JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Huu uzi simuoni mwenye id ya Faizafox....alikesha uzi mwengine unaofanana na huu akitetea serikali ya jk....

Hii kashifa sawa na Richmond ndo maana walishindwa kuvuana gamba....el akakanyaga moto chini akiutaka urais kama walivyokubaliana....sasa si jui bado anautaka au amebadilisha mawazo.

Cc faizafox MSALANI a.k.a choo na magamba wengineo!!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani mkuu wa Kaya alikuwa akiburuzwa buruzwa na washauri wake kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. Maana ilihitaji tafakari ndogo tu ili kujua kama malipo haya yanafilisi nchi.
Kama mkuu wa nchi kuruhusu tu haya malipo kufanyika kwa mtindo wa kufanya ujanja wa kukwepa kodi ilikuwa ni kosa kubwa kwa taasisi ya Ukuu wa Nchi.
Ova
 
Sikushangazwa kabisa kwa hilo.
Ukoo wa panya unawajumlisha wote.
Na hata sikushangaa kusikia amekimbilia Marekani kwa 'matibabu', na wapambe wake wepesi sana kutuwekea picha kila siku ili kutuonyesha na kutuhakikishia ya kwamba sio uzushi, Profesa wa kichina anaumwa!
Siku kadhaa kabla hajakimbia nchi nilikuwa nazungumza na jamaa yangu wakati suala la ESCROW linanong'onwa bado halijawa wazi, nikamwambia kitakaponuka JK hatakuwepo nchini...
Wezi wote ukoo mzima, hata yule usiyemdhania, mradi ameingia kwenye huo ukoo atakuwa mwizi.
Nani alifikiria Profesa Anna Tibaijuka naye ataingia kwenye mkumbo huo?
Hawasafishiki... Wachafu wote kuanzia Profesa wa kichina mpaka tarishi!
 
Last edited by a moderator:
Damn...usalama wa whatever siku hizi wanahusishwa na mambo yasiyo ya kiusalama!
Idara ya usalama wa Taifa, iliondoka na Mwalimu Nyerere alipofariki mwaka 1999, baada ya kuondoka Mwalimu,Idara hiyo yenye majukumu nyeti sana kwa nchi,ikabadilisha kinyemela majukumu yake na kuwa usalama wa watawala wa CCM!

Hivi katika mazingira ya kawaida pesa zote hizo bilioni 321, ambazo zilipaswa zirejeshwe TANESCO, wajanja wachache wakaamua kuzi-hijack,na kuanza kuzigawa kama njugu, bila intelejinsia ya policcm wala usalama wa Taifa kustukia, hivi katika mazingira hayo waTZ, tuna haja gani ya kuendelea kukiita kitengo hicho Idara ya usalama wa Taifa,badala ya jina wanalostahili la Usalama wa watawala wa CCM?

Hata mkiangalia 'movements' zote zinazofanywa kwa sasa na Idara hiyo kwa sasa ni kufanya juhudi zote za kufa na kupona, kuhakikisha ripoti hiyo ya CAG haitingi bungeni tarehe 26 ili ijadiliwe,kwa lengo moja tu la kuwaokoa na dhahma inayoelekea kuwakuta watawala wa CCM kutokana na skandali hiyo ya Escrow/IPTL!
 
Ngoja niweke bundle ya kutosha nataka niwe among the first to read the report!!! maeneo kama haya MSALANI na buku 7 fc hawakatizi kabisa maana vidole vinawatetemeka.
 
Uzoefu wangu JF kama kuna dataz huwa zinawekwa, ukiona hata Mkuu Invisible anatishia "nyau" ujue hamna kitu.

Huu nao ni upepo utapita tu! Hadi hili dude la ESCROW liishe mjadala wa katiba na UKAWA tutakuwa tumewasahau.
 
Last edited by a moderator:
Hawa washenzi ndio wanafanya maisha yanakuwa magumu wanapiga fedha za tanesco then tanesco wanatuumiza sisi walalahoi,wasaga unga nao wanapandisha bei,wauza mchele nao wanapandisha bei,wauza mafuta nao wanapandisha bei,gharama zote hizo za ongezeko anazilipa mlalahoi,ila wao wanaolala kwenye maghorofa wanapata usingizi mwanana na kaupepo kwa mbali ka-bahari....
 
Idara ya usalama wa Taifa, iliondoka na Mwalimu Nyerere alipofariki mwaka 1999, baada ya kuondoka Mwalimu,Idara hiyo yenye majukumu nyeti sana kwa nchi,ikabadilisha kinyemela majukumu yake na kuwa usalama wa watawala wa CCM!

Hivi katika mazingira ya kawaida pesa zote hizo bilioni 321, ambazo zilipaswa zirejeshwe TANESCO, wajanja wachache wakaamua kuzi-hijack,na kuanza kuzigawa kama njugu, bila intelejinsia ya policcm wala usalama wa Taifa kustukia, hivi katika mazingira hayo waTZ, tuna haja gani ya kuendelea kukiita kitengo hicho Idara ya usalama wa Taifa,badala ya jina wanalostahili la Usalama wa watawala wa CCM?

Hata mkiangalia 'movements' zote zinazofanywa kwa sasa na Idara hiyo kwa sasa ni kufanya juhudi zote za kufa na kupona, kuhakikisha ripoti hiyo ya CAG haitingi bungeni tarehe 26 ili ijadiliwe,kwa lengo moja tu la kuwaokoa na dhahma inayoelekea kuwakuta watawala wa CCM kutokana na skandali hiyo ya Escrow/IPTL!

Niko na mlevi mmoja hapa ananiambia idara hii ilikufa mwaka ambao Mwalimu aling'atuka Madarakani na Mzee Mwinyi kutobadilisha mfumo where by bwana Imran aliendelea kuwa mkuu wa kitengo chini ya Mwinyi na baadaye zikaingia Family interest kwa watoto wao kuoana(Kijana wa Mwinyi kumwoa binti wa Kombe) Kwa muktadha huo hakuna idara hiyo tena...unaweza kukojolea hata ukuta wa ikulu na kuondoka bila wanaoitwa state details ku reveal...Napata kilevi hapa!
 
Thread hii imfikie faiza foxy popote alipo!
aisome kimya kimya au louder itamwingia tu!
 
Last edited by a moderator:
The buck stops with JK. Stop scapegoating.

Haingii akilini kwamba alikua hajui huu ni wizi.

Kama alikua hajui huu ni wizi hastahili kuwa Rais. Incompetence.
 
hahahaha
Kwenye hili Taifa kwanza !

Naona watu wanaleta ushabiki kwakujifanya wanajua kumbe mapunguani tu...

Najiuliza Kama mambo mepesi Kama wanavyodhani joto kubwa Dodoma la nini?

Nawasubiri akina Lizaboni na Chabruma nione Kama wataendelea na nyimbo zao za ufisadi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom