini litapeleka CCM kaburini. Can you imagine sasa hivi baada ya wauza mafuta kuishikisha adabu serikali iseme italipa Dowans? Tayari Richmond ilisababisha Baraza la mawaziri kuvunjwa, sasa Dowans itasambaratisha chama. Na huyo aliachana na siasa uchwara ili kushughulikia biashara nadhani aliasahau/aliamua makusudi kutosema kuwa biashara yake kwa sasa ni 'kupanga' mijeledi tayari kwa minyukano ndani ya ccm. Watachapana kuliko.

Ushauri kwa ccm maana hakuna lisilowekezana kwa hawa wakubwa, wapitishe sheria kwa sasa inayosema kuwa mwanasheria yoyote mtanzania akishiriki kwenye kuandaa mikabata 'inayohujumu' uchumi wa nchi basi atakuwa anatenda kosa. Hii inaweza kusaidia potential scandals huko mbeleni.
 
kwa kweli sijui mmiliki wa Dowans hasa baada ya kuambiwa kuwa Symbion imenunua assets zake. Ina Symbion alinunua nusu nusu?
 
Wakuu mimi napenda kutoka nje yamada kidogo,huko mwanza kuna sikuya 3 leo hakuna umeme jiji lote isipokuwa jeshini na hospitali tu nahata maji hakuna,hakuna taarifayoyote kutoka tanesco,inasemekana kwakua wanamwanza wamechagua upinzani watakiona chamoto,leo watu walitaka kuandamana ila hawakuandama haijulikani kwanini?tanesco mwanza kunani paaleeeh!
 
Mkuu Pasco: Napingana na wewe kwa nguvu zote kuhusu hapo nilipo-highlight na red. Serikali hii katu haina utawala wa sheria na mifano ambayo ipo ni mingi sana, nawe unafahamu fika. ....

Madevu, nadhani that was a bit of sarcasm by Pasco and nothing more...
 
"wasilipwe" "wasilipwe", kiko wapi? Tulisema humuhumu JF, kuzuia kuwalipa Dowansa ni kujitafutia matatizo mengine makubwa. Hawa si wapumbavu wanafanya biashara za kimataifa kwa muda mrefu.

Sasa Fedha tutawalipa, na hii Security ya US$ 5M tutailipa na Interest rate ya kuwachelewesha fedha yao ya malipo tutailipa. Hakuna mahakama duniani itakayopinga maamuzi ya ICC.

Semeni sasa, na hawa waingereza wamehongwa na Al Adawi.

Mnakazana kusifia ujinga siku zote. Haya sasa tunaona Madrasa na skuli zenu, ipi zaidi?
 
Una maana uamuzi wa kulipa dola milioni tano kama sercurity ya kuhairisha kesi? If so, then Tanesco wanaweza kukata rufaa kwenye mahakama za Uingerezeza. Lakini mahakama za UK haziwezi kutengua uamuzi uliotolewa na ICC Tribunal. Pia for update, there is no longer the House of Lords. Siku hizi inaitwa Supreme Court. House of Lords imebakia kuwa sehemu ya bunge tuu.

Kwanza walipe security halafu ndio wa appeal, hiyo ndio sheria.
 
I disagree with Pres. Kikwete's statement concerning the incompetency of ppl in contract law, the problem is he is not utilizing the competent ppl to do the job. ALL govt. contracts go through the AG's office and what goes on there who knows, but the proof is right before our eyes in these contracts the gvt. enters with so called shady investors that are today costing this country's people their and with that the country's own future.

Throughout the years, how many times do the same names keep repeating in these dubious contract deals: the AG's office, Mkono etc. The individuals who sign these dubious contracts are nothing short of traitors! How can a President or for that matter the AG of a sovereign country even think of obeying the law of an International arbitration court and fail to obey the rule of law of the country's own Highest court of the land, the Court of Appeals, concerning the Valambhia case. How can this President even allow the abuse of law, abuse of the courts, abuse of ppl's legal rights, and stealing of taxpayers money in the ongoing scam (a financial crime) of few TZ officials taking place today at the HC-the Valambhia case.

The former AG Chenge blatanly ignored and even passed laws in Parliament so that the Decree of the HC could not be paid. WHY? Why were so many cases marshalled against a man who won a decree from the High court of Tanzania and why was the AG sabotaging his entitlement? Keep in mind, when all these cases were going on against Mr. Valambhia the billing and invoicing continued to take place at the Bank of Tanzania. Also, money that was owed to Valambhia flowed out of the BoT to his other partner when the case was subjudiced. Millions and millions came out of the BoT. The retainer attorney for Bank of Tanzania advised the late gov. Balali not to pay the amount but instead continue to take Mr. Valambhia to court.

Why?

Because again Mkono was getting paid for his "job" in representing the BoT. And the amounts calculated for payment are astronomical: the decretal amount is used with interest and all additional other "fees" to reach the legal fee amount! Who benefitted from all these cases, certainly not Mr. Valambhia for he died in complete financial destitution, nor the people of Tanzania for the future generations will have to carry the burden of the astronomical costs of the still ongoing case. In 2003, AG Chenge again ignores the final and unappealable Judgement of the coa when the COA ordered the gvt. to pay Mr. Valambhia his entitlement & within a couple of months drags Mr. Valambhia back to court on an issue already decided by the court.

As per the late Mr. Maira, the so called new case was unconstitutional in inception. Looking beyond the fog of legalities, Chenge's action to "block" a court order resulted in continued money flow out of the BoT in legal commissions and fees.

To date, in their failure to not obey the court judgement from the Highest court of the land, the govt. has allowed the decretal amount to be exhausted in legal fees and commissions to prominent lawyers and let unsurmountable cost to be incurred to the TZ taxpayer. AND remains deaf, dumb, blind to the thievery of the money of the Tanzanian taxpayer.

The scam of denying Justice and stealing the lawful, legal right of Mr. Valambhia continues to take place in full force after his sudden demise on september 17, 2005.....The daylite robbery continues.....

Below is an excerpt from an article titled "The most expensive legal suit in Dar's history", by Richard Mgamba, dated June 28, 2009.
In the words of a senior Bank of Tanzania official concerning the Valambhia case:

"This is a project for some top officials because in practice there is no case, but its become the best way to earn commissions resulting from legal fees." "The way it is today, this might take another twenty years to be concluded, but the cost will be unbearable to the taxpayers. We have given legal opinion but no one cares because this is their cash generating machine."
 
CCM na serikali yake wasipoondoka madarakani nchi haitaendelea .. i swear

Serikali hata iwe ys Shetani huwezi kuwapa watu mkataba wameutimiza halafu uwaambie basi ondokeni, siwalipi!

Hata Nyerere aliwahi kufanya hivyo kwa Tiny Rowlands, alikiona cha mtema kuni. Alisema hatazami nyuma atageuka jiwe. Tiny akamwambia hujui sheria wewe. Baada ya muda, mbona Nyerere alirudisha mali zao zote na kuwalipa hasara zote juu. Aliufyata. Mcheze na Watanzania tu, msicheze na mijitu inayojuwa biashara za kimataifa. Kiranga komo! siku ingine itakuwa ni fundisho la kukurupuka kujidai kudhulumu eti kwa kuwa ni Mwaarabu. Huyo Mwaarabu sasa, anafanya mavitu yake, na kila tunapozidi kuipinga hukumu ya ICC ndivy mifedha yake inavyozidi kuongezeka, bureeeee "bilash" kisemeo cha waarabu.
 
Dowans wana haki kwenye hii issue,wether we like it or not.
Kuhusu LORNHO....Tiny anamjua Nyerere ni nani,get ur facts right...just start by googling,it helps.
 
Nadhani watu wanapigia kelele kitu kisicho. Sakata la Dowans limefika hapa kwa sababu nafasi zote tulizopewa na wengine tulizipigia kelele mapema kujitoa hazikuchukuliwa. Kama wengine wanavyosema nami naweza kuona kuwa ni vigumu sana kutowalipa hawa jamaa na tatizo liko katika a. Msingi wa kesi ya kwanza kabisa haikuwa katika hoja ambazo nilizidokeza wakati ule. Mkataba wa Dowans na Tanesco ungekataliwa mapema kwa saababu ulivyoingiwa haukuwa halali (kwamba Dowans ilirithi mkataba kutoka kwa Richmond bila maridhiano na Tanesco kama mkataba ulivyotaka kuhusu kurithishana) na vile vile juu ya hoja nzima ya Dowans kama kampuni.

Tulipoacha mkataba uingiwe na watu waingie na kuzalisha na sisi tukanunua umeme kutoka watu hao ni vigumu kuwakatalia tusiwalipe. Lakini haya yote ni kwa sababu waliopewa dhamana ya kuangalia maslahi ya nchi hawakufanya hivyo na hadi kesho hawajawa tayari kufanya hivyo. Wengine wanasema ati "tuna competent lawyers" well ni ngumu sana kumshawishi mtu hili.

Mikataba ya madini
Mikataba ya nishati
na sasa hivi mikataba ya ardhi yote ina dalili kuwa tuna matatizo katika kuandika mikataba yenye maslahi ya nchi. kama wanasheria wetu wanaosukumwa na wanasiasa kuingiza vipengele visivyo na maslahi kwa nchi kwanini hawaprotest? Of course hawakatai kwa sababu watakula vipi?

Nimeangalia mkataba mmoja wa mwaka jana tu wa ardhi ambapo mwekezaji ameambiwa atalipa sh 200 kwa ekari ya ardhi kwa mwaka kama rent! Tutaelezea vipi hili?
 
Back
Top Bottom