JF Beware: Upinzani si Uadui

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,458
8,521
Jumamosi iliyopita hapa JF palikuwepo na mjadala uliohusu Kikwete kuwauzia waMarekani sehemu ya kuweka kambi ya kijeshi kwa jeshi la waAmerica.

Tuliambiwa Rais wetu atafunga safari ya kwenda huko hivi karibuni kuonana na wahusika ili jambo hilo lijadiliwe na pengine likubalike.

Hii ni taarifa nzito sana isiyohitaji utani, na hata kama ni katika nyanja za upinzani wa kisiasa, jambo kama hili ni zito mno; na hasa linapohusishwa na ofisi kuu ya kitaifa kama hiyo ya Rais wa nchi.

Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.

Jumapili tunaambiwa Rais Kikwete anakwenda huko kwa shughuli za kibiashara (Sullivan.......), jambo ambalo lipo mbali kabisa na hiyo mipango iliyosemwa katika mjadala ule.

Maombi yangu ni kwamba tusiupeleke mbali sana huu upinzani wa kisiasa tukafikia hata mahali pa kuuana au kulisaliti taifa letu.

Ninazielewa mbinu chafu zinazotumika katika siasa, lakini kila mara tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa tunaweka usalama wa taifa letu katika janga.
 
Nilikuwa nimeamua kuachana na hii mada baada ya kuona wadosi wa JF wameihamisha (na kama kawaida sikuanza kulia kama mtoto kuwa hii mada irudi kama super whiners hapa JF) lakini kwa sababu umeuliza swali kwa muanzisha mada basi nitakujibu kama ifuatavyo:

  • 1. Ni kweli kuwa Kikwete na Kichaka wameongea kuhusu mpango wa kuweka kambi ya jeshi la marekani nchini Tanzania.

    2. Ni kweli kuwa Safari ambazo Kikwete amefanya marekani zimekuwa muda fulani au mwingi pia zinahusishwa na hiyo mipango ya kuiweka hiyo kambi.

    3. Moja ya namna marekani inavyolipa fadhila kwa nchi marafiki zake ni pamoja na kutoa misaada ya nguvu - Misri na Pakistani. Au kulinda utawala ulio madarakani - Saudi Arabia, - Kutoa msaada mkubwa na ulinzi wa kijeshi - Israel, - Kununua kwa rushwa na vitu vingine rais wa nchi husika - Mobutu wa Zaire.

    4. Marekani imetangaza msaada mkubwa kabisa kwa Tanzania mwaka huu. Wakati nikishugulikia mipango ya kuwaalika Zitto na Slaa hapa US kukutana na members wa Congress, Nilielezwa wazi kuwa pesa hizo za msaada zina connection kubwa na uwekwaji wa kambi hiyo.

    5. Sio safari zote na mambo yote ya JK au rais yoyote duniani huwekwa wazi. Hili suala la kambi ya kijeshi ni kubwa na kwa vile JK ameamua kutosema ukweli. Hutasikia yeye au ofisa wa ikulu akikuambia safari ya Kikwete itahusu masuala la kambi.

    6. Ni kweli kuwa at one point Kikwete na Kichaka walikubaliana kimsingi kabisa kuhusu hili jambo. Nina ushahidi wa ndani na reliable juu ya hili.

    7. Si kweli kuwa mada kama hizi zinaanzishwa ili kuvunja amani na usalama wa taifa unless wewe una definition mpya ya usalama wa taifa.

Hii habari ni ya kweli na iliwekwa hapa ili ijadiliwe na membaz wote wa Tanzania na pia kuwapa nafasi waandishi wa habari wa home kui-quote JF na kuiandika hii story ili wasibughudhiwe na wana-usalama wa nyumbani (providing cover).

Inawezekana kuna watu wana nia mbaya na nchi yetu hasa ukisoma wapondeaji wa JF na watetezi wa mafisadi hapa. Hii mada haikuwa na nia yoyote ya kuharibu amani na utulivu nyumbani zaidi ya mtoa mada kujiweka hatarini (kama kawaida yake) ili kuujulisha umma wa watanzania wa kile presidaa wao anachofanya kwa niaba yao
 
Mwafrika wa Kike :
Ninakushukuru kwa kurudi na kutoa mwanga zaidi kuhusu jambo hili. Nilipoitafuta ile mada hapa JF na kuikosa nilianza kujiuliza mambo mengi, na kufikia kusema niliyosema hapo juu.

Sasa kuna jambo jingine ambalo nadhani itafaa lianzishiwe kichwa cha habari nalo lijadiliwe kwa mapana na marefu yake. Nalo ni mamlaka makubwa haya aliyonayo Rais, kufikisha kuamua jambo zito kiasi hiki kwa nchi yetu bila ya kupingwa na mtu yeyote.

by the way, huo msaada wa dola sijui 600 au 700; ni kwa miaka mitatu au mitano hivi. Kwa hiyo sio msaada mkubwa huo.

Hata hivyo ninakubaliana na wewe kuhusu nia ya hawa wakubwa wa dunia na urafiki wa kipumbavu anaouingia nao Kikwete.
Wao wanaingia kwa manufaa ya nchi yao, sijui kweli kama Kikwete anaingia katika urafiki huo na nia gani. Atakuwa amebadili kabisa mwelekeo na uhuru wa taifa letu daima.
 
  • 5. Sio safari zote na mambo yote ya JK au rais yoyote duniani huwekwa wazi. Hili suala la kambi ya kijeshi ni kubwa na kwa vile JK ameamua kutosema ukweli. Hutasikia yeye au ofisa wa ikulu akikuambia safari ya Kikwete itahusu masuala la kambi.

    6. Ni kweli kuwa at one point Kikwete na Kichaka walikubaliana kimsingi kabisa kuhusu hili jambo. Nina ushahidi wa ndani na reliable juu ya hili.

    7. Si kweli kuwa mada kama hizi zinaanzishwa ili kuvunja amani na usalama wa taifa unless wewe una definition mpya ya usalama wa taifa.

MwK, what a good response, nimependa sana majibu yako, kwani yana ukweli mwingi tu... kuna thread hii: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=5345&highlight=frelimo, nilichangia, mambo yaliyoongelewa yalihusisha jeshi, ghafla mtu akaja na kupost kuwa haturuhusiwi kuongelea mambo fulani... Mwawado ilibidi afute baadhi ya posts, pia posts nyingine pia zilifutwa mara moja. Sasa sijui, inawezekana hili nalo linahusiana...sijui miye..

SteveD.
 
Kalamu, nafikiri umehukumu kwa haraka. Itakuwa ni jambo la kusikitisha kuwa Rais afunge safari toka Dar kuja hapa kwa ajili ya kutangaza ujio wa mkutano wa Sullivan kitu ambacho tayari kilikuwa kinajulikana na siyo kama kutangazwa nchi itakayohost kombe la dunia au olympiki. Mkutano wa Sullivan ulikuwa unajulikana kuwa utafanyika Tanzania kwa muda mrefu sasa.

Hata hivyo hatuna budi kujihoji kuwa je inampasa Rais kuja na kutangaza jambo hilo? Je isingiwezekana Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri mwingine mwenye dhamana ya mambo hayo? Hivyo utaona kuwa kuja kwa Rais kufanya jambo la dakika 10 ni matumizi mabaya kabisa ya mali na muda wa Watanzania.. unless...

Unless anakuja na ajenda ambayo inahitaji Rais kuishughulikia. Sasa suala la nchi nyingine kufungua kambi kwenye ardhi yetu na wananchi kutaka kujulishwa siyo uhaini. Madai ya uhaini (treason) ni kosa kubwa zaidi dhidi ya jamhuri yetu, na kudai kuwa mtu kutaka kuelezwa juu ya mpango huo ni uhaini ni kurahisisha hoja.

Endapo kuna taifa lolote duniani linataka kuingia ubia wa kiusalama au vinginevyo na nchi yetu wananchi wanayo haki ya kutaka kujulishwwa na lazima wajulishwe. Na kimsingi, Wawakilishi wa wananchi wanapaswa kujulishwa. Ni usiri huu wa kisingizio cha "usalama wa Taifa" ndio uliosababisha tukanunua rada na wabunge wetu kushindwa kuambiwa ukweli.

Sasa, kama wao wanataka kufanya sualahili liwe siri (kama mpango huo upo) basi sisi wengine tutawasaidia kuliweka hadharani kama tulivyofanya suala la rada. Na believe me, hutaki hawa mademokrati wapate kisingizio cha kumshambulia Bush. Kama ni mpango mzuri, una maslahi kwa nchi na haugongani na sheria zetu au sera zetu za usalama, si wawaambie wananchi tu halafu yaishe? Haitakuwa ajabu kuwa na kambi au kikosi cha kijeshi cha nchi nyingine kwenye ardhi yetu. Wale wanaokumbuka watakumbuka tuliwahi kuwa na vikosi vya Urusi hapo hapo Tanzania. Haikuwa siri.

Binafsi, naamini kuwa tusihukumu vikali hivyo bila kujua ukweli wote. La maana ni waandishi watakapopata nafasi ya kuuliza waulize swali jepesi tu "Je serikali ya Tanzania ina mpango wa kuruhusu Marekani kujenga kambi yao katika ardhi yake?" Kama wameweza kututangazia tunapeleka majeshi Lebanon, tunafundisha majeshi ya Somalia na tunapeleka vikosi huko Darfur; ninaamini wataweza kutuambia kama tumeuza sehemu ya ardhi yetu kwa Wamarekani wajenge kambi yao; halafu kwa vile hatufungamani na upande wowote, itakuwa vizuri tuombee na Warusi na wenyewe wajenge something...resembling a military installation..
 
Makelele tu kama kawa!!, hakuna la ajabu lilofanyika au litakalofanyika, fikiria Rais Mbowe angefanyaje ktk hilo dili alopewa Kikwete na mbwia ugolo Joji Kichaka!!!. Kwani mmesahau ile " either you are with us or with the terrorists." Kwanini usichukue kifuta machozi na kuendelea kubaki upande wao? Halafu Bongo ikikataa kuwekwa kwa hiyo kambi chepi kitacho ongezeka na chepi kupungua? kwani Bongo ndio itakuwa nchi ya kwanza kuwekwa kambi za kimarekani?. Mijikambi ya kimarekani ipo dunia nzima kuanzia ulaya mpaka mashariki ya mbali, tena nchi nyingine za MAANA kushinda hiyo Bongo( Ujerumani na Japan). Na hakuna lolote lilo haribika zaidi ya kambi hizo kuwa ni mojawapo ya vitega uchumi ya miji zilizomo.

Mie nina issues na US foreign policies, pia sijawahi kumpenda Kikwete kwa lolote(maelezo zaidi kapuni). Lakini hii ya kambi sidhani kama alikuwa na options ki vile kwani imekaa kidizaini ya "kusuka au kunyoa chagua moja." mwenzenu kachezewa "hardball."!!
 
Mkjj:
Nadhani hujasoma vizuri niliyoyaandika katika bandiko langu la mwanzo, hasa kuhusu utumiaji wa neno hilo 'uhaini.' Kama sikueleza vizuri jinsi nilivyolitumia na kusababisha uelewe ulivyoweka mawazo yako hapo, basi nadhani kuna lugha gongana.
 
YNIM

Makelele ya kumlinganisha Mbowe na Kikwete hayakuwepo kabisa wakati nikianzisha hii mada. Labda kama wewe unataka kuingiza hii issue kwenye upinzani kati ya JK na Mbowe.

Soma hiki nilichoandika kwenye thread iliyohamishwa - original:

Mwafrika wa Kike said:
Vyanzo vyangu vya hapa USA vimethibitisha uvumi ambao kwa muda umekuwa unaendela Tanzania kuwa serikali ya marekani ina mpango wa kujenga kituo cha kijeshi cha kudumu (permanent base) nchini Tanzania.

Ingawa serikali ya Tanzania imekuwa inajaribu kuficha hizi habari kwa visingizio kuwa mambo ya kijeshi hayajadiliwi kwa vile yanahusu usalama wa taifa, nimeamua kuwaambia wanajeshi kuwa hili suala la kuwa na base ya wamarekani Tanzania ni kubwa na hivyo ni vyema wakaruhusu watanzania wakalijadili.

Siku za karibuni Kikwete amekuwa na vikao vya wazi na vya siri na wamarekani ambao wanatafuta nchi katika pwani na pembe ya afrika ili wajenge kambi ya kijeshi ya kudumu kama ile waliyo nayo kule KATARI (sijui namna ya kutamka hii nchi kwa kiswahili) kule mashariki ya kati.

Wazo la kuweka kambi Ethiopia limeonekana gumu kutokana na hali ya usalama, chaguo la pili la marekani lilikuwa Kenya ambayo hali ya ukabila inatishia usalama wa Kenya. Wamarekani wameamua kuchagua Tanzania ambao so far wanaona kama nchi yenye amani na utulivu.

Habari zinasema kuwa kimsingi Kikwete amekubali (nani angekataa pesa kibao wamarekani walizotoa) na Marekani imelipa pesa indirect kwa kuahidi kutoa mabilioni ya pesa za msaada. Yes, hizi pesa walizoahidi juzi za kuisaidia Tz zitaishia mfukoni mwa wachache na zitakazobaki zitasaidia kujenga base.

MY TAKE.

1. Mimi naunga mkono suala la wamarekani kuwa na base ya Tanzania maana ikiwepo au isiwepo sioni faida au hasara yoyote ukichukulia kuwa Kikwete na wenzake wanauza nchi kila siku.

2. Ni vizuri Kikwete aendeleze mchezo wa kula pande zote mbili za wa-Irani na wamarekani.

3. Kikwete awaambie ukweli wa-Tanzania wa kile kinachoendelea.

4. IMF na Benki ya dunia wakome kusifia Tanzania kuwa inaendelea wakati wakijua ni uongo ila wanatimiza moja ya masharti ya Tz kukubali ku-host base ya marekani.

5. Kikwete atimize ahadi yake kabla Raila hajashinda uchaguzi wa Kenya maana Raila naye amekubaliana na wamarekani katika hili.

Thanks!

Nimetafuta sana jina la Mbowe hapo na sijaliona kabisaaaaaa
 
Mkjj:
Nadhani hujasoma vizuri niliyoyaandika katika bandiko langu la mwanzo, hasa kuhusu utumiaji wa neno hilo 'uhaini.' Kama sikueleza vizuri jinsi nilivyolitumia na kusababisha uelewe ulivyoweka mawazo yako hapo, basi nadhani kuna lugha gongana.

Kalamu najua hujaelekeza swali lako kwangu ila yafuatayo kwenye post yako ya mwanzo yanahusiana kabisa na huo uhaini (angalia msisitizo kwenye rangi nyekundu):

Kalamu said:
Jumamosi iliyopita hapa JF palikuwepo na mjadala uliohusu Kikwete kuwauzia waMarekani sehemu ya kuweka kambi ya kijeshi kwa jeshi la waAmerica.

Tuliambiwa Rais wetu atafunga safari ya kwenda huko hivi karibuni kuonana na wahusika ili jambo hilo lijadiliwe na pengine likubalike.

Hii ni taarifa nzito sana isiyohitaji utani, na hata kama ni katika nyanja za upinzani wa kisiasa, jambo kama hili ni zito mno; na hasa linapohusishwa na ofisi kuu ya kitaifa kama hiyo ya Rais wa nchi.

Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.

Jumapili tunaambiwa Rais Kikwete anakwenda huko kwa shughuli za kibiashara (Sullivan.......), jambo ambalo lipo mbali kabisa na hiyo mipango iliyosemwa katika mjadala ule.

Maombi yangu ni kwamba tusiupeleke mbali sana huu upinzani wa kisiasa tukafikia hata mahali pa kuuana au kulisaliti taifa letu.

Ninazielewa mbinu chafu zinazotumika katika siasa, lakini kila mara tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa tunaweka usalama wa taifa letu katika janga.
 
Makelele tu kama kawa!!, hakuna la ajabu lilofanyika au litakalofanyika, fikiria Rais Mbowe angefanyaje ktk hilo dili alopewa Kikwete na mbwia ugolo Joji Kichaka!!!. Kwani mmesahau ile " either you are with us or with the terrorists." Kwanini usichukue kifuta machozi na kuendelea kubaki upande wao? Halafu Bongo ikikataa kuwekwa kwa hiyo kambi chepi kitacho ongezeka na chepi kupungua? kwani Bongo ndio itakuwa nchi ya kwanza kuwekwa kambi za kimarekani?. Mijikambi ya kimarekani ipo dunia nzima kuanzia ulaya mpaka mashariki ya mbali, tena nchi nyingine za MAANA kushinda hiyo Bongo( Ujerumani na Japan). Na hakuna lolote lilo haribika zaidi ya kambi hizo kuwa ni mojawapo ya vitega uchumi ya miji zilizomo.

Mie nina issues na US foreign policies, pia sijawahi kumpenda Kikwete kwa lolote(maelezo zaidi kapuni). Lakini hii ya kambi sidhani kama alikuwa na options ki vile kwani imekaa kidizaini ya "kusuka au kunyoa chagua moja." mwenzenu kachezewa "hardball."!!

Samahani, YNIM naomba nikuulize yafuatayo kuhusu ubabe wa Marekani:

Je, ubabe wao wa kutulazimisha/kutupelekesha sisi kujiunga nao katika mambo watakayo:

--- umekuwa rahisi kuwezekana hivi sasa kuliko wakati wa Mwl. Nyerere au ulikuwa rahisi wakati wa Mwalimu?

---umekuwa rahisi kutendeka hivi sasa baada ya 9/11 au kabla yake?

---umekuwa rahisi kutendeka hivi sasa baada ya uvamizi wa Iraq au kabla?

Ni hayo tu, asante.

SteveD.
 
Mwk,
Hamna ambiguity hapo.....point yangu ilikuwa simple, kwamba raisi yeyote kwa mazingira yalokuwepo nisinge shangaa kukubali kwake kuwekwa kwa hiyo kambi hapo Bongo!!!. Sasa tatizo liwapi?wapi nimesema,kwamba wewe umesema mbowe? mie sina haja ya kulumbana na wewe kwani ile kwisha kuwa OLD, nilikuwa natoa two cents zangu tu!! au ndio ilibidi niwe nime-quit nini? mie nae na ujeuri wangu, sikomi tu kwikwikwikwikwi. Angalia your local NBC channel!!!! Have a goodnite.
 
Ndugu yangu,
Kichaka kwanza alisema anatengeneza "coalition of the willing," hilo halikuwezekana na ndipo akaja na hiyo nyingine ya arm twisting halafu wanakupoza na vimisaada.....hapo unakwenda na ule usemi wa "baniani mbaya lakini kiatu chake dawa." Nyerere ujeuri wake kama mie "mjukuu" wake kwikwikwi lilimshinda ndio maana akang'atuka, kwanini unafikiri miongoni mwa mengi muungano na Zanzibar ulikuwa muhimu wakti ule wa vita baridi!!???Unadhani Zanzibar lau kama ingekuwa kivyake ingeenda na sisi ku-side na losers kama Cuba na Russia? Thubutu!!!. 9/11 yes, lakini hilo rungu limeshafikwa na uzee. Sie ni victims wa uchumi wetu mbovu,sadly!!!.
 
YournameisMine:
....'rais yeyote?'.....
....'kwa mazingira yalokuwepo?'

Nakataa katakata, Mwalimu Nyerere asingekubali (akiwa rais).

Mazingira yapi tena yalokuwepo yanayotulazimisha kuwekewa 'kambi ya kudumu' ya kijeshi?
 
Asante kwa jibu, pamoja na kuwa kuna mengi ningeweza kuuliza hapo kwani jibu naona liko nusunusu (kama sijakosea). Basi, nitaruka na kukuuliza kingine, kama hutojali.

---kwa kuwa unautaja uchumi wetu kuwa mbovu na ndiyo huo kutupelekesha sisi ku-side nao; je, katika mwelekeo wa uchumi duniani kwa miaka 25 ijayo, nchi zipi zifuatazo wewe ungelipenda ku-side nazo iwapo ku-side na nchi mojawapo yeyote inaleta mkwaruzano na Marekani:

---China,
---Urusi,
---India,
---Brazil,

Ningeweza kuweka Iran, lakini naona niiache kwani ina utata wake.
Ahsante.

Kaka,
Issue yako hiyo imeshajibiwa automatically huko juu.........ukisoma vizuri utaona Nyerere kazungumziwa kiaina.
Narudia tena, kwa mazingira ya sasa RAIS yeyote waTZ kwa kauchumi kenye kwashikor lazima ataburuzwa na mabeberu fullstop. Kama hutaki basi unakaribishwa.............
 
Asante kwa jibu, pamoja na kuwa kuna mengi ningeweza kuuliza hapo kwani jibu naona liko nusunusu (kama sijakosea). Basi, nitaruka na kukuuliza kingine, kama hutojali.

---kwa kuwa unautaja uchumi wetu kuwa mbovu na ndiyo huo kutupelekesha sisi ku-side nao; je, katika mwelekeo wa uchumi duniani kwa miaka 25 ijayo, nchi zipi zifuatazo wewe ungelipenda ku-side nazo iwapo ku-side na nchi mojawapo yeyote inaleta mkwaruzano na Marekani:

---China,
---Urusi,
---India,
---Brazil,

Ningeweza kuweka Iran, lakini naona niiache kwani ina utata wake.
Ahsante.

SteveD.

Kaka,
Najua jibu langu lipo kimtindo, lakini mie si mwandishi na nina avoid sana maneno mengi ktk kuelezea jambo...nina assume tu kama utakuwa umepata ile general idea ya suala lililopo mezani.
Mie nina problem sana na eastern world, siwaamini hata kidogo. Assume kwamba China ndio undisputed super power!!!!! the same to India(kama Super power), naomba jibu lako. Kwahivo basi mie sita side na Hao jamaa. Russia tulishakuwa nao kidizaini wakti ule, lakini hakuna la maana tulilolipata, kwahiyo nao pia nawatosa. Mie nabaki na Originals......USA. Maelezo yangu ni chochote utakachofikiria wewe!!!! kama sijajibu swali....Sorry.
 
Habari iliyoandikwa humu kuhusu kupewa nafasi ya kujenga Base ya Wamarekani kwenye Ardhi ya Tanzania ni Nzito.Jambo hili limekuwa linazungumzwa mara kwa mara ndani ya Pentagon.Wamarekani wanatafuta Eneo Africa haswa kusini mwa Jangwa la Sahara ili kuthibiti Ugaidi uliopo Horn of Africa na Eneo zima la Sudan.

Toka mwezi July 2006 kuna wanajeshi 1800 waliowekwa Djibouti na 450 Waliopo Pwani ya Mombasa (Simba Camp) ili kuangalia Mienendo ya Sudan,Somalia na Ethiopia.Hivi karibuni baadhi ya Viongozi wa ngazi za Juu wa Jeshi la Marekani wamepita kwenye Nchi za EA ili kuwashawishi Viongozi wetu watoe Eneo la kujengwa Africom.Kwa maelezo ya Magazeti ya Nyumbani Viongozi wote wa SADCC walikataa wazo hilo la wamarekani.

Kuna ushindani Mkubwa wa kibiashara kati ya US na China,hali hiyo inawafanya US wajaribu kuingia kwa nguvu zote Africa ili kupata uhakika wa kufanya mambo yao na kuwavuta Waafrika upande wao,US wana wasiwasi wa issue za kiuchumi hata usalama (Ulinzi)hiyo inathibitishwa na Ziara za mara kwa mara ya Viongozi wa Marekani barani Afrika.Rais Bush alitembelea Nchi 5 Mwanzoni mwa July na sasa Waziri wa Fedha (Henry Paulson) yupo Afrika kwa ziara ya wiki tatu.

Masuala ya kijeshi ni siri kubwa za serikali,lakini kwenye Nchi huru na ya kidemokrasia kama Tanzania sio siri Tena kulijadili Jeshi letu na mikataba yake.Wanaweza kufanya siri kutia saini utoaji wa Eneo kwa sababu ya shughuli za kijeshi lakini itafika wakati kila kitu kitakuwa wazi.Tulifichwa Kutiwa saini mkataba wa kuruhusu ndege za kijeshi za US kuruka kwenye anga ya Tanzania kulikofanywa na Rais Bill Clinton March/1998 lakini baadaye kila kitu kilikuwa wazi.

Sasa hizi Fununu za Us kupewa Eneo ndani ya Tanzania zinaweza kuwa na ukweli kwani Mwezi July 2007 Rais Bush alipotembelea Uganda aliweka jiwe la Msingi sehemu ambayo kitajengwa kituo cha kutia mafuta Ndege za Jeshi la Marekani,sasa hawa waungwana wanakuja taratibu,walianza kuomba ruhusa ya kurusha ndege zao kwenye Anga yetu,na wakapewa Eneo la aircraft refueling kwa maana hiyo sasa watakuja na issue ya BASE.

Wamarekani wana kituo kikubwa cha kijeshi Africa kilichopo kwenye Meli huko katikati ya Bahari ya Hindi sehemu iitwayo Diego Garcia.

Mama MWK aksante kwa habari yako hii,Muungwana atakuja huko tarehe 12/12 tutaiona delegation atakayokuja nayo na ni wazi ukweli utajulikana,mambo hayo hayana siri!!!
 
Nakubaliana na MK kwa asilimia kubwa, nadhani kama kiongozi umeingizwa madarakani kwa nguvu ya wananchi, basi huna budi kuwajulisha wananchi ni nini unafanya au nini unategemea kufanya.

Swala la Nchi yoyote kuweka kambi ya kijeshi nchini Tanzania ni swala zito na linalotakiwa kufanyiwa uchambuzi yakinifu. Ifahamike ya kwamba hili swala limeshavuma sana, mimi binafsi sifahamu ni nini ukweli wake, inaweza kuwa kweli au speculation. Kwani juzi juzi tuu serikali ya marekani imejadili kuja na mfumo mmpya wa kusaidia Africa kwa kuongeza wanajeshi katika bara hilo, swala ambalo limepata ubishani mkubwa sana kutoka kwa wanajeshi wengi nchini humo.

Swala JK kuja U.S kwa ajili ya unneccessary award, kwangu mimi personal ni upuuzi. Lakini ifahamike ya kwamba JK amependa kuongoza nchi katika style ya uchekibob, kitu ambacho kinatucost sana Watanzania.

Again, it maight be a speculation kuhusu hiyo base, lakini nadhani tunahaki ya kuongea anything concern our country, kuanzia tuna Vifaru vingapi mpaka tuna warembo wangapi bungeni. Hiyo haimaanishi kwamba tunatishia national security, inaonyesha tuna ishi katika karne ya demokrasia.
 
Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.

Boss, you are blowing this issue out of proportion unnecessarily. Ama huelewi maana ya uhaini au bado upo katika dimbwi zito la mawazo mgando ya mkubwa haambiwi amejamba. Ni hivi tuna haki ya ku-question dhamira, fikra, mawazo, maneno na matendo ya Rais wetu katika kila jambo alifanyalo kwa niaba yetu. Hii ni pamoja na jeshi, maana lile jeshi sio la kwake ni la kwetu sote yeye akiwemo. Na kama alivyokujibu vizuri sana dadangu Mwafrika wa Kike nani amekwambia kila anachofanya Rais kinawekwa hadharani hasa kwenye magazeti ya bongo. Hayo magazeti yetu yanasubiri press release ya ikulu ndiyo yaandike, hiyo utasikia leo kweli. Ukitaka kujua ni kweli au la uwe unafuatilia magazines za kimataifa.

Hiyo tabia ya kufikiri mambo ya jeshi hayajadiliwi hadharani ndio inawapa mwanya baadhi ya mafirauni kutuibia pesa zetu kupitia huko. Kama unaipenda nchi na jeshi letu utapenda kufuatilia pia yanayofanyika huko. Marekani inaweka base zake karibu kila kona ya dunia hii hasa kwenye nchi za ndio mzee, sasa kujadili kwamba ina-contemplate the same for Tanzania, ndio tuambiwe ni uhaini, no way. Kwani wewe hukuona wananchi wa mataifa hayo anayokwenda kila Rais wetu walivyotofautiana kuhusu vita ya Iraq na wengine walipinga waziwazi jeshi lao kwenda huko, kwa hiyo ingekuwa hapa kwetu ungewaita wahaini? Tujadili hoja, tuache lugha za kutishana, tumeshatoka huko pengine unaishi kizazi kisicho chako kisiasa ndugu yangu. Those days are gone and we are determined to see that they never come back!

Na kuhusu kichwa cha habari, kwamba upinzani si uadui, hsiku umetukumbusha jambo ambalo tunalijua na tunalifanya!
 
Mwk,
Hamna ambiguity hapo.....point yangu ilikuwa simple, kwamba raisi yeyote kwa mazingira yalokuwepo nisinge shangaa kukubali kwake kuwekwa kwa hiyo kambi hapo Bongo!!!. Sasa tatizo liwapi?.

Na ndio tukaulize, je, kujadili hili ndio usaliti kama anavyosema aliyebandika mada hii?

Na pili sio kweli kwamba kila Rais hapa duniani anakubali ujinga wa Marekani. Wapo kibao waliokataa kuendeshwa na taifa hili na wanadunda. Labda google Hugo Chavez hapo ulipo ili uanze kujifunza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom