Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30

Mkuu MM


-Kuna madudu mengi sana NSSF ila huwa yanafunikwa na POAC na mpaka leo sijawahi kuelewa kwanini huwa hawayasemi...Time will tell


-Hata mwaka jana baadhi ya wabunge kushabikia shirika kujiingiza kwenye mradi wa umeme zaidi ya bilioni 300...yaani kila jambo NSSF ,Wanachama wao hawashirikishwi....bomu likija kulipuka sijui itakuwaje?


-ukiangalia hata sheria mpya wanazoziweka sasa ni kulinda wizi huu coz pesa nyingi imewekezwa kwenye issue ambazo hazilipi




sina uhakika na malengo yao kwa sasa,vision yao ni ipi ila nitaanza kufanya uchunguzi..why huwa hawagusi...
 
NSSF ni shirika la jamii ambalo linaongozwa kwa sheria ya mashirika ya jamii inayotaka fedha zake kuwekezwa ndani ya nchi na asset zisizohamishika etc..lakini NSSF hawafuati hizi sheria pengine siasa imeingia sana humo maana ndipo watu wanapopatia ulaji sasa hivi. Nimesikia NSSF imeinvest sijui ni Bulgaria, kinyume na sheria zinavyosema..anyway....pia mojawapo za ofisi zake zimehama kutoka jengo walilokuwa wanalipa $5 per sq m kwenda jengo la mkuu mmoja ambalo wanalipa more than three times of the previous amount hali katika majengo yote ya NSSF hakuna linalokodishwa that pricy..

Ninachojaribu kudeduce ni kuwa..hawana umakini katika kuinvest fedha wa wanachama...if they continue like this..in less that 15 yrs watakuwa bila bila..
 
Machinga Complex ile kwa ilipofikia sasa hali mbaya,maana wamachinga wenyewe hawataki kufanya biashara inabidi irudi kwa NSSF ili watafute maofisi yaingie pale yafanye kazi.

Kama serikali inataka kusaidia wamachinga wachukue pesa zao wenyewe za kodi za manispaa.

Mimi nipo kwenye mchakato wa kuchukua pesa zangu kutoka NSSF... nimeshahamia PPF
 
Na Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?

Mwanakijiji,

Unajua haya ni matatizo ya siasa kuingia kwenye mambo nyeti!

Regulator wa mapensheni ilikuwa aje zamani sana lakini wanasiasa wamekuwa wakipinga muda mrefu. Jambo la kutia kichefuchefu zaidi ni kwamba hii mifuko ipo chini ya wizara ya kazi na ajira. Jiulize wizara ya ajira na kazi ina uwezo gani wa kusimamia mifuko ya pensheni? Na hawa jamaa wa wizara ya kazi na viongozi wa mifuko walikuwa wabishi mno kuruhusu hii mifuko ihamishiwe wizara ya fedha ambapo walijua kabisa wakifika kule watawekwa chini ya usimamizi wa BOT. Na hapo ndio ingekula kwao maana BOT dept ya Supervision ingekula nao sahani moja.

Sasa turudi kwenye swali lako kuhusu uwekezaji hawana jamaa hawana msimamizi anayewaambia wawekeze vipi kwahiyo ni utashi tu wa managament na wakipata support ya Board of Directors imetoka!. Akija Regulator sasa utasikia habari yake maana wataambiwa wa DIVERSIFY waweke kidogo kwenye dhamana za serikali, kidogo kwenye Account za riba, kidogo kwenye Real Estate labda 15% ( ambako wao naona wameshazidi hata 30%).

Huwezi kusikia mabenki yanayumba hovyo kwa sababu yanafanya kazi kwenye misingi hiyo na BOT kila siku wanawaangalia ni kiasi gani wameweka wapi! wakipitiliza tu wanapigwa STOP!!
 
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.

ritz, nakubaliana na wewe kabisa na hakuna namna ya kulinusuru hilo jengo zaidi ya kuboa hivyo vizimba na kulifanya liwe 'soko'. Wangejaribu kusoma mazingira wanayofanyia biashara wamachinga na ku-reflect hiyo style kwenye hilo jengo, lakini sio kujengea vijumba vya panya!
 
Last edited by a moderator:
ritz, nakubaliana na wewe kabisa na hakuna namna ya kulinusuru hilo jengo zaidi ya kuboa hivyo vizimba na kulifanya liwe 'soko'. Wangejaribu kusoma mazingira wanayofanyia biashara wamachinga na ku-reflect hiyo style kwenye hilo jengo, lakini sio kujengea vijumba vya panya!

naomba mnipanue mawazo kama nitakosea nijuavyo mimi kwa majengo ya mjini hususani jiji la Dar huwa yanapanda thamani kila siku iwapo hao jiji wameshindwa kulipa hilo deni NSSF watakuwa na haki za kulikamata jengo au mali zilizodhamini mkopo huo . si shauri NSSF waingie kufanya biashara nyingine katika jengo hilo nia iwe kurudisha pesa zetu hata kama jengo litauzwa kwa thamani ya sas kwa Deweji or Azam.
 
akata la jengo la Machinga Complex lililoko Ilala, Dar es Salaam limebainika kuendesha biashara ambayo hailipi na imeshindikana kulipa deni la mkopo wa ujenzi wake.

Jengo hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lilijengwa kwa mkopo kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sh. bilioni 12.9.

Kutokana na kufanya biashara isiyolipa na kushindwa kulipa deni la mkopo huo, NSSF imesema kuwa jengo la Machinga Complex limeshindwa kurudisha fedha hizo ambazo lilizitoa kwa Jiji la Dar es Salaam kama mkopo.

Jengo hilo la ghorofa lilijengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapatia wamachinga waliozagaa jijini sehemu ya kufanyia biashara zao.

Hadi sasa Jiji limeshindwa kulipa mkopo huo wa NSSF, ambalo kwa sasa deni linakadiriwa kufikia Sh. bilioni 30 kutokana na ongezeko la riba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya NSSF, Manispaa ya Ilala na Jiji la Dar es Salaam, fedha za kulipia deni hilo zilitarajiwa zitokane na kodi ya jengo hilo ambalo kwa sasa lina idadi ya wamachinga 5,000 waliopanga kwenye vizimba vya kufanyia biashara.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa NSSF, Eunice Chiume, amethibitisha kwamba shirika lake mpaka sasa halijalipwa fedha zozote kama sehemu ya kulipia mkopo walioutoa kwa Jiji la Dar es Salaam.

Chiume alilihakikishia NIPASHE kwamba Jiji halijaanza kulipa fedha hizo, huku akikataa kuingia kiundani katika suala hilo ambalo hivi karibuni limekuwa likizua maswali mengi.

Awali wakati wa ujenzi huo unaanza, serikali ilijigamba kwamba ungekuwa na tija ikiwemo kujiendesha kwa faida na kuwahudumia wamachinga wanaozagaa hovyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, mradi huo hivi sasa umeshindwa kutekeleza malengo hayo sambamba na kushindwa kulipa deni la NSSF.

KAULI YA ZUNGU
Mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu, ambaye alikuwa katika bodi ya ujenzi wa jengo hilo, aliliambia NIPASHE kuwa kazi aliyokuwa amepewa ni kuwakusanya wamachinga na kuwaingiza katika jengo hilo ili wafanye biashara.

Zungu alisema kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi na kufanikiwa kupata wamachinga 5,000 ambapo kila mmoja alitakiwa kulipia kizimba chake Sh. 60,000 kwa mwezi kama kodi.

“Mimi kazi yangu ilimalizika baada ya kuingiza wamachinga 5,000 ili wafanye biashara katika jengo hilo, lakini kazi ya kuhakikisha wanadumu hapo bila kuhama pamoja na kulipa kodi hilo siyo suala langu tena,” alisema Zungu.

Hata hivyo, taarifa kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema kuwa baadhi ya watalaamu wamekuwa wakishauri yawekwe mabango ya matangazo juu ya jengo hilo ili kusaidia kulipa deni hilo, lakini suala hilo linakwamishwa kutokana na vitendo vya ufisadi.

Taarifa hizo zinasema kuwa kama ushauri huo ungekubalika na kutekelezwa, jiji lingeweza kupata zaidi ya Sh. milioni 30 kwa mwezi kutokana na mabango ya matangazo ambazo zingesaidia kulipia mkopo wa NSSF.

MEYA MASABURI
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alipotafutwa hivi karibuni kuzungumzia sakata hilo, aliitupia lawama Manispaa ya Ilala kwa maelezo kuwa ndiyo ilikuwa inashughulika na utaratibu wa kuwaingiza wamachinga katika jengo hilo.

MKURUGENZI ILALA AKOSOA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, alipotafutwa na NIPASHE ili kutoa ufafanuzi wa sakata hilo, alithibitisha kuwa mradi huo haulipi kama ilivyotarajiwa na waliotoa wazo la kuuanzisha.

Aidha, Fuime alithibitisha kwamba mabilioni ya fedha yalitumika katika kujenga jengo hilo, lakini akaweka bayana kwamba ni mradi ambao hauna faida.

Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ilala aliongeza kwamba mapato kutoka kwa wamachinga hayatoshi kulipia deni la NSSF ambalo kwa sasa linazidi kuongezeka kutokana na riba.

Fuime alithibitisha kuwa Manispaa ya Ilala ilishirikishwa katika kuanzisha mradi huo, lakini alisema walioingia katika mkataba ni Ofisi ya jiji la Dar es Salaam pamoja na NSSF.

“NSSF walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo huku jiji likitoa ardhi kama dhamana yake katika kukamilisha mradi huu,” alisema Fuime.

Alisema mradi wa jengo hilo haulipi kwa kuwa wafanyabishara ndogondogo waliokuwa wamekusudiwa kupewa hawana uwezo wa kulipa fedha ili NSSF warudishe mtaji wao pamoja na riba.

Kwa mujibu wa Fuime, ujenzi wa jengo hilo ulifanyika bila kufanyika utafiti wa kina kubaini aina ya jengo lililotakiwa kujengwa pamoja na eneo lilipotakiwa kuwekwa.

Fuime alisema kuwa kutokana na mambo hayo kutozingatiwa, ndiyo maana NSSF inacheleweshwa kulipwa deni lake na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa shirika hilo kuchelewa kupata fedha hizo.

“Mmachinga anatakiwa kujengewa jengo la kawaida ambalo siyo ghorofa na kama likiwa ghorofa basi iwe ghorofa moja, lakini sio kama lile jengo la sasa la Machinga Complex ambalo lina ghorofa zaidi ya mbili,” alisema Fuime.

Aidha, Fuime aliliambia NIPASHE kuwa jengo la aina ile lilitakiwa kuweka soko la wamachinga pamoja na kuwa katika kituo cha daladala ili kuvutia wateja.

Fuime alikiri kuwa siasa ni miongoni mwa vitu vinavyochangia kukwamisha juhudi za watalaamu wanaotaka kubuni njia mbadala za kuwavuta wamachinga wengi ili waingie katika jengo hilo na kufanya biashara.

“Mtalaamu akisema hivi anakuja mwanasiasa anasema acheni watu wangu msiwaguse kwa hiyo mnajikuta mnashindwa kufanikisha miradi mbalimbali inayobuniwa kitalaamu,” alisema.

Aidha, alisema wamachinga waliopewa vizimba katika jengo hilo wengi wao hawakustahili na kwamba waliostahili hawakupata fursa hiyo.

Alifafanua kuwa utaratibu uliotumika kuwaingiza wamachinga hao ni kuwatumia viongozi vya vyama vya wafanyabishara hao na kwamba taratibu kadhaa zilikiukwa.

“Kutokana na makosa hayo yote niliyosema, ni vigumu jengo la Machinga Complex kutengeneza faida hata kama lingekuwepo miaka mingapi kwa kuwa wapangaji wake ambao ni wafanyabiasha ndogo ndogo hawana uwezo wa kulipa mapato ya kutosha,” alisema.

MAONI YA WAMACHINGA
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo waliozungumza na NIPASHE walisema wakati ujenzi wa jengo hilo unaanza waliamini watapata sehemu nzuri ya kufanyia biashara zao, lakini bahati mbaya eneo hilo limekuwa halilipi kwa kuwa hakuna wateja.

Said Haule, alisema watu waliopewa vizimba vya kufanyia biashara siyo wenzao kwa kuwa walichukuliwa watu wengine na kugawiwa huku wao wakibakia katika soko la Karume.

Haule alisema hakuna mmachinga mwenye mtaji mdogo wa mashati matano ambaye anahitaji kuwa mpangaji katika ghorofa kama lile la Machinga Complex.

John Mwakyoma alisema wamachinga wengi waliokuwa wamelengwa kufanya biashara katika jengo hilo wameachwa nje.

Alisema mbali ya kuachwa nje na kukosa nafasi katika jengo hilo, lakini pia wamachinga waliopewa vizimba wameshindwa kufanya biashara vizuri kwa kuwa ni vidogo pamoja na eneo hilo kutokuwa na wateja.
Mkopo wa NSSF kwa ajili ya Machinga Complex ni moja ya mikopo iliyotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2010/11 kuwa ya utatanishi inayoweza kusababisha fedha za wanachama kupotea.


CHANZO: NIPASHE

My Take:
Well..what can I say...

Kuna ulazima na hawa NSSF wakafanyiwa auditing ya Maana coz Utaskia tu wamepata hasara hapa mara kuleee....kuna harufu ya ufisadi kwny hii organisation naamini hivyo. Recently nimesikia SERIKALI inadaiwa mabilioni na hakuna sign ya kulipa. Cjui kuna umuhimu WA kuicheki hii.
 
Kuna ulazima na hawa NSSF wakafanyiwa auditing ya Maana coz Utaskia tu wamepata hasara hapa mara kuleee....kuna harufu ya ufisadi kwny hii organisation naamini hivyo. Recently nimesikia SERIKALI inadaiwa mabilioni na hakuna sign ya kulipa. Cjui kuna umuhimu WA kuicheki hii.

Kwa hali ya sasa sioni kama kuna hatua yoyote ya maana itachukuliwa dhidi ya haya mashirika. Kaangalie safu ya Board ndio utajua mkorogo ulipo! Pia angalia Board wa WAMA utapata mwanga zaidi!
 
Kuhalisia hata deni lisipolipika NSSF itakuwa imepata hasara ya mtaji yaani TShs.12.9 billion na siyo TShs. 30 billion. Riba nijuavyo mimi inaingizwa kwenye vitabu inapopokelewa
 
Mkuu mwanakijiji hebu niambie kama kwenye hiyo hasara michango yangu inahusika...


NSSF ni shirika la hifadhi la jamii but siasa zimekuwa too much ndani yake..

nimehamia ppf.

Hivi zile milioni 50 alizokopaga Sumaye hapo NSSF alirudisha? na ilikuwaje NSSF ikamkopesha mtu asiye mwanachama?

Ipo sana, tena sasa wanapanga kukulipa utapofikisha miaka 60, hata kama utastaafu na mika 50 na kama pesa yenyewe itakuwepo.Imekula kwako
 
Kinachokera ni kuwa nssf hawajaingia hasara ya fedha yao...hiyo ni hela inatokana na makato wanayofanyiwa wafanyakazi wanaoishi maisha magumu na ya kudunduliza...na wanapostaafu wanahenyeka kupata visenti vyao hivyo ambavyo nssf inavitumia kuchezea kamari za uwekezaji!!!
 
Nyakati zile ndio Wanamtandandao walikuwa kwenye fungate na ushirika mzuri...........Meya wa jiji aliyekuwepo (Adam Kimbisa - swahiba mkubwa wa mkuu wa nchi na Edward lowassa) alikuwa na hamu isiyokuwa na kipimo kufanya jambo litakalompa sifa ya kisiasa...na kwa kuwa kiranja mkuu wa mawaziri ni swahiba suala mchakato wa kupata pesa NSSF halikuwa gumu.

Jenga jengo la wamachinga mengine yatafuata baadaye......................na likajengwa.
 
1. Mmachinga hajengewi duka kama ambavyo mmasai hajengi nyumba ya matofali kule Ngorongoro.
2. Wamachinga wangapi wanaweza kulipa kodi ya 60,000Tsh kwa mwezi?
Hii project haikuwa na due diligence yeyote! La kufanya sasa ni kuwaza jinsi ya kutumia hilo jengo kufanya vitu vingine vitakavyolipa. Nafuu walete watu wenye maduka Kariakoo waje na wawape incentive kama kutolipa kodi kwa mwezi, nk! Mbona wanafanya haya mambo kwa wazungu na wachimba madini?
 
Vibanda walipewa waheshimiwa ili wawakodishe machinga kwa bei ya juu. Hapo ndipo mchezo ulipoanza haribika.
 
Waziri anayehusika na shirika hili akae mkao wa taahadhari (wabunge na wadau tumeliona hili) au achukue hatua zinazostahili kwa bodi kwa kuzembea na kupitisha miradi magumashi ambayo hailipi na vile vile kushindwa kwa bodi hiyo kuwachukulia hatua watendaji ndani ya shirika hilo kwa kusababisha hasara hii.
 
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?


Bado uwekezaji daraja la kigamboni!!! Subiri twende tu!!
 
Umeongea point ndugu. Vijana wanatakiwa wabaki uko walipo ili wajiajiri. Na sio kukimbilia dar es Salaam.

Swali linakuja: watabakije uko walipo, wakati hapalipi??? Miundo mbinu mibovu, na hakuna huduma za afya??

Ndo maana tunataka states gvt. Kila state iwe na vipaumbele vyake. Sio kupangiwa na waziri anayeishi Dar es Salaam. Kila state iwe na Dar es Salaam yake. Ikuze miji yake, na kuleta internal investment bila kupangiwa na waziri au Rais anayeishi Dar es Salaam.

Utashangaa watu wa Geita wanakimbilia Dar es Salaam, wakati Geita wameacha madini. Utashangaa watu wa Musoma wanakimbilia Dar es Salaam, wakati Musoma wameacha Dhahabu.

Turudishe madaraka kwa wananchi, ili wanafaike na rasili mali zao. Tuacha mfumo wa waziri mmoja kuwapangia wanaGeita wafanye nini? WanaGeita wajipangie wenyewe nini cha kufanya kwa maslahi yao, na taifa kwa ujumla.

Kwa hili la Machinga complex, ni mfano dhahiri kwamba. Serikali inataka Tanzania yote iamie Dar es salaam. Vijana watoke uko vijijini waje kuuza mitumba Dar. Na ni kweli, kutokana na maisha magumu uko vijijini. Kila kijana anataka kuja Dar es Salaam

Umezungumzia serikali za majimbo bila kujua, naiunga mkono sera hii, itatusadia sana
 
Lile jengo haliku dizainiwa ki biashara. Wachoraji wa lile jengo hawakushirikisha wafanya biashara kupata ushauri.

Nna uhakika bado linaweza likaleta faida nzuri tu ikiwa atapewa mfanya biashara kuliendesha na wamwache ali re design atakavyo, theme itakuwa ni hii hii ya kuwawacha "chinga" wafanye biashara zao lakini mtazamo uwe tofauti.
 
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.

Ni JK alisema hayo na bado ameahidi tano nyingine!!!!! Haya ndiyo madhara ya kutofanya tafiti makini kabla ya kutoa maamuzi.
 
Back
Top Bottom