Anaandika Jerry C. Muro
Taifa la Tanzania limeingia katika Historia ya Dunia Kufuatia Kampuni ya Barrick Gold kukubali kwa mara ya kwanza Kugawana asilimia hamsini kwa hamsini 50/50 ya Faida katika uzalishaji wa Dhahabu nje ya Asilimia 16 ya Mrahaba na Kodi ambayo taifa itapata.
Nimedadisi katika nchi mbalimbali ambazo Barrick wamefanya uwekezaji kama huu na kugundua Tanzania ndio nchi pekee ambayo imethubutu na kufanikiwa katika hili, Hongera Tanzania Hongera Rais Mzalendo Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli katika kurekebisha kwa vitendo makosa ya watangulizi wako, huu ndio Uongozi unaoacha alama tukufu, naamini kwa sasa watangulizi wako wanafuraha kubwa ya kuona umesahihisha kwa vitendo pale walipokosea.
Muafaka Baina ya Tanzania na Barrick umewaacha "bila nguo" tena nasisitiza "bila nguo kama mnyama" wale wote waliokuwa wakisubiri Tanzania ipelekwe mahakama ya kimataifa kutokana na kuchukua hatua za kuzuia makinikia, kwangu nasema shame on you najua wamenielewa na wamesikia, Leo Tanzania imepata Shilingi Bilioni 700 kama hela tu ya kujenga uaminifu, bado nasubiria tupate kodi yetu, tupate Mrabaha wetu, kisha tugawane faida hamsini kwa hamsini.
Nimefarijika sana na kauli ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka wawekezaji wengine wote katika Sekta ya Madini kujitafakari na kuanza kufuata uelekeo wa makubaliano kama Haya na Barrick, sasa tutaanza kuvuna neema kwenye Tanzanite, Almasi na kisha tutaingia kwenye Gesi na Mali asili zingine, Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili ya Uongozi wa Mhe Magufuli, naamini akimaliza miaka Mitano ya kwanza na ile mingine lazima Tanzania tutakuwa "Donor country"
Naomba nimalize kwa kufikisha salamu kule Nairobi, mwambieni kulikuwa na sababu ya Mungu kumuweka hai ili aje ashuhudie ukuu wa Mungu kupitia Mhe Magufuli, lile alilosema haliwezekani kwa sasa limewezekana na Hatimae Mhe Magufuli ameibuka shujaa na kinara wa kielelezo cha Rais Bora Africa anaepigania rasilimali za nchi yake, Mungu alisema Muombee sana "adui" yako aishi miaka mingi ili Ashuhudie Baraka za Mungu kwako, Hatimae maombi yetu yamejibu sasa.
Wasalamu
Jerry C. Muro
Dodoma, Tanzania
20/10/2017
Mwambieni huyu mpumbavu asome wenzake waliokwenda shule wanavyosema:
Muyabi Joseph:
Kuna mambo umeyaandika hapa ambayo hayapo kwenye sheria yoyote, nq hayapo sawa. Yawezekana kuna mahali hukuelewa au hukusikia vizuri:
1) Hakuna mrabaha (royalty) wa 16%, iwe kwa sheria ya zamani auiliyopitishwa hivi karibuni. Sheria iliyopitishwa hivi karibuni mrabaha ni 6%.
2) Kuhusu ofisi, nadhani alimaanisha operations offices.
3) dola million 300 zitalipwa in good faith ina maana hakuna kosalililothibituka kufanywa na Acacia. Siyo sahihi kusema ni malipo ya kuanzia.
3) Hilo la ujenzi wa barabara halipo. Lakini kama sehemu ya social responsibility, kampuni itaendelea kusaidia jamii zinazowazunguka
4) Hilo la kusema watahusika nadhahabu, copper na silver pekeeyaliyobakia yatakuwa mali ya Tanzania, tunataka kujiridhisha kwa ambacho hakipo. Nimefanya kazi katika migodi hiyo, zaidi ya hayo madini hakuna mengine ambayo yapo katika economic concentrations. Sharti hilo Barrick wamekubali kwa sababu halina athari yoyote kwao
5) Kuajiri na kuwafundisha watanzania, tangu makampuni haya yaanze, imekuwa ndiyo sera inanyoyaongoza. Hayo yamekuwepo wakati wote, ndiyo maana sasa hivi kuna watanzania kwenye senior managent positions. Mimi nilianza kwenye makampuni haya nikiwa junior geologist, nikapanda mpaka kuwa country manager.Nikaenda kufanya nje, nikiwa project manager, na chini yangu kukiwa na expatriates 71. Kwa hiyo ni kitu ambacho kimekuwepo. Na watanzania wengi walio na uwezo na nidhamu, wamepanda, na wengi wapo nje ya Tanzania.
6) Kutolala kwenye premises za kampuni sioni kama ni kitu cha kumsaidia mfanyakazi. Hiyo inamsaidia mwajiri. Inampunguzia gharama za kumhudumia. Pale Buly Barrick walitaka sana wafanyakazi wote wakae nje ya mgodi, tulio wengi, hasa tuliokuwa kwenye senior positions tulikataa.
7) Kazi zote kufanywa na kampuni za kitanzania. Hilo limekuwepo wakati wote. Sera inayoongoza kwenye makampuni haya kufuatia sera ya madini 2010 ni kwamba kunapokuwa na kazi, priority ya kwanza ni kampuni zilizomo ndani ya wilaya, kama hakuna unatafuta kampuni iliyomo ndani ya mkoa, kama hakuna, kazi inakuwa open kwa kampuni yoyote iliyopoTanzania, ikishindikana unatoka nje ya Tanzania.
Mengi yaliyotajwa kwa wasiofahamu wataona ni mapya, lakini yalikuwepo siku zote. Jipya ni hilo la kugawana faida 50/50. Nalo hilo siyo la kupigia vigelegele. Huko Mwadui tulikuwa na 50/50 lakini mpaka leo tumepata nini.
Wengi wasichofahamu, makampuni haya hayapati faida kubwa kutoka kwenye mauzo ya dhahabu baliwanapata faida kubwa kutrade shares. Production inalenga kuwapa confidence shareholders ili shares ziweze kupanda. Mathalani kabla ya Brexit hisa za Acacia zilikuwa na thamani kama ya dola 2.5 hivi. Baada ya Brexit zilipanda mpaka kufikia dola 5. Walioamua kuuza hisa zao walipata faida ya 100%. Wewe kama unasubiria faida ya 50/50 unaweza kusubirimpaka uchoke. Serikali itamiliki 16%, je tutakuwa tunauza hisa na kununua?