Jengo la Makao Makuu ya TANESCO Ubungo kubomolewa wakati wowote kupisha ujenzi wa 'Interchange'

Dr Magufuli huyu m baba hajawahi kuniangusha aisee!

Sheria ifuate mkondo wake, ujenzi wowote uliopo hifadhi ya barabara bomoa tu mwenyewe kabla rungu halijakufikia
 
Umeongeo uongo sana, na inaonekana uwezo wa kuelewa mambo ni mdogo sana. Mh Rais jana alikuwa anazungumzia sheria ya na mabadiliko yake mpaka 2007. Na akasema sheria ilishapitishwa na bunge upana wa barabara, kwahiyo hao wanaolalamika wakati wako ndani ya hifadhi ya barabara hakuna jinsi. Ndio akatolea mfano kwamba kuna inter change itakayojengwa ubungo, huenda ikawa na gholofa mbii au tatu. Ujenzi utakapo anza ndio wataona kama kuna haja ya kulibomoa jengo la Tanesco, akimaanisha ubomoaji hauwahusu wananchi tu, hata majengo ya serikali. Sasa uelewa wako mdogo umekuja na hiyo thread ya udogo wa ufahamu wako wa akili. Pole sana, ndugu yetu Lisbon.
Mkuu, sasa umekanusha ama umefanyaje? Maana nashindwa kukuelewa hata kidogo. Hoja hapa ni kubomolwa kwa jengo la TANESCO kupisha ujenzi wa Interchange. Jengo hilo lipo kwenye road reserve na kwa vyovyote vile lazima libomilewe. Wakati mwingine tunapaswa kutafakari kabla ya kuandika vinginevyo tunaonekana kichekesho
 
Ila kweli lizaboni kaongeza chumvi. Yale mazungumzo ya mheshimiwa na makonda hayakuwa na maneno yanayoashiria "kubomolewa wakati wowote". Jpm alifafanua sheria husika na kuonyesha kuwa majengo ya serikali kikiwemo la tanesco yanaweza kubomolewa wakati ukifika.
 
Hakuna mwenye hasara!!!!!! Jengo la Umma, Shirika la Umma.
Dhamana ya Ardhi ni ya Wizari husika, ni vyema sasa mipangilio ya matumizi bora ya Ardhi ikasimamiwa na Wizara husika.
Umefika wakati muaafaka wa Alama kuu itakayotenganisha maeneo ya miundo mbinu na makazi iwekwe 1/1 na wizara kama m50, m70, m100, ndo yawepo makazi ama maofisi
 
Kama hili likitekelezwa nitampa hongera zake JPM.It will send a signal that no body is above the law.Hata hivyo bado tunasubiri mafisadi kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi.Wengi wetu bado tunaona kuna double standards na hakuna dhamira ya kweli ya kushuhulikia mafisadi.Wengine wanashuhulikiwa kwa nguvu zote na wengine wanawekwa viporo!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.
 
Mkuu, sasa umekanusha ama umefanyaje? Maana nashindwa kukuelewa hata kidogo. Hoja hapa ni kubomolwa kwa jengo la TANESCO kupisha ujenzi wa Interchange. Jengo hilo lipo kwenye road reserve na kwa vyovyote vile lazima libomilewe. Wakati mwingine tunapaswa kutafakari kabla ya kuandika vinginevyo tunaonekana kichekesho
Nenda pale kapima meter kutoka katikati ya barabara mapaka lilipo jengo la Tanesco ndio utajua nini naongea. Nikusaidie tena inter change ya gholofa haina upana wa meter 22.5 ndugu yangu, hizo fani za watu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.

Hizi akili zingine jamani tutaingia hasara sana, hivi hawa watu wamewahi kuwaza kama wakijenga flying over katika eneo hilo gharama yake ikoje. Hili jingo naona litabaki hapo kuliko hii biashara ya kuchezea raslimali zetu. Kumbukeni ni kiasi gani kimetumika kujenga hapo plus inflation ya gharama mtuhurumie kwa makodi mnayotubebesha hatusongi Mbele kwa mipango hisiyoeleweka.
 
Safi sana, majengo yapishe miundo mbinu yenye manufaa kwa wengi.

TANESCO ni wakati muafaka wahamie Dodoma, katikati ya nchi.
 
Hizi akili zingine jamani tutaingia hasara sana, hivi hawa watu wamewahi kuwaza kama wakijenga flying over katika eneo hilo gharama yake ikoje. Hili jingo naona litabaki hapo kuliko hii biashara ya kuchezea raslimali zetu. Kumbukeni ni kiasi gani kimetumika kujenga hapo plus inflation ya gharama mtuhurumie kwa makodi mnayotubebesha hatusongi Mbele kwa mipango hisiyoeleweka.

Mkuu tukianza kuangalia hasara Kuna vitu vingi nchi hii havitafanyika
 
Nenda pale kapima meter kutoka katikati ya barabara mapaka lilipo jengo la Tanesco ndio utajua nini naongea. Nikusaidie tena inter change ya gholofa haina upana wa meter 22.5 ndugu yangu, hizo fani za watu.
Ndugu yangu. Yaonekana uelewa wako ni mdogo sana. Umbali wa mita 22.5 ni kutoka pale Makutano ya Barabara ya Mandela na Morogoro. Kutoka Ubungo hadi Kibaya upana wa barabara ni mita 30 na hii ipo kisheria. Kabla hujaandika kitu jaribu kuwa makini na ujiridhishe juu ya hicho ukiandikacho. Nenda kapime barabara kutoka pale kwenye makutano kuelekea Posta na kuanzia kwenye mataa kuelekea Mbezi utaona upana ni tofauti. Na hii ni kwa sababu pale lamewekwa kama filter. Si magari yote yanayoingia Dar yatapita barabara ya Morogoro. Mengine yanatumia barabara ya Mandela ambayo ni mengi hasa yale ya Mizigo. Mengine hutu,ia barabara ya Sam Nujoma
 
Waliompa hela za Kulibomoa wampe na hela za kulijenga upya (ku replace).
Tena tunataka lenye hadhi sawa na lile au zaidi ya hilo.
Siyo kukurupuka kama mlivyo kurupuka kwenda Dodoma mukatujengee vigorofa vya ajabu ajabu!!
 
Back
Top Bottom