Jeshi la Polisi: Abdul Nondo alijiteka na kujisafirisha mwenyewe mpaka Iringa. Ladai alifuata mapenzi

unapiga kelele akati hata kumpigia kura hukumpigia...

sisi tuliomchagua tunakula matunda ya nchi na tunaona mema yake..

nyie ambao hamkumchangua pigeni kimya muendelee kuisoma namba

shaabaaaash....!!
Avatar yako inatisha umemwaga risasi kama njugu.
Au ni wale wale watu wasiojulikana??
 
Hee kumbe polisi wa Tanzania wanachunguza kisanyansi siku hizi! Tutafika tu.
 
Hivi kumbe ukiwa mwongo ufahamu na kumbukumbu hupetea! nafikiri Mola aliweka hivyo kwa makusudi. Polisi kuweni makini kwani weledi wenu kikazi na kuaminiwa unaporomoshwa na hao ccm wanaowatumia. Jitafakarini na mjitambue.
 
Mnatumia nguvu kubwa kuaminisha umma kuwa kajiteka, hizi sinema zenu za hovyo sana.


Ni mtu asiye na akili timamu ndio atadanganyika na haya maigizo yenu.

Ila wenye akili walishajua kinachoendela toka siku ya kwanza.
..
embu kua na akili finyu km funza,''tunatumia'' io tuna mm na nani? ao wenye akili unaosema km waljuass iweje wanacheza same game na losing everytime.. thinking outside the box huiwezi kaa kando
 
..
embu kua na akili finyu km funza,''tunatumia'' io tuna mm na nani? ao wenye akili unaosema km waljuass iweje wanacheza same game na losing everytime.. thinking outside the box huiwezi kaa kando

Rudi kwanza darasa la pili kajifunze kuandika vizuri.
 
Hawa polisi wetu wanatuambia kwamba wanajua mtu aliyetekwa na kundi la watu wasiojulikana anakuwaje, na kwa Maana nyingine wanajua hilo kundi la wasiojulikana halikuhusika kwa utekaji wa huyu mwanafunzi na kukonkludi wanalijua hilo kundi la wasiojulikana.
 
Wapi alisema katekwa? Mtu akisema im in risk, tafsiri yake ni kutekwa tu? Mnataka akanushe namna gani wkati mmemshikilia? Kwa nini mnamsemea? Kama ninyi siyo yale mauaji, ni kitu gani kiliwafanya mmshikilie? Ninyi ndio mlimwita aende polisi? Alipokuja polisi alisema alitekwa? Kwa nini mnamnyima hata nafasi ya kuonana na wakili wake walalndugu yeyote? Kafanya jinai gani? Kwa nini msiwakamante wanafunzi wenzake waliosema katekwa?

Kutekwa kwa huyu kijana kunawezaje kufuta alama za uharamia unaofnaywa hadharani? Ben Sanane yuko wapi? wlaiompiga Lisu wako wapi? Aliyemtishia Pistol Nape yuko wapi? Waliomteka Ulimboka wako wapi? Waliomteka Roma wako wapi? Waliovamia Clouds studio ni akina nani? Azory yuko wapi?

Kwa nini taharuki ya huyu kijana iwe na thamani kwenu kuliko hizo taharuki hapo juu? Hizo mnazisemaje? Nao wamejiteka?

Ombeni sana huyo kijana atoke salama huko mnakomfanyia mnavyojua. Vinginevyo, mtajua ninyi hamna uwezo wa kuumba hata mdoli!
Ndio wape ukweli wamezidi sana kufanya uharamia hadharani na kutisha watu, kuteka watu, kuua, watanzania wote wanaona mabaya haya na Mungu anawaona ipo siku watalipwa mabaya yote wanayoyafanya.
 
bado wanivuruga akili hawa polic,apewe fursa kijana atoe ya moyoni mwake ili tupate ukweli wa jambo hili,
 
Jeshi la polisi leo limeongelea uchunguzi wake kuhusu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliyedaiwa kutekwa, Abdul Nondo kwamba alitekwa na watu wasiojulikana, taarifa ambayo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kujamii.

Kamanda Mambosasa amesema walifungua shauri la kuchunguza na kubaini ukweli, anasema walipata taarifa kutoka jeshi la Polisi Iringa kwamba mwanafunzi huyo alipatikana Mafinga akiwa salama na kuendelea na shughuli zake na hakuripoti popote kabla ya kukamatwa.

Jeshi la polisi kanda maalumu limesema mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka au kuamua kutoa taarifa hizo ambazo zilikuwa na maslahi kwake binafsi, labda umaarufu wa kisiasa kulingana na kujishulisha na mtandao wa kisiasa kwa mujibu wa kamanda Mambosasa.

Mambosasa amesema upelelezi umebaini mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambae alikuwa akifanya nae mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa, baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi wameona muda baada ya kusema ametekwa, simu yake iliendelea kufanya mawasiliano na binti aliemfata.


Kweli ukiwa kamanda akili inatoka unageuka mropokaji,duuuu!!upuuzi kama huuu ukitoka kinywani mwa mtu kama yuleeee inaumiza
 
mkuu hata mimi sijawai kusikia uchunguzi wa kisayansi ukoje na unahojiwaje,nipewe elimu hapo,
 
sina sana hakika na kauli zao za ripoti za uchunguzi ,hata kama ni kwa maslahi ya wakubwa lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
kidemocrasia movement aliyoianzisha huyu bwana mdogo ina mashiko na ndo umaana wa democrasia kukemea uovu na kuondoa madarakani wasiowajibika kwa maslah ya umma na hawa ndo wauwaji wakubwa wa taifa wanalitukanisha taifa kwa kutowajibika ipasavyo
 
Back
Top Bottom