Jumamosi iliyopita hapa JF palikuwepo na mjadala uliohusu Kikwete kuwauzia waMarekani sehemu ya kuweka kambi ya kijeshi kwa jeshi la waAmerica.
Tuliambiwa Rais wetu atafunga safari ya kwenda huko hivi karibuni kuonana na wahusika ili jambo hilo lijadiliwe na pengine likubalike.
Hii ni taarifa nzito sana isiyohitaji utani, na hata kama ni katika nyanja za upinzani wa kisiasa, jambo kama hili ni zito mno; na hasa linapohusishwa na ofisi kuu ya kitaifa kama hiyo ya Rais wa nchi.
Mtu mzima ukiwa ni mwenye akili timamu ukiamua kukaa mbele ya kompyuta na kupanga uongo kama huo na kuusambaza kwenye kadamnasi ya watu, kwa sababu tu za kipinzani za kisiasa; (mtaniwia radhi nikisema kuwa) utakuwa una mawazo ya kihaini kwa nchi yako.
Jumapili tunaambiwa Rais Kikwete anakwenda huko kwa shughuli za kibiashara (Sullivan.......), jambo ambalo lipo mbali kabisa na hiyo mipango iliyosemwa katika mjadala ule.
Maombi yangu ni kwamba tusiupeleke mbali sana huu upinzani wa kisiasa tukafikia hata mahali pa kuuana au kulisaliti taifa letu.
Ninazielewa mbinu chafu zinazotumika katika siasa, lakini kila mara tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa tunaweka usalama wa taifa letu katika janga.