Jerry Muro: Tundu Lissu njoo uone

Jerry Muro: Tundu Lissu njoo uone

Anaandika Jerry C. Muro


[HASHTAG]#Taifa[/HASHTAG] la Tanzania limeingia katika Historia ya Dunia Kufuatia Kampuni ya _Barrick Gold_ kukubali kwa mara ya kwanza Kugawana asilimia hamsini kwa hamsini *50/50* ya Faida katika uzalishaji wa Dhahabu nje ya *Asilimia 16* ya Mrahaba na Kodi ambayo taifa itapata.

[HASHTAG]#Nimedadisi[/HASHTAG] katika nchi mbalimbali ambazo Barrick wamefanya uwekezaji kama huu na kugundua Tanzania ndio nchi *PEKEE* ambayo *IMETHUBUTU* na kufanikiwa katika hili, Hongera Tanzania Hongera Rais Mzalendo *Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli* katika kurekebisha kwa vitendo makosa ya watangulizi wako, huu ndio Uongozi *UNAOACHA ALAMA* tukufu, naamini kwa sasa watangulizi wako wanafuraha kubwa ya kuona umesahihisha kwa vitendo pale walipokosea.

[HASHTAG]#Muafaka[/HASHTAG] Baina ya Tanzania na Barrick umewaacha "UCHI" tena nasisitiza "*UCHI WA MNYAMA* " wale wote waliokuwa wakisubiri Tanzania ipelekwe mahakama ya kimataifa kutokana na kuchukua hatua za kuzuia MAKINIKIA, kwangu nasema *SHAME ON YOU!!!* najua wamenielewa na wamesikia, Leo Tanzania imepata Shilingi Bilioni 700 kama hela tu ya kujenga *UAMINIFU*, bado nasubiria tupate kodi yetu, tupate Mrabaha wetu, kisha tugawane faida hamsini kwa hamsini.

[HASHTAG]#Nimefarijika[/HASHTAG] sana na kauli ya Mhe Rais, *Dkt. John Pombe Magufuli* ya kuwataka wawekezaji wengine *WOTE* katika Sekta ya Madini kujitafakari na kuanza kufuata uelekeo wa makubaliano kama Haya na Barrick, sasa tutaanza kuvuna neema kwenye Tanzanite, Almasi na kisha tutaingia kwenye Gesi na Mali asili zingine, Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili ya Uongozi wa Mhe Magufuli, naamini akimaliza miaka Mitano ya kwanza na ile mingine lazima Tanzania tutakuwa "*Donor country*"

[HASHTAG]#Naomba[/HASHTAG] nimalize kwa kufikisha salamu kule Nairobi, mwambieni kulikuwa na sababu ya Mungu kumuweka hai ili aje ashuhudie ukuu wa Mungu kupitia Mhe Magufuli, lile alilosema haliwezekani kwa sasa *LIMEWEZEKANA* na Hatimae Mhe Magufuli ameibuka shujaa na kinara wa kielelezo cha Rais Bora Africa anaepigania *RASILIMALI* za nchi yake, Mungu alisema Muombee sana "*ADUI* " yako aishi miaka mingi ili Ashuhudie Baraka za Mungu kwako, Hatimae maombi yetu yamejibu sasa.

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*Dodoma, Tanzania*
*20/10/2017*
Unashangilia hewa? Mbona hakuna jipya? Waliotufikisha hapa ni chama tawala. Kwanini unawalaumu wasiokuwepo kwenye dhambi hii? Huwajui vizuri wafanya biashara wa madini,furaha yako kwa ajili ya njaa yako itakushtaki siku moja kwa usaliti huu.
 
Nafasi za uteuzi zinatafutwa kwa nguvu skuhizi eeehhhhh.....[emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Yaani kweli hii dunia maajabu hayaishi!!Ukitumikia tumbo badala ya kichwa mawazo kama haya ni ya kawaida kabisa.
 
Bavicha mmekuwa wapole baada ya Acacia kukubali
tapatalk_1508471849675.jpeg

Ukihitaji mkalimani sema nikusaidie tafsiri ya neno kwa neno maana ccm ni kambi ya maiti.
 
Mungu siku zote ni mwaminifu.. Jerry Murro Mungu aendelea kukutunza na akutendee kama uwazavyo ili matakwa yake yatimie kwa dhihaka juu ya binadamu Mwenzako.
 
Jerry Muro.................. tena shukuru Tundu Lissu bado hajapona sawa sawa angekufafanulia vema nini kinaendelea na ungeona aibu haswa...... tulia tuli wewe vijembe vyako vyafaa kwako na Manara Haji hukuu ni kwingine kunahitaji akili na sio taarab kwa kweli.............. Jerry rudi darasani na safari hii soma sheria bado muda unakuruhusu.

By the way una watoto wangapi now? au wewe na mwenzako Bashite ndio hivyo tena
 
Anaandika Jerry C. Muro

Taifa la Tanzania limeingia katika Historia ya Dunia Kufuatia Kampuni ya Barrick Gold kukubali kwa mara ya kwanza Kugawana asilimia hamsini kwa hamsini 50/50 ya Faida katika uzalishaji wa Dhahabu nje ya Asilimia 16 ya Mrahaba na Kodi ambayo taifa itapata.

Nimedadisi katika nchi mbalimbali ambazo Barrick wamefanya uwekezaji kama huu na kugundua Tanzania ndio nchi pekee ambayo imethubutu na kufanikiwa katika hili, Hongera Tanzania Hongera Rais Mzalendo Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli katika kurekebisha kwa vitendo makosa ya watangulizi wako, huu ndio Uongozi unaoacha alama tukufu, naamini kwa sasa watangulizi wako wanafuraha kubwa ya kuona umesahihisha kwa vitendo pale walipokosea.

Muafaka Baina ya Tanzania na Barrick umewaacha "bila nguo" tena nasisitiza "bila nguo kama mnyama" wale wote waliokuwa wakisubiri Tanzania ipelekwe mahakama ya kimataifa kutokana na kuchukua hatua za kuzuia makinikia, kwangu nasema shame on you najua wamenielewa na wamesikia, Leo Tanzania imepata Shilingi Bilioni 700 kama hela tu ya kujenga uaminifu, bado nasubiria tupate kodi yetu, tupate Mrabaha wetu, kisha tugawane faida hamsini kwa hamsini.

Nimefarijika sana na kauli ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwataka wawekezaji wengine wote katika Sekta ya Madini kujitafakari na kuanza kufuata uelekeo wa makubaliano kama Haya na Barrick, sasa tutaanza kuvuna neema kwenye Tanzanite, Almasi na kisha tutaingia kwenye Gesi na Mali asili zingine, Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili ya Uongozi wa Mhe Magufuli, naamini akimaliza miaka Mitano ya kwanza na ile mingine lazima Tanzania tutakuwa "Donor country"

Naomba nimalize kwa kufikisha salamu kule Nairobi, mwambieni kulikuwa na sababu ya Mungu kumuweka hai ili aje ashuhudie ukuu wa Mungu kupitia Mhe Magufuli, lile alilosema haliwezekani kwa sasa limewezekana na Hatimae Mhe Magufuli ameibuka shujaa na kinara wa kielelezo cha Rais Bora Africa anaepigania rasilimali za nchi yake, Mungu alisema Muombee sana "adui" yako aishi miaka mingi ili Ashuhudie Baraka za Mungu kwako, Hatimae maombi yetu yamejibu sasa.

Wasalamu
Jerry C. Muro
Dodoma, Tanzania
20/10/2017
Penye ukweli uongo hujitenga ...BG up [HASHTAG]#magufuli[/HASHTAG]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom