Jeshi la Polisi mmefeli sana

Jeshi la Polisi mmefeli sana

Niliposikia tu hiyo habari nilijua ni uongo uliopitiliza mwanajeshi hata wa boko haramu hauwezi kumkamata akiwa na mabomu yake hawa watu sijui wanafanya hivi ili iweje aisee..
 
Taarifa zilizotolewa kuhusu madai ya “mwanajeshi wa Marekani” kukamatwa Tarime zimeibua maswali mazito kuliko majibu. Kutaja jina lisilo la kawaida kama Onkuri Ongeta.

Pamoja na picha zinazomuonyesha mtu huyo akiwa amejipamba kwa pete kama Mganga wa Kienyeji na mavazi yasiyoendana na mafunzo ya kijeshi, koti kuubwa kama Mc Mboneke, haya yanatosha kulifanya jambo hili lionekane kama maigizo yaliyopitiliza.

View attachment 3506344

Zaidi, kutumia mabomu ya machozi ya aina CS M68, ambayo hutumiwa na polisi, si jeshi la Marekani, kunadhoofisha kabisa hoja iliyotolewa.

Tanzania ya leo ina wananchi wanaodai ukweli. Vyombo vya dola vinapaswa kuheshimu umma na kutoa taarifa sahihi bila utani wala propaganda.
Eti mwanajeshi wa marekani ana kitambi utadhani askari magereza wa Tanzania...AIBU
Eti mabomu yana rangi za chadema....AIBU
Mwanajeshi anandevu utadhani mpishi pale polisi ofisas mess. AIBU

NIMEAMINI POLISI NI FOMFOO FAILURES.
HIVI WALITAKA KUMU IMPRESS BOYA GANI MWENZAO
 
Back
Top Bottom