Nimepita na bodaboda naona njia nzima za mjini kuna wanajeshi wenye silaha na magari mengi sana, naambiwa njia ya Namtumbo wameweka road blocks za kutosha, Ruhuwiko kule kuna bodaboda wamesimamishwa, mbele ya hospital ya mkoa (Homso) zimepaki defender za kutosha zenye bendera nyekundu, kila anayehisiwa vibaya anasimamishwa hasa wa magari anasimamishwa na kuhojiwa/kupekuliwa...nasogea karibu na bank ya NMB naona wameanza kupiga mabomu ya machozi sijajua chanzo, nimeamua kusogea Mambo Leo kidogo kula, nitarudi mjini baadaye kupata taarifa kamili.