Jenista Mhagama kalipwa sh. ngapi na Azam?

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Jenista Mhagama ametumia muda wa matangazo kuzipigia debe bidhaa za azam, amefanya tangazo la biashara kabisa, Je hii haikinzani na kanuni zao? (just asking!) inawezekana kala mkwanja kufanya alichofanya?
 
Mwenyekiti wa Bunge Jenister Mhagama, wakati wa kipindi cha matangazo mbali mbali (kutambua wageni, ratiba za vikao vya kamati n.k.) amesema ana tangazo ambalo amefikiria ameona si vibaya likitangazwa.

"Waheshimiwa Wabunge Kampuni ya AZAM inawatangazia waheshimiwa wabunge kwamba watumie bidhaa za Azam... (kicheko ukumbuni!) ...aidha, AZAM inawatangazia wabunge kwamba bidhaa za AZAM ni bora kwa afya."

Ndugu zangu, hii ni sawa? Serikali (na hususan Bunge) kazi yake moja kubwa ni kusimamia, ku monitor, mienendo ya biashara nchini. Kitendo cha Bunge kutangaza biashara za Bakhressa ni kinyume na maadili ya utawala bora, na si jambo la kufanyia utani na kuchekeshea bungeni. Utawezaje kumratibu mfanyabiashara ambae unamtangazia biashara yake wewe mwenyewe?

AZAM amelipia shilingi ngapi, na wamemlipa nani (Jenister Mhagama?) kutumia muda wa bunge na wa TBC kutangaza biashara? And why AZAM? Kamati ya maadili ya Bunge iko wapi, viongozi wa Bunge mbona mnashusha viwango vya bunge hili namna hii?
 
Jenista Mhagama ametumia muda wa matangazo kuzipigia debe bidhaa za azam, amefanya tangazo la biashara kabisa, Je hii haikinzani na kanuni zao? (just asking!) inawezekana kala mkwanja kufanya alichofanya?

Simba hoyeeeeee
 
mh sidhani kama inafaa wanalishushia tu bunge letu tukufu heshima!!!
 
Hii ndio Tanzania, tatizo hawa viongozi wetu wameshatuona sisi mabwege na hata wafanye nini sisi hatuna uwezo wa kuwakemea kwa sababu ya UOGA wetu na kukosa UZALENDO kwa nchi yetu!!
 
Pia ameipigia debe shule anayosoma mtoto wake.
Nadhani tatizo ni uwezo mdogo wa kufikiri na kutambua dhamana aliyonayo.
Tatizo la uwezo mdogo wa kuelewa masuala linawakabili wabunge wengi wa ccm

inawekana akawa mwepesi kiasi hiki? atakua kapewa pesa, unajua watu wengi wanafatilia bunge, kwa kupitia redio, tv, na hata mitandao sasa mfanyabiashara akifanikiwa kupenyeza matangazo yake mjengoni anakua kapata bonge slope, yule mama nahisi atakua kawezeshwa sio bure
 
mwenyekiti wa bunge jenister mhagama, wakati wa kipindi cha matangazo mbali mbali (kutambua wageni, ratiba za vikao vya kamati n.k.) amesema ana tangazo ambalo amefikiria ameona si vibaya likitangazwa.

"waheshimiwa wabunge kampuni ya azam inawatangazia waheshimiwa wabunge kwamba watumie bidhaa za azam... (kicheko ukumbuni!) ...aidha, azam inawatangazia wabunge kwamba bidhaa za azam ni bora kwa afya."

ndugu zangu, hii ni sawa? Serikali (na hususan bunge) kazi yake moja kubwa ni kusimamia, ku monitor, mienendo ya biashara nchini. Kitendo cha bunge kutangaza biashara za bakhressa ni kinyume na maadili ya utawala bora, na si jambo la kufanyia utani na kuchekeshea bungeni. Utawezaje kumratibu mfanyabiashara ambae unamtangazia biashara yake wewe mwenyewe?

Azam amelipia shilingi ngapi, na wamemlipa nani (jenister mhagama?) kutumia muda wa bunge na wa tbc kutangaza biashara? And why azam? Kamati ya maadili ya bunge iko wapi, viongozi wa bunge mbona mnashusha viwango vya bunge hili namna hii?

tundu lissu alikuwepo? Mbona hakusimama leo
 
Mleta mada kwanza declare interest, je wewe ni mpenzi/mshabiki wa Simba SC? MAANA HATA MIMI HAPA NAENDA KUNUNUWA BIDHAA ZA AZZAM sasa hivi.
 
Hii nchi ni ya kitu kidogo. Hapo lazima Jenista Muhagama kapewa kitu kidogo. Kwa misingi na mantiki hii nchi yetu imeingia katika hali mbaya sana.
Wabunge, na hasa viongozi wa bunge haoneshi heshima kabisa wakiwa bungeni. Wamekuwa na tabia ajabu sana. Ee Mungu wasaidie waweze kuona watendalo, na wawezeshe wajue wanayopaswa kutenda kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
 
Pasi na shaka yoyote mleta mada ni mshabiki wa SIMBA.

Pole sana. Kule kwetu Znz ( ipokuna barza moja maarufu sana)ipo sehemu pale malindi inaitwa Simba chai(utaona simba kapakatwa kisha ananyweshwa Chai) sasa kwa hili sima kapakatwa na kunyweshwa juisi tatu za Azam.
Pole sana
 
Mleta mada kwanza declare interest, je wewe ni mpenzi/mshabiki wa Simba SC? MAANA HATA MIMI HAPA NAENDA KUNUNUWA BIDHAA ZA AZZAM sasa hivi.

azam wamefanya makusudi kwa sababu jana wamewapa kichapo simba sc(team ya zitto kabwe:happy:), kwa hiyo hapo ilikua kama vile wameweka utani wa mpira, na mimi kwa vile ni mshabiki wa yanga na mi leo hii naenda kununua bidhaa za azam coz jana wamenifurahisha sana :biggrin1:
 
Ni mambo ya mpira tu,tusiweke ktk uhalisia...na mda wa matangazo ulikuwa unaruhusu!alitaka kufikisha ujumbe kwa mashabiki wa Simba...ni kweli jana mnyama kapakatwa...tena ajabu kalainika kwa hugongwa Ice-cream tu!Msishutumu Muhagama
 
Pasi na shaka yoyote mleta mada ni mshabiki wa SIMBA.

Pole sana. Kule kwetu Znz ( ipokuna barza moja maarufu sana)ipo sehemu pale malindi inaitwa Simba chai(utaona simba kapakatwa kisha ananyweshwa Chai) sasa kwa hili sima kapakatwa na kunyweshwa juisi tatu za Azam.
Pole sana
Naam sheikh Barubaru,
Habari za swaumu Sheikh wangu.
 
Hii nchi ni ya kitu kidogo. Hapo lazima Jenista Muhagama kapewa kitu kidogo. Kwa misingi na mantiki hii nchi yetu imeingia katika hali mbaya sana.
Wabunge, na hasa viongozi wa bunge haoneshi heshima kabisa wakiwa bungeni. Wamekuwa na tabia ajabu sana. Ee Mungu wasaidie waweze kuona watendalo, na wawezeshe wajue wanayopaswa kutenda kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
mimi tangia siku nilipomuona huyu mama anaongea mchana kweupeee kuwa "waliomtake Dr. Ulimboka Stephen walikuwa wamevaa nguo kama za polisi kwa hiyo watakuwa ni CDM maana ndio huvaa magwanda yanayofanana na hizo nguo" ndipo taingia siku hiyo imani ikaniishia juu yake.
Na bahati nzuri Mwanasheria mkuu alinipa mwanga baadae kuwa 'vichwa sio kwa ajili ya kuotesha nywele'

Back
Top Bottom