Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,408
- 31,392
Mkuu ni kweli alisema, na hoja yake ni kutafuta sababu tu. Miaka yote ya utumishi kati ngazi ya uwaziri hakuwahi kugundua hili? Mwanasheria mkuu ambaye ni mshauri wake hakuliona hilo na alimshauri nini. Kwanini asianze na kutafuta mwanasheria mkuu (AG) kutoka nje. Kesi ilipounguruma si walijua kuwa tuna wanasheria dhaifu (kama ni kweli) ilikuwaje wakamtuma yule wa Tanesco kwenye kesi kubwa kama ile ikiwa walijua kuna udhaifu.Mkuu I don't agree with what President Kikwete said, if he really said that. We have very competent lawyers in our country. The problem is we don't use them. Tuna maprofesa wazuri tuu on contractual issues. Tofauti na watu wanavyofikria, the issue does not lie with the agreement between Dowans and Tanesco. Issue iko kwenye sheria yetu ya arbitration. Inasema kuwa uamuzi wowote utakaotolewa na Tribunal utakuwa wa mwisho. Hii ina maana hautatenguliwa na mahakama yoyote ile.
Sasa wakati Tanesco wanaingia kwenye mkataba na Dowans, what they did was to copy and paste the clause from our arbitration Act to the effect that the arbitral award should be final and binding. Kama sheria yetu ingekuwa updated kwa kuondoa neno "final", then wasingeweza kukubaliana kuwa the award should be final.
On what is the way out for Tanesco and Tanzania as a country in this case, the answer is simple: there is no a way out. We have to pay Dowans the amount awarded by the Tribunal. The more we delay making the payment, the more it will cost us. Imagine kwa hii kesi tuu Tanesco imeamriwa kulipa dola milioni 5 kama security ili kuhairisha kesi mpaka Decemba 2011. Bado hujaweka gharama za kumwajiri mwanasheria ya Uingereza kuwakilisha Tanesco mahakamani. Where will Tanesco get this money wakati hawana hata umeme wa kuuza?
Mambo yote yanajadiliwa katika baraza la mawaziri, je hawakuona udhaifu huo.
Kwa kujua hatuna wataalamu kulikuwa na shida gani kutafuta kutoka nje? mbona wao wakiugua wanakwenda kutibiwa na wataalam nje ya nchi.
Kuhusu copy and paste, mkuu sio kama walifanya hivyo kwa bahati mbaya, walijua kabisa lakini 10% ilishatembea. Tunakumbuka Dr Mwakyembe alisema hata mwanafunzi wake angeshinda kesi,ipo namna si kuwa hawakujua walifanya nini.
Kama wataalamu wa sheria wana walakini, je wanasiasa wanaofanya maamuzi ni competent? Rais katika kamati kuu alisema lazima walipwe, alipokwenda kuonana na wabunge akasema hawalipwi! sasa hapa ametumia wanasheria kumshauri, na kama yeye anayumba kiasi hicho tutegmee nini inapofikia hapa.
Mkataba uliohamishwa kutoka Richmond kwenda Dowans, hivi kweli ni jambo linalohitaji mwanasheria kutambua makosa! Rais alishajua kuwa kampuni haikuwepo hapo alihitajika elimu gani kubwa kiasi hicho cha kutambua kuwa yapo matatizo.
Nani amewajibika kwa suala hili kisheria. Kama tatizo ni wanasheria mbona upuuzi huo umejirudia TRL ingawa ni kwa namna tofauti.
Nakubaliana nawe kuwa wapi ambapo katika mikataba yetu tumeona wataalamu waliobobea kama maprofesa wakishirikishwa?
Kinacholiumiza taifa ni rushwa ya hali ya juu kwa viongozi wa serikali, na hakukuwa na dhamira ya kulimaliza suala hili kwa manufaa ya taifa.
Huwezi kuliongelea jambo hili bila kuwahusisha mapacha, baraza la mawaziri ambalo kiongozi wake ni Rais.Kwa mchanganyiko huo nani atamfunga paka kengele! na kwanini tuwalaumu wanasheria kwa makosa ya siasa yaliyosabababishwa na uingiliaji.