Jumamosi iliyopita hapa JF palikuwepo na mjadala uliohusu Kikwete kuwauzia waMarekani sehemu ya kuweka kambi ya kijeshi kwa jeshi la waAmerica.
Tuliambiwa Rais wetu atafunga safari ya kwenda huko hivi karibuni kuonana na wahusika ili jambo hilo lijadiliwe na pengine likubalike.
Hii ni taarifa nzito sana isiyohitaji utani, na hata kama ni katika nyanja za upinzani wa kisiasa, jambo kama hili ni zito mno; na hasa linapohusishwa na ofisi kuu ya kitaifa kama hiyo ya Rais wa nchi.
Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.
Jumapili tunaambiwa Rais Kikwete anakwenda huko kwa shughuli za kibiashara (Sullivan.......), jambo ambalo lipo mbali kabisa na hiyo mipango iliyosemwa katika mjadala ule.
Maombi yangu ni kwamba tusiupeleke mbali sana huu upinzani wa kisiasa tukafikia hata mahali pa kuuana au kulisaliti taifa letu.
Ninazielewa mbinu chafu zinazotumika katika siasa, lakini kila mara tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa tunaweka usalama wa taifa letu katika janga.
5. Sio safari zote na mambo yote ya JK au rais yoyote duniani huwekwa wazi. Hili suala la kambi ya kijeshi ni kubwa na kwa vile JK ameamua kutosema ukweli. Hutasikia yeye au ofisa wa ikulu akikuambia safari ya Kikwete itahusu masuala la kambi.
6. Ni kweli kuwa at one point Kikwete na Kichaka walikubaliana kimsingi kabisa kuhusu hili jambo. Nina ushahidi wa ndani na reliable juu ya hili.
7. Si kweli kuwa mada kama hizi zinaanzishwa ili kuvunja amani na usalama wa taifa unless wewe una definition mpya ya usalama wa taifa.
Makelele tu kama kawa!!, hakuna la ajabu lilofanyika au litakalofanyika, fikiria Rais Mbowe angefanyaje ktk hilo dili alopewa Kikwete na mbwia ugolo Joji Kichaka!!!. Kwani mmesahau ile " either you are with us or with the terrorists." Kwanini usichukue kifuta machozi na kuendelea kubaki upande wao? Halafu Bongo ikikataa kuwekwa kwa hiyo kambi chepi kitacho ongezeka na chepi kupungua? kwani Bongo ndio itakuwa nchi ya kwanza kuwekwa kambi za kimarekani?. Mijikambi ya kimarekani ipo dunia nzima kuanzia ulaya mpaka mashariki ya mbali, tena nchi nyingine za MAANA kushinda hiyo Bongo( Ujerumani na Japan). Na hakuna lolote lilo haribika zaidi ya kambi hizo kuwa ni mojawapo ya vitega uchumi ya miji zilizomo.
Mie nina issues na US foreign policies, pia sijawahi kumpenda Kikwete kwa lolote(maelezo zaidi kapuni). Lakini hii ya kambi sidhani kama alikuwa na options ki vile kwani imekaa kidizaini ya "kusuka au kunyoa chagua moja." mwenzenu kachezewa "hardball."!!
Mwafrika wa Kike said:Vyanzo vyangu vya hapa USA vimethibitisha uvumi ambao kwa muda umekuwa unaendela Tanzania kuwa serikali ya marekani ina mpango wa kujenga kituo cha kijeshi cha kudumu (permanent base) nchini Tanzania.
Ingawa serikali ya Tanzania imekuwa inajaribu kuficha hizi habari kwa visingizio kuwa mambo ya kijeshi hayajadiliwi kwa vile yanahusu usalama wa taifa, nimeamua kuwaambia wanajeshi kuwa hili suala la kuwa na base ya wamarekani Tanzania ni kubwa na hivyo ni vyema wakaruhusu watanzania wakalijadili.
Siku za karibuni Kikwete amekuwa na vikao vya wazi na vya siri na wamarekani ambao wanatafuta nchi katika pwani na pembe ya afrika ili wajenge kambi ya kijeshi ya kudumu kama ile waliyo nayo kule KATARI (sijui namna ya kutamka hii nchi kwa kiswahili) kule mashariki ya kati.
Wazo la kuweka kambi Ethiopia limeonekana gumu kutokana na hali ya usalama, chaguo la pili la marekani lilikuwa Kenya ambayo hali ya ukabila inatishia usalama wa Kenya. Wamarekani wameamua kuchagua Tanzania ambao so far wanaona kama nchi yenye amani na utulivu.
Habari zinasema kuwa kimsingi Kikwete amekubali (nani angekataa pesa kibao wamarekani walizotoa) na Marekani imelipa pesa indirect kwa kuahidi kutoa mabilioni ya pesa za msaada. Yes, hizi pesa walizoahidi juzi za kuisaidia Tz zitaishia mfukoni mwa wachache na zitakazobaki zitasaidia kujenga base.
MY TAKE.
1. Mimi naunga mkono suala la wamarekani kuwa na base ya Tanzania maana ikiwepo au isiwepo sioni faida au hasara yoyote ukichukulia kuwa Kikwete na wenzake wanauza nchi kila siku.
2. Ni vizuri Kikwete aendeleze mchezo wa kula pande zote mbili za wa-Irani na wamarekani.
3. Kikwete awaambie ukweli wa-Tanzania wa kile kinachoendelea.
4. IMF na Benki ya dunia wakome kusifia Tanzania kuwa inaendelea wakati wakijua ni uongo ila wanatimiza moja ya masharti ya Tz kukubali ku-host base ya marekani.
5. Kikwete atimize ahadi yake kabla Raila hajashinda uchaguzi wa Kenya maana Raila naye amekubaliana na wamarekani katika hili.
Thanks!
Mkjj:
Nadhani hujasoma vizuri niliyoyaandika katika bandiko langu la mwanzo, hasa kuhusu utumiaji wa neno hilo 'uhaini.' Kama sikueleza vizuri jinsi nilivyolitumia na kusababisha uelewe ulivyoweka mawazo yako hapo, basi nadhani kuna lugha gongana.
Kalamu said:Jumamosi iliyopita hapa JF palikuwepo na mjadala uliohusu Kikwete kuwauzia waMarekani sehemu ya kuweka kambi ya kijeshi kwa jeshi la waAmerica.
Tuliambiwa Rais wetu atafunga safari ya kwenda huko hivi karibuni kuonana na wahusika ili jambo hilo lijadiliwe na pengine likubalike.
Hii ni taarifa nzito sana isiyohitaji utani, na hata kama ni katika nyanja za upinzani wa kisiasa, jambo kama hili ni zito mno; na hasa linapohusishwa na ofisi kuu ya kitaifa kama hiyo ya Rais wa nchi.
Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.
Jumapili tunaambiwa Rais Kikwete anakwenda huko kwa shughuli za kibiashara (Sullivan.......), jambo ambalo lipo mbali kabisa na hiyo mipango iliyosemwa katika mjadala ule.
Maombi yangu ni kwamba tusiupeleke mbali sana huu upinzani wa kisiasa tukafikia hata mahali pa kuuana au kulisaliti taifa letu.
Ninazielewa mbinu chafu zinazotumika katika siasa, lakini kila mara tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa tunaweka usalama wa taifa letu katika janga.
Makelele tu kama kawa!!, hakuna la ajabu lilofanyika au litakalofanyika, fikiria Rais Mbowe angefanyaje ktk hilo dili alopewa Kikwete na mbwia ugolo Joji Kichaka!!!. Kwani mmesahau ile " either you are with us or with the terrorists." Kwanini usichukue kifuta machozi na kuendelea kubaki upande wao? Halafu Bongo ikikataa kuwekwa kwa hiyo kambi chepi kitacho ongezeka na chepi kupungua? kwani Bongo ndio itakuwa nchi ya kwanza kuwekwa kambi za kimarekani?. Mijikambi ya kimarekani ipo dunia nzima kuanzia ulaya mpaka mashariki ya mbali, tena nchi nyingine za MAANA kushinda hiyo Bongo( Ujerumani na Japan). Na hakuna lolote lilo haribika zaidi ya kambi hizo kuwa ni mojawapo ya vitega uchumi ya miji zilizomo.
Mie nina issues na US foreign policies, pia sijawahi kumpenda Kikwete kwa lolote(maelezo zaidi kapuni). Lakini hii ya kambi sidhani kama alikuwa na options ki vile kwani imekaa kidizaini ya "kusuka au kunyoa chagua moja." mwenzenu kachezewa "hardball."!!
Samahani, YNIM naomba nikuulize yafuatayo kuhusu ubabe wa Marekani:
Je, ubabe wao wa kutulazimisha/kutupelekesha sisi kujiunga nao katika mambo watakayo:
--- umekuwa rahisi kuwezekana hivi sasa kuliko wakati wa Mwl. Nyerere au ulikuwa rahisi wakati wa Mwalimu?
---umekuwa rahisi kutendeka hivi sasa baada ya 9/11 au kabla yake?
---umekuwa rahisi kutendeka hivi sasa baada ya uvamizi wa Iraq au kabla?
Ni hayo tu, asante.
SteveD.
Mwk,
Hamna ambiguity hapo.....point yangu ilikuwa simple, kwamba raisi yeyote kwa mazingira yalokuwepo nisinge shangaa kukubali kwake kuwekwa kwa hiyo kambi hapo Bongo!!!. Sasa tatizo liwapi?wapi nimesema,kwamba wewe umesema mbowe? mie sina haja ya kulumbana na wewe kwani ile kwisha kuwa OLD, nilikuwa natoa two cents zangu tu!! au ndio ilibidi niwe nime-quit nini? mie nae na ujeuri wangu, sikomi tu kwikwikwikwikwi. Angalia your local NBC channel!!!! Have a goodnite.
Ndugu yangu,
Kichaka kwanza alisema anatengeneza "coalition of the willing," hilo halikuwezekana na ndipo akaja na hiyo nyingine ya arm twisting halafu wanakupoza na vimisaada.....hapo unakwenda na ule usemi wa "baniani mbaya lakini kiatu chake dawa." Nyerere ujeuri wake kama mie "mjukuu" wake kwikwikwi lilimshinda ndio maana akang'atuka, kwanini unafikiri miongoni mwa mengi muungano na Zanzibar ulikuwa muhimu wakti ule wa vita baridi!!???Unadhani Zanzibar lau kama ingekuwa kivyake ingeenda na sisi ku-side na losers kama Cuba na Russia? Thubutu!!!. 9/11 yes, lakini hilo rungu limeshafikwa na uzee. Sie ni victims wa uchumi wetu mbovu,sadly!!!.
YournameisMine:
....'rais yeyote?'.....
....'kwa mazingira yalokuwepo?'
Nakataa katakata, Mwalimu Nyerere asingekubali (akiwa rais).
Mazingira yapi tena yalokuwepo yanayotulazimisha kuwekewa 'kambi ya kudumu' ya kijeshi?
Asante kwa jibu, pamoja na kuwa kuna mengi ningeweza kuuliza hapo kwani jibu naona liko nusunusu (kama sijakosea). Basi, nitaruka na kukuuliza kingine, kama hutojali.
---kwa kuwa unautaja uchumi wetu kuwa mbovu na ndiyo huo kutupelekesha sisi ku-side nao; je, katika mwelekeo wa uchumi duniani kwa miaka 25 ijayo, nchi zipi zifuatazo wewe ungelipenda ku-side nazo iwapo ku-side na nchi mojawapo yeyote inaleta mkwaruzano na Marekani:
---China,
---Urusi,
---India,
---Brazil,
Ningeweza kuweka Iran, lakini naona niiache kwani ina utata wake.
Ahsante.
SteveD.
Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.
Mwk,
Hamna ambiguity hapo.....point yangu ilikuwa simple, kwamba raisi yeyote kwa mazingira yalokuwepo nisinge shangaa kukubali kwake kuwekwa kwa hiyo kambi hapo Bongo!!!. Sasa tatizo liwapi?.