Haki ndio kitu cha kwanza, ndio kila kitu, hasa haki za msingi. Amani ni moja ya kipengele kimoja ndani ya haki.
Binadamu yoyote akizaliwa tu popote duniani ana haki za msingi kama haki ya kuishi, kuabudu, kuongea, kulindwa mali zake, utu wake, akikamatwa kufikishwa mahakamani mara moja.
Binadamu wameweka mfumo unaitwa serikali wa kuchagua watu wachache kupitia uchaguzi huru, ulio wazi kati yao kuzilinda hizi haki zao pamoja na kodi zao, maliasili zao ziwanufaishe raia wote.
Sasa ukiwa na serikali iliyojaa ufisadi, hailindi watu, utu wao, maisha yao, mali zao,maliasili zao,kodi zao hakuna haki hapo.
Serikali inayoiba chaguzi na kuweka ndugu zao (nepotism), na washikaji wahuni, mafisadi, (Kleptocracy) haifanyi chaguzi halali ina maana hakuna haki kwenye hiyo nchi japo unaweza kusema kuna utulivu, amani (negative peace)sababu bado hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Ukraine na Urusi wakisitisha kupigana kwa muda unaweza kusema kuna utulivu(amani) ila kimsingi hakuna amani wala haki. Sawa na Israel na Palestine wamesitisha kupigana lakini unaweza kusema kuna utulivu (amani) ili hakuna haki hadi pale mambo yote ya msingi yaliyosababisha vita kutatuliwa kama ardhi, fidia, kukiri makosa, kuondoa chanzo cha ugomvi n.k.
Tanzania kwa sasa hatupigani wenyewe kwa wenyewe, kwa hiyo unaweza kusema kuna utulivu(amani) ila hakuna haki.
Haki zote za msingi hazipatikani Tanzania kama chaguzi huru, mahakama huru, kulinda utu, maisha ya watu, maliasili za taifa, kutumia kodi vizuri, teuzi zinafuata vigezo.
Mtu anaweza kutekwa, kuteswa, kupotezwa, kodi zinachezewa na familia chache, maliasili za taifa zinauzwa kama njugu lakini wananchi wametulia hiyo ni amani ya uongo (fake, negative peace)
Ukiwa na serikali inayotenda haki kwa wote automatically unakuwa na amani ya kweli (positive peace).
Serikali ya Samia inasisitiza tuendelee na amani ya kuigiza, waendelee kufanya uhuni wowote wanaotaka bila kuulizwa chochote na yoyote.