Watu watatu washikiliwa kwa tuhuma za kuwa ni "Kamchape"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. ERICK S/O SINKALA [33] Mkazi wa Ilembo - Sumbawanga 2. SAID ERNEST MIHAYO [41] ña 3. AMOS BENARD NYANZANDU [25] wote wakazi wa Mbagala D’Salaam kwa tuhuma za kupiga ramli chonganishi @ lambalamba kwa lengo la kujipatia pesa isivyo halali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Watuhumiwa wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kufanya kafara za kuwaua ndugu zao ili kuwa matajiri na kumiliki mali.

Amesema Watuhumiwa wamekutwa wakiwa na vitu mbalimbali ikiwemo simu 09 za mkononi aina tofauti za kufanyia uhalifu, mabunda 15 ya karatasi zilizotengenezwa mfano wa noti, chekeche moja ya kufanyia shughuli za uganga, dawa za kienyeji aina mbili zilizofungwa kwenye gazeti na kwenye chupa ndogo, kitambulisho 01, cheti cha uganga wa tiba asili pamoja na vipeperushi viwili vya uganga wa tiba asili.

Pia soma:
 
Back
Top Bottom