Jeshi la Polisi mmefeli sana

Jeshi la Polisi mmefeli sana

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Taarifa zilizotolewa kuhusu madai ya “mwanajeshi wa Marekani” kukamatwa Tarime zimeibua maswali mazito kuliko majibu. Kutaja jina lisilo la kawaida kama Onkuri Ongeta.

Pamoja na picha zinazomuonyesha mtu huyo akiwa amejipamba kwa pete kama Mganga wa Kienyeji na mavazi yasiyoendana na mafunzo ya kijeshi, koti kuubwa kama Mc Mboneke, haya yanatosha kulifanya jambo hili lionekane kama maigizo yaliyopitiliza.

1763902080679.jpg

Zaidi, kutumia mabomu ya machozi ya aina CS M68, ambayo hutumiwa na polisi, si jeshi la Marekani, kunadhoofisha kabisa hoja iliyotolewa.

Tanzania ya leo ina wananchi wanaodai ukweli. Vyombo vya dola vinapaswa kuheshimu umma na kutoa taarifa sahihi bila utani wala propaganda.
 
Hata kutengeneza uongo unaofanana na ukweli wameshindwa.
 
😆 😂 😂 😂 Eheheheheeeeee...
 
Taarifa zilizotolewa kuhusu madai ya “mwanajeshi wa Marekani” kukamatwa Tarime zimeibua maswali mazito kuliko majibu. Kutaja jina lisilo la kawaida kama Onkuri Ongeta.

Pamoja na picha zinazomuonyesha mtu huyo akiwa amejipamba kwa pete kama Mganga wa Kienyeji na mavazi yasiyoendana na mafunzo ya kijeshi, koti kuubwa kama Mc Mboneke, haya yanatosha kulifanya jambo hili lionekane kama maigizo yaliyopitiliza.
View attachment 3506344
Zaidi, kutumia mabomu ya machozi ya aina CS M68, ambayo hutumiwa na polisi, si jeshi la Marekani, kunadhoofisha kabisa hoja iliyotolewa. Tanzania ya leo ina wananchi wanaodai ukweli. Vyombo vya dola vinapaswa kuheshimu umma na kutoa taarifa sahihi bila utani wala propaganda.

Majamaa ya nywinywi hayana mikakati,
 
Hilo koti lenyewe mbona kama limeshonwa na fundi maiko wa pale keko?!
 
Hamna mwanajesh hapo...mpiga ramli tu kama walivyo wengine
 
Hili filamu sijui liliishaje!

Au bado litaendelea!
 
1. Huyo kwenye picha ndio soldier wa US Army au uyo ni kamanda wa polisi?
Wanasema ndio US soldier eti, ila hawa watawala wetu 🤣🤣
Inanikumbusha zile picha za gari na jamaa aliyemteka MO 🤣🙌
 
Back
Top Bottom