yani ndugu kinachonisikitisha ndio hicho.
yani mijitu inakuwa na mihemuko hadi inashindwa kukumbuka kauli za dogo alipokuwa kituoni iringa...
Kwani MTU akisema hajui amefikaje iringa anakuwa amemaanisha nn?!
Je hakuna uwezekano matapeli wamehusika?! Mbona kuna yule Dada Wa kimara aliokotwa bunju? Na akaripoti hajui amefikaje huko.. Anashikiliwa?!
Hatuwezi kumuhukumu MTU kwa kitu kinachotokea akilini mwetu. Ametoweka..amejikuta iringa.. Amewataarifu polisi.. Sasa akili zetu na tafsiri yake isiwe ndio sababu ya kumhukumu.
Nani kati yetu sote ajuaye Hugo dogo alipatwa na nn?! Sijasikia popote.. Sana maelezo yanashtua akili.
1. Taarifa kituoni dar ilitolewa na wanafunzi wenzake.. Akithibisha baada ya ujumbe alikuwa hapatikani. Lakini maelezo ya polisi yanasema alikuwa anawasiliana na mpenzi wake kwa simu IPI.. Ambayo Wazazi, na marafiki wake wote hawana?! Ukweli hapa wanao TCRA huyo mtoto anayo namba nyingine??!
2. Alikuwa akimfata mpenzi wake.. Mpaka muda huu aliyemuokota jina limetajwa kuna ugumu gani kumtaja huyo mpenzi wake?! Na yupo wapi.. Mufundi , Kilolo, Njombe, Iringa au Songea?! Hii itasaidia kujua alikuwa anaendelea na safari kwenda kwa mpenzi wake au alifika akaamua kupitiliza kwenda mbele kujiteka?!
3. Alikwenda kwa usafiri gani?! IT? Basi, helkopta?! Haya ni maswali ambayo polisi wanajua maana wamemuhoji huyo dogo. Lazima ameaambia japo kwa ufupi ni kwann alihisi yupo katika hatari.. Chaajabu hizi taarifa hatuzisikii kwenye uwasilishaji Wa Polisi. Inaleta mashaka.
Polisi wamefanya kazi yao.. Na kwa Mara ya kwanza ninaona emotion ndio zinatawala uchunguzi... Kiongozi mkubwa wa kipolisi unapoanza character assassination.. Unamshambulia subject na maneno kama Muhuni, Muongo... Vila kuuacha umma au vyombo vingine vya kisheria viamue kwa kuzingatia facts ulizowasilisha, inatufanya tuiname chini.
Ni Aibu.