Jerry Muro: Tundu Lissu njoo uone

Jerry Muro: Tundu Lissu njoo uone

Hahahahaha Muro kiboko ya chadema hahahaha
Hana ukiboko wowote Zaidi ya kuota ndoto za mchana. Hivi waliyoingia hiyo mikataba mibovu ambayo leo wanairekebisha walikuwa ni akina nani hasa? walikuwa ni wapinzani au watawala?! Acha huyo jamaa anitafutie ukuu wa wilaya. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuupata.
 
Atakae kuja nae atasema tunaibiwa sanaaa na kusema yale yalikua hewa tu hahahahah..nasikia waungwana wanasema kilichoandikwa na herufi kubwa kumbe yalishakuwepo vile vile isipokua yamerudiwa na kuwekewa maua kwa nje ili ionekane mapya...Mungu ibariki Tanzania
 
Hii ni riwaya ya mtu asiyejua chochote kuhusu uchumi na biashara ya madini. Barrick ndio walioshinda katika hili. We have lost.
 
Kuna kitu watu hawajakielewa. Ukitaka neema kwenye nchi hii kuwa adui wa upinzani. Yaani hutachukua round. Tutaanza kukusikia mh. Fulani.
 
Hapo kweli kazi tuu wamebana wameachia mangufuli ni jembe wamebaki midomo wazi na kutoka mipovu mdomoni sasa tumelipwa malizetu na wazugu kwakua ni Mali zanchietu
 
unajisifa kupewa 0.2%(less than 1%) ya unachodai halafu unashangilia

japo mazungumzo yanaendelea, huoni kwenye mahesabu tume wamepika? that meam ACACIA wako sawa kwa 99.8% mpaka muda huu

Lissu hakukataa kama tunaibiwa ila alisema tunaibiwa kwenye mikataba ndo kitu kilichofanyiwa kazi

Mimi nampongeza Rais na Lissu inawezekana waliwasiliana hata kwenye simu kuona ni jinsi gani wanaibiwa kwenye mikataba
The Elephant, you are the Great Thinker
 
Anaandika Jerry C. Muro


[HASHTAG]#Taifa[/HASHTAG] la Tanzania limeingia katika Historia ya Dunia Kufuatia Kampuni ya _Barrick Gold_ kukubali kwa mara ya kwanza Kugawana asilimia hamsini kwa hamsini *50/50* ya Faida katika uzalishaji wa Dhahabu nje ya *Asilimia 16* ya Mrahaba na Kodi ambayo taifa itapata.

[HASHTAG]#Nimedadisi[/HASHTAG] katika nchi mbalimbali ambazo Barrick wamefanya uwekezaji kama huu na kugundua Tanzania ndio nchi *PEKEE* ambayo *IMETHUBUTU* na kufanikiwa katika hili, Hongera Tanzania Hongera Rais Mzalendo *Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli* katika kurekebisha kwa vitendo makosa ya watangulizi wako, huu ndio Uongozi *UNAOACHA ALAMA* tukufu, naamini kwa sasa watangulizi wako wanafuraha kubwa ya kuona umesahihisha kwa vitendo pale walipokosea.

[HASHTAG]#Muafaka[/HASHTAG] Baina ya Tanzania na Barrick umewaacha "UCHI" tena nasisitiza "*UCHI WA MNYAMA* " wale wote waliokuwa wakisubiri Tanzania ipelekwe mahakama ya kimataifa kutokana na kuchukua hatua za kuzuia MAKINIKIA, kwangu nasema *SHAME ON YOU!!!* najua wamenielewa na wamesikia, Leo Tanzania imepata Shilingi Bilioni 700 kama hela tu ya kujenga *UAMINIFU*, bado nasubiria tupate kodi yetu, tupate Mrabaha wetu, kisha tugawane faida hamsini kwa hamsini.

[HASHTAG]#Nimefarijika[/HASHTAG] sana na kauli ya Mhe Rais, *Dkt. John Pombe Magufuli* ya kuwataka wawekezaji wengine *WOTE* katika Sekta ya Madini kujitafakari na kuanza kufuata uelekeo wa makubaliano kama Haya na Barrick, sasa tutaanza kuvuna neema kwenye Tanzanite, Almasi na kisha tutaingia kwenye Gesi na Mali asili zingine, Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili ya Uongozi wa Mhe Magufuli, naamini akimaliza miaka Mitano ya kwanza na ile mingine lazima Tanzania tutakuwa "*Donor country*"

[HASHTAG]#Naomba[/HASHTAG] nimalize kwa kufikisha salamu kule Nairobi, mwambieni kulikuwa na sababu ya Mungu kumuweka hai ili aje ashuhudie ukuu wa Mungu kupitia Mhe Magufuli, lile alilosema haliwezekani kwa sasa *LIMEWEZEKANA* na Hatimae Mhe Magufuli ameibuka shujaa na kinara wa kielelezo cha Rais Bora Africa anaepigania *RASILIMALI* za nchi yake, Mungu alisema Muombee sana "*ADUI* " yako aishi miaka mingi ili Ashuhudie Baraka za Mungu kwako, Hatimae maombi yetu yamejibu sasa.

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*Dodoma, Tanzania*
*20/10/2017*

Out of context! Sidhani kuna Mtanzania alitaka au alinuia Barrick waipeleke Tanzania kwenye makahama za kimataifa. Actually, kama kusingekuwa na maridhiano pengine tungeishia huko na tushukuru kuwa maridhiano yamepatikana. Hivyo, kudhani kuwa au kufikiria kuwa wale waliotaka tupelekwe kwenye mahakama za kimataifa wameachwa uchi wa mnyama is out of context.
 
Kama nakiona kichwa cha habari kwenye CNN"ILE NCHI ILIYOKUWA INAIDAI ACCACIA DOLLAR BILLION 190 WAMERIDHIA KULIPWA DOLLAR MILLION 300"and am like what the f....!!!mara naona share price za accacia zinaongezeka mara dufu...mwambieni sizonje huu mchezo hauhitaji hasira....
 
Kiboko ya Chadema ni Bashite...

Kama huamini kamuulize Tundu Lissu.
Hahahaha.....
IMG_1508429681813.jpg
 
Unapewa 0.2% ya kile unachodai badala ya kudiscuss alternatives ya kupata stahiki zako unapanua domo kushangilia!!!! Hakika Abhazungu are very Clever.
Watz sio bure tumerwoga.
 
Kama nakiona kichwa cha habari kwenye CNN"ILE NCHI ILIYOKUWA INAIDAI ACCACIA DOLLAR BILLION 190 WAMERIDHIA KULIPWA DOLLAR MILLION 300"and am like what the f....!!!mara naona share price za accacia zinaongezeka mara dufu...mwambieni sizonje huu mchezo hauhitaji hasira....

Lakini pia ukisoma press release ya Barrick makubaliano hayo yako subject to Barrick approval. So, let's be humble rather than being proud.
 
Ingekuwa heri kama mngejishughulisha kuisoma barua kutoka acia imeeleza wazi kwamba ni mpaka aproval yao na mpaka sasa hawajapokea proposal yoyote, sasa sielewi shangwe hizi ni za nini,ndio maana tunaibiwa sana kwenye mikataba ya kimataifa kama hii kwa kuwa hatupendi kusoma
 
Back
Top Bottom