Jeshi nchini Gabon lapindua Serikali ya Ali Bongo

Jeshi nchini Gabon lapindua Serikali ya Ali Bongo

Shida huyu Mkuu wa majeshi wa huku ni purely CCM.. Hawezi hizo mbanga kama za GABON
 
mkuu huna ya kibantu ?
hii familia ya Bongo wameifanya Gabon ya mama yao !
Omary alitawala umri wa binaadamu, Ali naye ni uccm tu..
Sukumiza kule !
tunaamini naye mayeboyebo hatotuangusha japo wanasema ni kabila lake ila si kweli, ni wa kuja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila huyo Bongo alikuwa kiazi na si ubongo tena..

Haiwekani ukae madarakani kwa zaidi ya miongo 5 pasipp nchi kusonga mbele..

Safi sana wanajeshi na hii iwe fundisho kwa wale viongozi wapenda madaraka...
 
Shida huyu Mkuu wa majeshi wa huku ni purely CCM.. Hawezi hizo mbanga kama za GABON

Vitu kama hivyo si lazima vifanywe na wanajeshi wa ngazi ya juu, wanajeshi wa ngazi ya kati ndo huwa wanalianzisha
 
Watu kwenye utawala wanazidiana
Mu7 lzma atamuachia mtoto ama ndg yke
Mu7 anajua kucheza na waganda syo kama Hao wakina bongo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo Baba yake HayatiOMARI BONGO alisilimishwa na GADAFI wakati Nchi yake asilimia 90 ni Wakristu na yeye ALLY BONGO alitawala kwa Ubavu sasa hiyo Stroke imembadilisha tabia.
 
Lakini Mapinduzi sio dili siku hizi,wawaachie wananchi wapige kura kwa kigezo kwamba raisi ni mgonjwa.
 
Lakini Mapinduzi sio dili siku hizi,wawaachie wananchi wapige kura kwa kigezo kwamba raisi ni mgonjwa.

Afrika kura siyo za maana tena, hapa kwetu tunapiga kura watu wana matokeo mfukoni, the only way to remove them from power ni hii ya kutumia nguvu. Siku si nyingi yatatokea ya kutokea hapa kwetu. uzuri washaanza kuwaonjesha madaraka kama alivyosema Lema.
 
"Amri ya kutotoka nje imetangazwa" inapotangazwa tahadhari kama hii na huna stock ya chakula wala nishati unafanyaje ili maisha yaende?

Ni usiku tu mkubwa....

Mchana shughuli zote zinaendelea kama kawaida

Sokoni kama kawaida....

kwenda dukani kama kawaida.....

Na kuuza na kununua kama kawaida...

Huko Gabon, nadhani kwa sasa ni saa 3asb, kama uko huko amka nenda sokoni kanunue mahitaji yako!!
 
Jeshi hilo limeshikilia Kituo cha Redio ya Taifa na kutangaza kushikilia madaraka huku wakieleza kuwa lengo lao ni kurudisha demokrasia nchini humo. Luteni Kelly Ondo Obiang ndiye aliyetangaza mapinduzi hayo na kuongeza kwamba Rais Ali Bongo wa nchi hiyo ameshindwa kufanya majukumu yake ipasavyo ya kuimarisha demokrasia. Rais Bongo anapinduliwa madarakani huku akiwa nchini Morocco, akipatiwa matibabu kwa maradhi ya kiharusi kwa miezi miwili sasa. Rais huyo ambaye aliingia madarakani Oktoba, 2009, akimpokea baba yake, Omar Bongo aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 42. Wanajeshi na vifaru vya jeshi vimeonekana kutawala mitaa ya nji mkuu wa nchi hiyo Libreville.
Wameona ni heri sasa ufalme ufikie mwisho. Kweli Demokrasia ya kweli ni muhimu kwa nchi za dunia hii.
 
Hao wanajeshi wapuuzi tu. Yaani wamesubiri mpaka amekuwa mgonjwa, tena yupo nje ya nchi, tena miezi miwili toka ameugua na kuwa nje ya nchi.

Hamna kitu hapo yatayofuata yatakuwa hayana tofauti na huyo mgonjwa ama yatakuwa mabaya zaidi kuliko ya mgonjwa.

Mawazo yangu tu.

Hiyo nchi imeandaliwa machafuko na wasiojulikana nadhani.
 
Jeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa.

Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

Wanakosoa pia viongozi wakuu wa jeshi nchini humo.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisikia uzalendo ndio huu sasa .
 
Back
Top Bottom