Jeshi la Polisi: Abdul Nondo alijiteka na kujisafirisha mwenyewe mpaka Iringa. Ladai alifuata mapenzi

Yeye kasema hajui kafikaje Iringa, hilo la kutekwa unalipata wapi?

jf kila mtu mchambuzi wa mambo...

sasa nyie pigine kelele fungueni thread hata buku ila ukweli ni kwamba dogo kaingia cha kike na lazima ashugulikiwe
 
Tangu rais wa awamu ya tano aingie madarakani kumekuwepo na mbinu chafu za upinzani kutaka kuichafua serikali kwa makusudi ya wazi wazi,ili nchi isitawalike

Mfano:
Swala elimu bure wamekuwa wakibeza tangu mwanzo na wakati hili limekuwa msaada mkubwa wa mtanzania maskini,,

Swala la ununuzi wa ndege mpya,,wamekuwa wakipinga na kudai ni mbovu lakini zinapiga kazi hadi leo,zinaimarisha ATCL ambalo ni shirika la umma na ni chanzo cha ajira,kuimarisha utalii na kuongeza mapato ya serikali

Usalama wa nchi,kumekuwa na matukio mengi ambayo ni ya uvunjifu wa amani ,Mauaji ya kibiti alisikika mbunge wa CDM akisema kama wapinzani hawatasikilizwa bungeni mauaji yale yangesambaa nchi nzima,,swali alikuwa anawajua wale wauaji? Alikuwa na mawasiliano nao?
Leo kuna mwanafunzi kacheza filamu ya kujiteka,nani yuko nyuma yake? Je kuna matukio mangapi ya uhalifu yamewahi pangwa na kutekelezwa ili kuichafua serikali?

Kwa mtanzania mzalendo Kuna kila sababu ya kuupuuza upinzani,ni dhahiri hauna nia njema na nchi yetu,,,,
Lisu kupigwa risasi ni filamu, Ben Saa Nane kupotea ni filamu, Mawazo kuchinjwa ni filamu??
Lumumba wamekulipa ngapi??
 
Kinachonishangaza zaidi ni kuwa huyu dogo hajawahi kusema ametekwa... kosa lake ni watu kumzushia katekwa??? Polisi wangepaswa kukamata waliozusha sio kijana aliyekuwa anaenda "kumtembelea mpenzi wake"
hapo ndo uwa shangae hao polisi na uchunguzi wao wa kisayansi,
 
Kwani Toka lini Polisi wetu wameanza kuaminika? Hii ni movie tu bado inaendelea tu ioa MUNGU ANAWAONA...
Jibu la maigizo haya ni tume huru ya uchaguzi na katiba mpya!!
Hiyo itaondoa umungu mtu wakati ulichaguliwa na hao wananchi!!
 
MBONA MATOKEO YA UPELELEZI WA ASKARI ALIYEMUUA AKWILINA MPAKA LEO KIMYA WAKATI MUUWAJI MNAE NDANI YA JESHI LA POLISI,,,JESHI LA POLISI MSTUFANYE SISI MAPOYOYO,,,MIMI NATAKA ASKAR ALIYEMPIGA RISASI NAKUMUUA AKWILINA AFIKISWE KIZIMBANI NA AHUKUMIWE PIA
 
Jibu la maigizo haya ni tume huru ya uchaguzi na katiba mpya!!
Hiyo itaondoa umungu mtu wakati ulichaguliwa na hao wananchi!!

unapiga kelele akati hata kumpigia kura hukumpigia...

sisi tuliomchagua tunakula matunda ya nchi na tunaona mema yake..

nyie ambao hamkumchangua pigeni kimya muendelee kuisoma namba

shaabaaaash....!!
 
Innocent until guilty.........Mahakama ndio chombo chenye kuweza kupima hatia ya mtuhumiwa na sio polisi, polisi ana wajibu wa kuihakikishia mahakama ili iweze mtia hatiani mtuhumiwa. Tuache ushabiki wa mitandaoni na tujadili fact
 
Jeshi la polisi leo limeongelea uchunguzi wake kuhusu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliyedaiwa kutekwa, Abdul Nondo kwamba alitekwa na watu wasiojulikana, taarifa ambayo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kujamii.

Kamanda Mambosasa amesema walifungua shauri la kuchunguza na kubaini ukweli, anasema walipata taarifa kutoka jeshi la Polisi Iringa kwamba mwanafunzi huyo alipatikana Mafinga akiwa salama na kuendelea na shughuli zake na hakuripoti popote kabla ya kukamatwa.

Jeshi la polisi kanda maalumu limesema mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka au kuamua kutoa taarifa hizo ambazo zilikuwa na maslahi kwake binafsi, labda umaarufu wa kisiasa kulingana na kujishulisha na mtandao wa kisiasa kwa mujibu wa kamanda Mambosasa.

Mambosasa amesema upelelezi umebaini mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambae alikuwa akifanya nae mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa, baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi wameona muda baada ya kusema ametekwa, simu yake iliendelea kufanya mawasiliano na binti aliemfata.



Huyu jamaa katunga story amna chochote hapa data za mtandao wa simu zinatosha kuonesha huyu jamaa kama anadanganya. Kila unapoama eneo simu nayo inabadilisha mnara kutokana na mnara uliokaribu kwa hiyo minara ya simu hupokezana kutoka unavyosogea eneo moja kwenda lingine. Sasa kama kuna data hizo na za watu aliongea nao na polisi imeweza kuzipata unahitaji nini zaidi kuprove hii kitu.
 
Wanajua wakimpeleka dogo mahakamani kesi inaisha kwa dk 2 tu..
Maana hakuna sehemu ambapo Nondo amesema ametekwa wala hakuandika kuwa ametekwa bali alisema "im at high risk"
Hata wale rafiki zake walio itisha press walisema mwenzao haonekani alipo hawakusema ametekwa..
Na kwenda iringa kwa uficho sio kosa kisheria..
Sina uhakika kama kesi hii itawasilishwa kwa namna hiyo japo wanasheria wa serikali wakati mwingine wanajitoa ufahamu. Kilichotokea hapa ni mtizamo wa taharuki uliojitokeza katika mitandao ya kijamii. Hisia ya hofu kutokana na uwasilishwaji wa tukio lenyewe na kulinganisha na matukio ya huko nyuma ya watu kupotea.
Hata hivyo, kwa nafasi aliyonayo kijamii, ujumbe wake ya kwamba alikuwa hatarini unatosha kuwaweka watu kwenye eti eti! Labda tumuombe moderator wa JF arudishe ule uzi wa Nondo kupotea ili tuone kama kuna hoja ya kihatia kisheria!
 
Okay, si mlisema wakili wake hawezi kumuona kwa sababu si mtuhumiwa, sasa kwakuwa ni mtuhumiwa, mruhusuni aonane na wakili wake
 
hivi usalama wa taifa wako wapi...maana kati ya mambosasa na yule kamanda wa iringa inatakiwa mmoja astep down kwa kulidanganya taifa.....
 
Back
Top Bottom