Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,317
- 11,181
Kulingana na radio ya Israel vikosi vya IDF vimefanya mashambulizi makubwa ndani ya Gaza usiku wa kuamkia leo. Hata hivyo taarifa zaidi za mashambulio hayo dhidi ya Hamas hayajwekwa wazi.
Habari hizo zinafuatia ahadi ya hapo jana ya waziri mkuu wa nchi hiyo aliposema mashambulio ya kuingia Gaza yapo karibu kuanza lakini akasita kutaja ni siku gani yangeanza. Na pia yanakuja wakati viongozi wa nchi za Ulaya wakikutana kujadili vita hivyo na umuhimu wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kwa Gaza.
Katika mkutano huo wa viongozi wa Ulaya,raisi Macron wa Ufaransa aliitahadharisha Israel kuwa kuingiza vikosi vya IDF itakuwa ni kosa kubwa itakalolifanya nchi ya Israel
Kwa takriban wiki mbili tangu patokee mashambulizi ya kushtukiza ya Hamas waziri mkuu wa Israel amekuwa katika malumbano na waziri wake wa ulinzi kuhusu uharaka wa kuingiza vikosi hivyo Gaza.
Wakati waziri wa ulinzi akihimiza kufanyika zoezi hilo kwa haraka kuokoa moyo wa kutaka kupiga wa askari wake walionao, waziri mkuu amekuwa akiakhirisha vita vya ardhini kwa kuhofia yatakayozuka hasa akiwafikiria Hizbullah.
Israeli army carries out a “relatively large” ground incursion into the Gaza Strip overnight to attack Hamas positions, according to the Israeli army radio.Aljazeera