Jeshi la Polisi: Abdul Nondo alijiteka na kujisafirisha mwenyewe mpaka Iringa. Ladai alifuata mapenzi

Acha mihemko..umesahau kama alienda kureport kituo cha Polisi Iringa na kudai hajui kafika vp Iringa!!!

yani ndugu kinachonisikitisha ndio hicho.

yani mijitu inakuwa na mihemuko hadi inashindwa kukumbuka kauli za dogo alipokuwa kituoni iringa...
 
Hawa si ndio waliosema "Dr. Shika, alitumwa na Lugumi kuharibu mnada?"

Yes amejisafirisha. Kosa la kujisafirisha ni lipi hadi wamshikilie na wasimruhusu hata kukuta na ndugu wale mwanasheria wake?

Kwa kuenda iringa kwa kujisafirisha ni jinai?

Alitolewa na kada wa ccm akisema, alimkuta kazimia kule mufindi. Akampa na nauri aende kureport kituo cha polisi.

Alipojisafirisha alifika mfindi akajiondolea fahamu, kisha yule kada wa ccm akamkamata kwa nguvu na kumfikisha kutuo cha polisi?

Mnasema wazazi waombe msamaha hadharani. Waombe msamaha kwa nani kwa kosa gani?

Mungu ni Mungu na kamwe hatakuwa binadamu.

Something is not adding up…..fulustopu...
 
Dola inafanya kazi yake,dogo kashashitumiwa labda akubali kuunga juhudi za rais anaweza achiwa huru
 
Kwanini hapewi nafasi ya kuzungumza na badala yake tunawasikiliza polisi tu ambao hawaoneshi kufanya uchunguzi wowote bali kutaka kuthibitisha na kuhalalisha kitu au kuilazimisha jamii iamini jambo fulani tu?
Hapo hata mimi nashangaa. Ntu yupo kwanini asizungumze yeye mwenyewe badala yake ni polisi ndiye anayezungumza. Kuna mmoja naye eti ilibidi mpaka waziri wa habari eti naye akahudhuria press conference ya utoaji wa taarifa
 
*Uchunguzi wa Kisayansi* wamwaga hadharani siri za mwanafunzi aliyedaiwa kutekwa ni Abdu Nondo anadaiwa alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.
UCHUNGUZI WA KISAYANSI ama kwa hakika tumeendelea
Ina maana waliingia maabara kufanya experiment?
 
Kijana katekwa rasmi sasa, tena katekwa kihalali kabisa na jeshi la polisi
Mbona mpenzi wake wamemwacha? Si wangemteka na yeye? Halafu mbona wanaongea wao wakati mwenyewe yupo? Mbona matukio mengine kama ya Lissu na Saa 8 hawajawahi kuwa faster kiasi hiki?
 
Aisee, jamani siku zote siasa acha iwe na wanasiasa maana mambo kama haya sasa yameshatia dosari elimu yake huyu kijana aitwaje nondo, na once ukishakuwa nimtuhumiwa na mshtakiwa elimu yake imekwisha kuharibika..
Kitu ambacho upande wangu naona kina umuhimu kwasasa ni kwa kijana huyu kuomba serikali msamaha na pamoja na wananchi kutokana, Himself he can not fight against is own Government..
Ingawaje kuna kale kamsemo cha aluta kontinua ila kwangu naona for the sake of is Carrier in education ni bora afanye hivyo...​
 
yani ndugu kinachonisikitisha ndio hicho.

yani mijitu inakuwa na mihemuko hadi inashindwa kukumbuka kauli za dogo alipokuwa kituoni iringa...
Kwani MTU akisema hajui amefikaje iringa anakuwa amemaanisha nn?!

Je hakuna uwezekano matapeli wamehusika?! Mbona kuna yule Dada Wa kimara aliokotwa bunju? Na akaripoti hajui amefikaje huko.. Anashikiliwa?!

Hatuwezi kumuhukumu MTU kwa kitu kinachotokea akilini mwetu. Ametoweka..amejikuta iringa.. Amewataarifu polisi.. Sasa akili zetu na tafsiri yake isiwe ndio sababu ya kumhukumu.

Nani kati yetu sote ajuaye Hugo dogo alipatwa na nn?! Sijasikia popote.. Sana maelezo yanashtua akili.

1. Taarifa kituoni dar ilitolewa na wanafunzi wenzake.. Akithibisha baada ya ujumbe alikuwa hapatikani. Lakini maelezo ya polisi yanasema alikuwa anawasiliana na mpenzi wake kwa simu IPI.. Ambayo Wazazi, na marafiki wake wote hawana?! Ukweli hapa wanao TCRA huyo mtoto anayo namba nyingine??!

2. Alikuwa akimfata mpenzi wake.. Mpaka muda huu aliyemuokota jina limetajwa kuna ugumu gani kumtaja huyo mpenzi wake?! Na yupo wapi.. Mufundi , Kilolo, Njombe, Iringa au Songea?! Hii itasaidia kujua alikuwa anaendelea na safari kwenda kwa mpenzi wake au alifika akaamua kupitiliza kwenda mbele kujiteka?!

3. Alikwenda kwa usafiri gani?! IT? Basi, helkopta?! Haya ni maswali ambayo polisi wanajua maana wamemuhoji huyo dogo. Lazima ameaambia japo kwa ufupi ni kwann alihisi yupo katika hatari.. Chaajabu hizi taarifa hatuzisikii kwenye uwasilishaji Wa Polisi. Inaleta mashaka.

Polisi wamefanya kazi yao.. Na kwa Mara ya kwanza ninaona emotion ndio zinatawala uchunguzi... Kiongozi mkubwa wa kipolisi unapoanza character assassination.. Unamshambulia subject na maneno kama Muhuni, Muongo... Vila kuuacha umma au vyombo vingine vya kisheria viamue kwa kuzingatia facts ulizowasilisha, inatufanya tuiname chini.

Ni Aibu.
 
Nashangaa jeshi la polisi kumshikilia Abdul Nondo kwa kosa la kudanganya ametekwa, lakini tukirudi kwenye ukweli hakuna sehemu ambayo Abdul Nondo alisema ametekwa, waliosema ametekwa ni wananchi hasa kutokana na SMS yake aliyowatumia marafiki zake.
Text yake ilikuwa na maana gani
 
Sasa huyo body guard nyuma yake wa nini wakati yeye mwenyewe ni askari? Ina maana hawezi kujilinda? Tena huyo wa nyuma ana cheo kidogo kuliko yeye ina maana yeye amebobea sasa mlinzi wa nini? Eti hata mkuu wa majeshi naye utaona ana mlinzi. Wa nini sasa?
 
Nashangaa jeshi la polisi kumshikilia Abdul Nondo kwa kosa la kudanganya ametekwa, lakini tukirudi kwenye ukweli hakuna sehemu ambayo Abdul Nondo alisema ametekwa, waliosema ametekwa ni wananchi hasa kutokana na SMS yake aliyowatumia marafiki zake.
Twaomba ku-balance story ....

a) KAULI yako kuwa mtuhumiwa Abdul Nondo HAKUTAMKA POPOTE kwamba ALITEKWA bali ni kauli ya jeshi la polisi .....

b) KAULI ya mtuhumiwa Abdul Nondo aliporipoti pale kituo cha polisi Mafinga kwamba ALITEKWA ...

Now which is which?
 
rejea maelezo yake aliyotoa alipojipeleka kituo cha polisi iringa

alisema namejikuta kule mafinga pasipo kujua amefikaje...

je hapo hakuumaanisha kuwa alitekwa then watekaji wakamdrug..

huyo dogo kacheza mchezo bila kuwaza nje ya box... wacha apigike...

Yeye kasema hajui kafikaje Iringa, hilo la kutekwa unalipata wapi?
 
Abdul Nondo kajiteka
Roma alitekwa..
je serikali ilifanya juhudi gani kumsaka mtekaji wa Roma ?
Azory katekwa serikali imefanya juhudi gani ?
hata kukemea hakuna..
Inaonekana kutekwa ni jambo la kawaida kwa CCM ila kujiteka ni uhaini hata kama ulitekwa kweli..
Mwigulu alisema Soweto Ars CDM wamejipiga mabomu.
Watu walikufa na wauwaji hadi leo hawajakamatwa.
Huo ni muendelezo wa mauwaji CCM!!
 
Taarifa ya Polisi wa Iringa wanasema alijipeleka mwenyewe kituo cha Polisi. Taarifa za Polisi wa kanda maalum Dar zinasema kwamba alikuwa anaendelea na shunguli zake hadi alipokamatwa na Polisi. Basi sawa.
 
Nashangaa jeshi la polisi kumshikilia Abdul Nondo kwa kosa la kudanganya ametekwa, lakini tukirudi kwenye ukweli hakuna sehemu ambayo Abdul Nondo alisema ametekwa, waliosema ametekwa ni wananchi hasa kutokana na SMS yake aliyowatumia marafiki zake.

Kuna Watu huwa mnadhalilisha kweli IQ's zenu humu Jamvini halafu mkidharaulika mnalaumu. Hivi ni nani aliyeanza kuwataarifu Wenzake kuwa yupo at risk? Hivi baada ya Yeye kupotea ghafla muda mfupi hicho Kitendo kinaitwaje? Hivi wote waliotekwa na kupatikana walisema mwanzoni au baada ya kupatikana? Unaposema kuwa Nondo hakusema ametekwa maelezo yake mwenye alipoenda Polisi kule alikopatika unayakumbuka? Ni Yeye ndiye alisema kuwa alitekwa sasa inakuwaje uje humu tena utake kukwepesha maelezo yake mhusika mwenyewe? Hivi hao Marafiki zake unadhani bila hayo mazingira ya Kutekwa ambayo aliyaonyesha mwenyewe Wao wangeanza kusema vile? Kuna Watu ' mnaboa ' mno.

Haya kamtaarifu huyo Nondo wako kuwa ' siku zote makali ya Panga hayajaribiwi Shingoni '.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom