Jerry Silaa ataka Serikali kutoyumbishwa uboreshaji wa Bandari

Rege

Senior Member
Jul 9, 2022
112
140
Mbunge wa Ukonga (CCM) Jerry Silaa ameishauri Serikali kutokubali kuyumbishwa na watu wanaotaka nchi isiendelee kiuchumi kwa kupinga utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali yaTanzania na Dubai juu ya uboreshaji wa bandari nchini.

Bunge liliridhia azimio makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya katika uendelezaji na uboreshaji wa utendaji wa bandari Tanzania la 2023.

Silaa ameyasema hayo leo Alhamis Juni 22, 2023 akichangia ripoti ya Hali ya Uchumi, Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/24.

Amesema makubaliano hayo yalipigiwa kelele na watu wengi na kwamba baada ya elimu juu ya suala hilo kutolewa wenye kuelewa wameelewa kuwa yalikuwa makubaliano tu.
Silaa amesema elimu iliyotolewa na Serikali imewawezesha Watanzania kuelewa juu ya makubaliano hayo.

Amesema wananchi wameelewa kuwa mikataba ya uwekezaji utakaofanyika bado haijaingiwa na pia wakati wa uingiaji wa mikataba hiyo Serikali imesema itazingatia maoni na ushauri uliotolewa na watu mbalimbali.
 
Kwani makubaliano yanasemaje? Yenye sahihi ya Samia na Mbarawa
 
Huyu Silaa inasemakena alikuwa na kampuni zake anazipa tenda alipokuwa meya wa Jiji... he is a sinner aache kuendeleza maudhi
 
Back
Top Bottom