Hahaha Nyani Ngabu, unafahamu assassins ni waajiriwa wa mtu, au kikundi. Na wanaweza kuwa wafungwa wakaaletwa uraiani kuua kisha kuridi gerezani, wanaweza kuajiriwa kutoka nje ya nchi au wakawa ni wa humu humu tunaishi nao lakini unnoticed au hiding in plain sight.
Polisi hawataki kuumbuliwa wana cheza na akili zetu, wanajua tutasahau tu. Nchi hii wamewahi kupeleleza nini?! Wanatufahamu tunachemka halafu baada ya muda tunapoa. Hivyo wako kwenye kusubiri tupoe kisha tusahau, hakuna upelelezi wowote utaletwa.
Stephen Ulimboka tuliisha sahau likapita, Aliyemtolea Nape bastola tuliisha sahau likapita.
Roma Mkatoliki, tuliisha sahau likapita, na mwanafunzi wa NIT wametoa ubani wameshiriki mazishi, tumesahau limepita.
Hili la Tundu Lisu tutasahau litapita. They hope.
Polisi wanatamani tusahau lakini hamsahau. Walishasema upelelezi hauna mwisho, lakini ukweli hawapelelezi chochote.