Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30

Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30

Mimi nasubiri kuchangia kwenye uozo wa PPF japo uhuru wa threads za PPF uko mikononi mwa moderators. Talking of PPF means uhaini ndani ya JF but talking of Dau and NSSF is seen to be ok. MM Tusaidie Mods asizuie threads zinazoongelea Erio wa PPF. Tunaamini Erio na Dau wote wanahaki ya kujadiliwa kama viongozi wa mashirika ya umma pale wanapoupeleka umma shimoni
 
Zungu alisema kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi na kufanikiwa kupata wamachinga 5,000 ambapo kila mmoja alitakiwa kulipia kizimba chake Sh. 60,000 kwa mwezi kama kodi.

Does this make economic sense.., 60,000/= kwa mwezi ??? , hapo tunaongelea machinga (wachuuzi / middle men / au wafanyabiashara wadogo wadogo).., ?

Kwa maisha ya sasa ya machinga wengine kutokupata hapa pesa ya kunywa chai kweli wanaweza kupata buku mbili kwa siku ya kulipa pango (tena ukizingatia biashara zao nyingi zinafanana, hence wakikaa sehemu moja competition inazidi).., kumbuka machinga wengine ni watu wanaopewa bidhaa na wauza maduka daily ili wawauzie hawana hata pesa ya mtaji
 
Vile vizimba vya lile jengo ni kama VIZIMBA VYA MAHAKAMANI, ni kachumba kadogo tu..very tiny..mtu mwenye mwli mkubwa kama mMkapa au John Komba pale ndani akiingia hageuki..
 
Discuss the issue that has been brought on the table, don't personalize the issue. Mzee Mwanakijiji amenukuu tu hiyo habari na yeye si chanzo chake, so what is your point here? Further more, kilichoandikwa ndio hali halisi na kielelezo cha uwekezaji usio makini unaofanywa na NSSF na mifuko mingine ya penshion. Ulitaka isijadiliwe?

Jaman kwa mjibu wa taarifa ya gazeti huo ni mkopo ambao jiji lilipewa kama ni uwekezaji wa NSSF hiyo riba inatoka wapi? tuwe makini.
 
Sizani kama tatizo la Machinga Complex ni NSSF, bali ni tatizo la wanasiasa la kutaka "kutowabughuza" wapiga kura! Tatizo kubwa la Machinga Complex ni kutokuwapo na wafanyibiashra pale.....na hii inatokana na uwepo wa soko la Mchikichini lililopo umbali mfupi tu toka Machinga Complex.
Kama pasingekuwa na upuuzi wa kuleta siasa kwenye serious issues, ilikuwa kwanza kufunga Soko la Mchikichini! Ingawaje wamachinga wanalalamika kwamba waliopewa hawakustahili, lakini bado kuna wengi tu wanaostahili ambao wamepewa lakini hawafanyi biashara kwa madai kwamba hakuna wateja. Na kimsingi, ni kweli wateja pale ni adimu kutokana na uwepo wa Soko la Mchikichini.
Madai kwamba pale hakuna kituo cha daladala nayo ni ya kipuuzi kwavile Barabara ya Kawawa inapita pale machinga Complex....na barabara hii inaunganisha maeneo mbali mbali ya jiji.....Magari kutoka Mbagala/Temeke hadi Kawe, yanapita hapa...so, unaweza kuona hapa katikati kuna maeneo mangapi...to mention few kuna keko, kigogo, mapipa, kinondoni (iliyo along Kawawa rd) , Mikocheni hadi Kawe! Magari ya Gongo la Mboto kwenda Masaki, yanapita hapa....Buguruni Masaki, yanapita umbali usiozidi meta mia 2, Buguruni, kigogo, Tabata kwenda city centre, yanapita hapa...kwahiyo hakuna hoja ya msingi ya kutokuwapo kituo!!
Solution ya Machinga Complex ni kuzuia kufanyika biashara pale Mchikichini....lakini kwavile wanaogopa kuwaondoa wapiga kura, ndo chanzo cha yote haya!!! Hivyo, sizani kama ni sahihi kuilamu NSSF.
Kwa upande mwingine Watanzania tuna matatizo sana. Pale SUA zamani walishawahi kufanya utafiti na ku-introduce mbegu moja ya mtama ambayo inaazaa sana tena kwa muda mfupi! Lengo, ilikuwa kukabili njaa hususani maeneo ya ukame...kwamba wapate mbegu inayokamaa mapema na kutoa mavuno mengi! Kama kawaida yetu, Wananchi wakawa hawaitaki ile mbegu, kisa eti sio mzuri kwa Pombe!
 
Jaman kwa mjibu wa taarifa ya gazeti huo ni mkopo ambao jiji lilipewa kama ni uwekezaji wa NSSF hiyo riba inatoka wapi? tuwe makini.

Huo ndio utaratibu ulivyo kwenye lending business.....ukichelewesha kulipa, lazima riba iongezeke....why? Kama umekopa milioni moja leo na baada ya mwaka unatakiwa uwe umerejesha 1.5m, hiyo 1.5m ya mwakani haitakuwa sawa na miaka mitano ijayo!!! Hivyo basi, lazima riba iongezeke ili ku-offset muda uliopita!
 
Does this make economic sense.., 60,000/= kwa mwezi ??? , hapo tunaongelea machinga (wachuuzi / middle men / au wafanyabiashara wadogo wadogo).., ?

Kwa maisha ya sasa ya machinga wengine kutokupata hapa pesa ya kunywa chai kweli wanaweza kupata buku mbili kwa siku ya kulipa pango (tena ukizingatia biashara zao nyingi zinafanana, hence wakikaa sehemu moja competition inazidi).., kumbuka machinga wengine ni watu wanaopewa bidhaa na wauza maduka daily ili wawauzie hawana hata pesa ya mtaji

Ukitaka kufahamu endapo ina-make sense au hapana, nenda pale Mchikichini ukapate ubao wa kuuzia....utakimbia!
 
Ukitaka kufahamu endapo ina-make sense au hapana, nenda pale Mchikichini ukapate ubao wa kuuzia....utakimbia!
NasDaz

Sijajua location ya hapo mchikichini pakoje wala sijui capacity yake ni watu wangapi.., point yangu ni kwamba kama kuna watu kama 5000 within the same building selling more or less same stuff sababu supply itakuwa kubwa hence itabidi price kushuka kutokana na kugombania wateja.. (sijui labda wewe unaongelea wamachinga gani ?) mimi naongelea wale the low class the bottom of the chain just before consumer ambao wanachukua mizigo hapa na kupeleka pale...

Kwahio kwangu mimi solution ya watu hawa sio kuwaongeza na kuhamasisha kuwaingiza kwenye supply chain bali long term solution ni kuanza uzalishaji (viwanda vya kubalisha mali ghafi into finished articles) ili kuweza kumeza hili lundiko la vijana ambao hawana any other means to get their bread..

Haya mambo ya supply tuyaache percent ndogo ifanye au watu wanaweza kufanya kama extra mradi wa kuwaongezea kipato.. (sio kushauri kila mjasiriamali au 80% ya vijana wote wasio na ajira wafanye uchuuzi)
 
Last edited by a moderator:

Mchikichini ndilo soko lililozoeleka kwa sasa....hata hivyo, hii Machinga Complex is just few metres from Mchikichini. Tatizo kubwa la Machinga Complex ni uwepo wa Mchikichini ambayo kama nilivyosema, zipo karibu karibu. Unfortunately, ama jiji au Manispaa wameshindwa kuwaondoa hawa wafanyabiashara waliopo Mchikichini...so, unakuta hata wale wanaokata shauri kuja Machinga Complex wanalazimika kurudi Mchikichini kwavile wenzao wengi wapo kule na wanunuzi wanaenda kule...!! Na hata wale wachache waliopo Machinga Complex, unakuta wameegesha tu bidhaa zao pale, lakini mauzo wanafanyia Mchikichini! Hawa wanaamua kuegesha baadhi ya bidhaa zao Machinga Complex, ili ikitokea serikali kufanya kweli na kuwatimua pale Mchikichini, wao wasipate taabu kwa kwenda!!! Likewise, hii Machinga Complex haikuwalenga Machinga wanaotembea barabarani, la hasha...bali wenye sehemu maalumu za kufanyia biashara kama ilivyo pale Mchikichini. Na kama nilivyosema, huwezi kupata eneo zuri pale Mchikichini bila kulipa angalau Laki 4 kwa mwezi....na hii pesa, inaliwa na wajanja tu kwavile hakuna mmiliki halali pale!

Kuhusu Location, Mchikichini ni sehemu ya kawaida sana, ni eneo dogo ambalo machinga wote wamerundikana hapo hadi kuathiri kituo cha daladala ambacho kipo karibu na hapo. Machinga wengi ukiwaliza kuhusu kutohamia Machinga Complex, wanalalamika suala la wenzao kuendelea kuwapo Mchikichini na wala sio bei au udogo wa vyumba. jambo lingine ambalo wanalalamikia ni kutowapo kwa kituo cha daladala. lakini kama nilivyotangua kusema hapo awali, Machinga Complex sio kwamba hakuna kabisa kituo, bali kituo kikuu kama ilivyo Mwenge, Ubungo, Kariakoo...in short hakuna gari zinazogeuzia hapo. Lakini kituo kama kituo, kipo na kinaitwa Karume. Magari kutoka sehemu mbalimbali za jiji yanapita hapa. In short, set up ya kituo cha Karume ni kama ilivyokuwa Manzese....kwamba magari yapo on transit lakini hakuna machinga aliyekuwa analalamika kwamba Manzese hamna kituo! And honestly, ilipo Machinga Complex ni rahisi kufikika kutoka sehemu mbalimbali za jiji kuliko ilivyokuwa Manzese. Na ndio maana nikasema, kinachotakiwa pale ni kupiga bakora tu wale machinga waliopo Mchikichini na wote watarudi Machinga Complex.....tatizo ni siasa, hawataki kuwabughudhi wapiga kura na wengi tunatetea ujinga!! hakuna sehemu ambayo zamani ilikuwa kushoto, kama mitaa ya Mliman City, but siku hizi watu wanaenda coz' wanafahamu wakitakacho watakipata! Au angalia ilipo Quality Centre, kushoto kabisa lakini watu wanaenda coz' they knw wakitakacho watakipata! Hivyo basi, hata madai ya Machinga kwamba Complex hakuna wateja ni madai ya kipuuzi tu kwani wote wakienda pale, wateja hawatakuwa na alternative, wataenda tu!
 
Jamanii eeeh mnaitafuta league bila sababu kabisa maana NSSF wao hawatapoteza kitu bali wame gain ardhi na jengo ambalo Manispaa ya Ilala ndio wameliwa hata kama ilikuwa siasa. Ikumbukwe tu jinsi Machinga walivyowasumbua viongozi wananchi kwa kila siku wanapojazana barababarni wakiuza mali zao. Hii ndio sababu kwanza sasa kama unayo idea nzuri zaidi bora muiweke hapa badala ya kulalamikia jengo.

Hata sisi tunapochukua mikopo nje na kuitumia ktk bajeti yetu kwa matumizi ya recurrent wazungu huwa wanajua hawakupoteza kitu japokuwa ukitazama matumizi yetu ni hasara tupu na wananchi wa nchi zao wanalia na kodi zao lakini hawajui undani wa mkopo huo nchi yao imefaidika vipi. Ndio maana ni muhimu kwetu sisi wakopeshaji kujaribu kujitegemea na sii wazungu kuendelea kutoa mikopo. hawa wataendelea kufanya hivyo na hata kusisitiza kuiweka dunia nzima ktk mikopo kwa sababu wanakula interest bila kutoka jasho na mkiharibu deni ndio linazidi - NSSF inachukua nafasi kubwa ya msajili wa majumba nchini na wanajua wanawekeza wapi.

Kama kuna makosa basi ni ya Mbunge wa Ilala ambaye kwa kushangaza alisema ati yeye kazi yake ilikuwa kuwatafuta machnga 5,000 na kuwapangisha swala la kukusanya kodi au mkataba halikuwa jukumu lake ilihali NSSF imetoa mkopo kwa Halmashauri yake.

Kama Azan anashindwa kuzalisha kazi za vijana 5,000 wialayani kwake badala yake anawaona kazi kubwa ilikuwa kuwapata Machinga, tena basi halmnashauri wakiomba kitu ili Machinga asajiliwe ktk jengo hilo.. Viongozi hatuna.. Wakazi wa Ilala wanatakiwa kujua kwamba Mbunge hawana na NSSF watalichukua jengohilo na kurudisha fedha yao harraka kuliko ilivyokuwa awali, nasi tutaendela kuwa na tatizo la Machinga barabarani.
 
Mie nawashangaa sana wanaopiga blah blah za NSSF wamepoteza hela wakati nawauliza maswali ya msingi hawajibu Mkandara. Je nani mmiliki wa jengo hilo? Nani aliwekeza hela yake binafsi katika jengo? Nani aliwakopesha kama walikopa kuweza kujenga jengo hilo? Project kama hizi lazima zina guarantor je alikuwa Serikali au nani? Je wanalipa nini in case jamaa atadefault? Tukishapewa majibu ya hayo ndio sasa tutafahamu kuwa kama NSSF imekula hasara au la. Vyenginevyo huu muendelezo wa Mwanakijiji na chuki yake binafsi dhidi ya NSSF na taasisi yeyote anayokuwapo mwislamu ndani.

By the way Mwanakijiji how is PPF doing? I hope they are surviving jinsi wafanyakazi wake wanavyotanua na magari ya bei mbaya mjini I wonder????
 
Vyenginevyo huu muendelezo wa Mwanakijiji na chuki yake binafsi dhidi ya NSSF na taasisi yeyote anayokuwapo mwislamu ndani.

By the way Mwanakijiji how is PPF doing? I hope they are surviving jinsi wafanyakazi wake wanavyotanua na magari ya bei mbaya mjini I wonder????

Duh... haya we angalia dini tu za watendaji wako ndio uamue kusema au usiseme!
 
Chuki za Mwanakijiji vs Dr Dau au Mwanakijiji vs NSSF au Mwanakijiji vs vijana wa Dau JF au Mwanakijiji vs Waislam wenye vyeo?
 
Mie nawashangaa sana wanaopiga blah blah za NSSF wamepoteza hela wakati nawauliza maswali ya msingi hawajibu Mkandara. Je nani mmiliki wa jengo hilo? Nani aliwekeza hela yake binafsi katika jengo? Nani aliwakopesha kama walikopa kuweza kujenga jengo hilo? Project kama hizi lazima zina guarantor je alikuwa Serikali au nani? Je wanalipa nini in case jamaa atadefault? Tukishapewa majibu ya hayo ndio sasa tutafahamu kuwa kama NSSF imekula hasara au la. Vyenginevyo huu muendelezo wa Mwanakijiji na chuki yake binafsi dhidi ya NSSF na taasisi yeyote anayokuwapo mwislamu ndani.

By the way Mwanakijiji how is PPF doing? I hope they are surviving jinsi wafanyakazi wake wanavyotanua na magari ya bei mbaya mjini I wonder????
Wanajamvi, ifike mahali tusome vitu 'between the lines'. Ukisoma habari utaona MM ameweka chanzo 'NIPASHE'. Tuhuma kuwa yeye anachuki na NSSF zilipaswa kwanza zielekezwe NIPASHE halafu tuangalie hoja zake zitokanazo kama zina chembe za tuhuma.

Pili, Mdondoaji hii ndiyo ilikuwa fursa nzuri ya wewe kueleza umma kile unachokijua kuhusu maswali hayo hapo juu.
Tatu, hakuna ubishi kuwa machinga complex haijatatua tatizo lililokusudiwa

Nne, Je kulikuwa na business plan kabla ya kuamua kujenga? kama ipo basi hii ndiyo fursa ya kutusadia sisi tusiojua na ambao tunaamini huu ni mradi wa kisiasa kuliko kisayansi.

Tano, hoja inajibiwa kwa hoja. Hili la kushambulia taasisi inayoongozwa na waislam ni udhaifu mkubwa sana.
NSSF ni mfuko wa umma na si wa dini au kundi fulani. Kuangauka kwake ni anguko la kila mwanachama.
Ramadhani dau siyo mkurugenzi wa NSSF mwislam, ni mkurugenzi wa NSSF kama alivyokuwa Mustafa Mkulo n.k.

Watu wanapojenga hoja ya udini sijui kama wanajua kuwa hilo litafumua mambo mengi sana. Mathalani, Rais Kikwete amedhihirisha kushindwa kulisadia taifa na ni 'mlezi' wa rushwa. Je, ahukumiwe kwa dini au kama Rais?

Mawaziri walioachishwa kazi nao wahukumiwe kwa kifungu gani. I mean kwa tuhuma za uzembe na ubadhirifu au kwasababu ya dini zao!

Hao Machinga wanaozurura wana dini gani? Jengo lilowazi linamsaidia nani?

Utaratibu wa kutumbukiza hoja za udini ili kuua mada ni udhaifu wa hali ya juu sana.
Ni jambo tunaloliona linakua kwa kasi na kuharibu heshima ya JF. Hivi mtu unawezaje kusema Ramadhani Dau anahujumiwa kwa dini yake bila kuweka ushahidi au kujenga hoja zinzoonyesha ukweli huo?

Endapo MM anachuki basi ni dhima ya wachangiaji kwanza kuiangalia mada, pili kupata chanzo chake halafu kwa kutumia mada hii tuliyo nayo wathibitishe tuhuma zao.

Vinginevyo 'innuendo na person attack' zinaweza kuanzishwa na mtu yoyote(thread) bila kuharibu, kuvuruga au kuingilia thread za mtu mwingine.

Hoja iliyopo mbele yetu ni machinga complex, NSSF na manispaa ya Ilala.
 
Mkuu wangu pamoja na maelezo mazuri hujamjibu mdondoaji!

Maswali yake muhimu sana, kamwe huwezi kufikia conclusion ya kuwa NSSF imepata hasara kama maswali yale

hayajajibiwa. Hata mimi siamini kama shirika kubwa kama NSSF tena linalotunza pesa zetu linaweza kuwekeza kibubusa!
 
Only fool will subscribe to this non sense mie unajua kujadili vitu bila ya kujua :-
a. Mkataba ukoje.

b. NSSF role yake ni nini?

c. Bankruptcy procedure zikoje if the investment default.

d. Marginal return on investment to NSSF ikoje?

Is purely uzushi and makes no sense to me I am sorry to say that Mzee Mwenzangu Mwanakijiji. Bare in mind kazi ya CAG (Chief Auditor General is to highlight the appropriate procedure have been followed and ensure transparency) sasa nieleze wapi CAG kasema huu mtaji una hasara kwa NSSF na kama hasara hiyo NSSF inabeba kiasi gani kama loss on net present value of the outstanding loan. Vile vile tukimaliza tufanye comparison between loss on loans defaulted between NSSF and PPF tuone who is worse off!!! Acheni uzushi wenu jamani and superficial accusation.
 
Sakata la jengo la Machinga Complex lililoko Ilala, Dar es Salaam limebainika kuendesha biashara ambayo hailipi na imeshindikana kulipa deni la mkopo wa ujenzi wake.

Jengo hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lilijengwa kwa mkopo kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sh. bilioni 12.9.

Kutokana na kufanya biashara isiyolipa na kushindwa kulipa deni la mkopo huo, NSSF imesema kuwa jengo la Machinga Complex limeshindwa kurudisha fedha hizo ambazo lilizitoa kwa Jiji la Dar es Salaam kama mkopo.

Jengo hilo la ghorofa lilijengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapatia wamachinga waliozagaa jijini sehemu ya kufanyia biashara zao.

Hadi sasa Jiji limeshindwa kulipa mkopo huo wa NSSF, ambalo kwa sasa deni linakadiriwa kufikia Sh. bilioni 30 kutokana na ongezeko la riba. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya NSSF, Manispaa ya Ilala na Jiji la Dar es Salaam, fedha za kulipia deni hilo zilitarajiwa zitokane na kodi ya jengo hilo ambalo kwa sasa lina idadi ya wamachinga 5,000 waliopanga kwenye vizimba vya kufanyia biashara.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa NSSF, Eunice Chiume, amethibitisha kwamba shirika lake mpaka sasa halijalipwa fedha zozote kama sehemu ya kulipia mkopo walioutoa kwa Jiji la Dar es Salaam.

Chiume alilihakikishia NIPASHE kwamba Jiji halijaanza kulipa fedha hizo, huku akikataa kuingia kiundani katika suala hilo ambalo hivi karibuni limekuwa likizua maswali mengi.

Awali wakati wa ujenzi huo unaanza, serikali ilijigamba kwamba ungekuwa na tija ikiwemo kujiendesha kwa faida na kuwahudumia wamachinga wanaozagaa hovyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, mradi huo hivi sasa umeshindwa kutekeleza malengo hayo sambamba na kushindwa kulipa deni la NSSF.

KAULI YA ZUNGU
Mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu, ambaye alikuwa katika bodi ya ujenzi wa jengo hilo, aliliambia NIPASHE kuwa kazi aliyokuwa amepewa ni kuwakusanya wamachinga na kuwaingiza katika jengo hilo ili wafanye biashara.

Zungu alisema kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi na kufanikiwa kupata wamachinga 5,000 ambapo kila mmoja alitakiwa kulipia kizimba chake Sh. 60,000 kwa mwezi kama kodi.

“Mimi kazi yangu ilimalizika baada ya kuingiza wamachinga 5,000 ili wafanye biashara katika jengo hilo, lakini kazi ya kuhakikisha wanadumu hapo bila kuhama pamoja na kulipa kodi hilo siyo suala langu tena,” alisema Zungu.

Hata hivyo, taarifa kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema kuwa baadhi ya watalaamu wamekuwa wakishauri yawekwe mabango ya matangazo juu ya jengo hilo ili kusaidia kulipa deni hilo, lakini suala hilo linakwamishwa kutokana na vitendo vya ufisadi.

Taarifa hizo zinasema kuwa kama ushauri huo ungekubalika na kutekelezwa, jiji lingeweza kupata zaidi ya Sh. milioni 30 kwa mwezi kutokana na mabango ya matangazo ambazo zingesaidia kulipia mkopo wa NSSF.

MEYA MASABURI
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alipotafutwa hivi karibuni kuzungumzia sakata hilo, aliitupia lawama Manispaa ya Ilala kwa maelezo kuwa ndiyo ilikuwa inashughulika na utaratibu wa kuwaingiza wamachinga katika jengo hilo.

MKURUGENZI ILALA AKOSOA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, alipotafutwa na NIPASHE ili kutoa ufafanuzi wa sakata hilo, alithibitisha kuwa mradi huo haulipi kama ilivyotarajiwa na waliotoa wazo la kuuanzisha.

Aidha, Fuime alithibitisha kwamba mabilioni ya fedha yalitumika katika kujenga jengo hilo, lakini akaweka bayana kwamba ni mradi ambao hauna faida.

Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ilala aliongeza kwamba mapato kutoka kwa wamachinga hayatoshi kulipia deni la NSSF ambalo kwa sasa linazidi kuongezeka kutokana na riba.
Fuime alithibitisha kuwa Manispaa ya Ilala ilishirikishwa katika kuanzisha mradi huo, lakini alisema walioingia katika mkataba ni Ofisi ya jiji la Dar es Salaam pamoja na NSSF.

“NSSF walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo huku jiji likitoa ardhi kama dhamana yake katika kukamilisha mradi huu,” alisema Fuime.

Alisema mradi wa jengo hilo haulipi kwa kuwa wafanyabishara ndogondogo waliokuwa wamekusudiwa kupewa hawana uwezo wa kulipa fedha ili NSSF warudishe mtaji wao pamoja na riba.

Kwa mujibu wa Fuime, ujenzi wa jengo hilo ulifanyika bila kufanyika utafiti wa kina kubaini aina ya jengo lililotakiwa kujengwa pamoja na eneo lilipotakiwa kuwekwa.

Fuime alisema kuwa kutokana na mambo hayo kutozingatiwa, ndiyo maana NSSF inacheleweshwa kulipwa deni lake na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa shirika hilo kuchelewa kupata fedha hizo.
“Mmachinga anatakiwa kujengewa jengo la kawaida ambalo siyo ghorofa na kama likiwa ghorofa basi iwe ghorofa moja, lakini sio kama lile jengo la sasa la Machinga Complex ambalo lina ghorofa zaidi ya mbili,” alisema Fuime.

Aidha, Fuime aliliambia NIPASHE kuwa jengo la aina ile lilitakiwa kuweka soko la wamachinga pamoja na kuwa katika kituo cha daladala ili kuvutia wateja.

Fuime alikiri kuwa siasa ni miongoni mwa vitu vinavyochangia kukwamisha juhudi za watalaamu wanaotaka kubuni njia mbadala za kuwavuta wamachinga wengi ili waingie katika jengo hilo na kufanya biashara.

“Mtalaamu akisema hivi anakuja mwanasiasa anasema acheni watu wangu msiwaguse kwa hiyo mnajikuta mnashindwa kufanikisha miradi mbalimbali inayobuniwa kitalaamu,” alisema.

Aidha, alisema wamachinga waliopewa vizimba katika jengo hilo wengi wao hawakustahili na kwamba waliostahili hawakupata fursa hiyo.

Alifafanua kuwa utaratibu uliotumika kuwaingiza wamachinga hao ni kuwatumia viongozi vya vyama vya wafanyabishara hao na kwamba taratibu kadhaa zilikiukwa.

“Kutokana na makosa hayo yote niliyosema, ni vigumu jengo la Machinga Complex kutengeneza faida hata kama lingekuwepo miaka mingapi kwa kuwa wapangaji wake ambao ni wafanyabiasha ndogo ndogo hawana uwezo wa kulipa mapato ya kutosha,” alisema.

MAONI YA WAMACHINGA
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo waliozungumza na NIPASHE walisema wakati ujenzi wa jengo hilo unaanza waliamini watapata sehemu nzuri ya kufanyia biashara zao, lakini bahati mbaya eneo hilo limekuwa halilipi kwa kuwa hakuna wateja.
Said Haule, alisema watu waliopewa vizimba vya kufanyia biashara siyo wenzao kwa kuwa walichukuliwa watu wengine na kugawiwa huku wao wakibakia katika soko la Karume.

Haule alisema hakuna mmachinga mwenye mtaji mdogo wa mashati matano ambaye anahitaji kuwa mpangaji katika ghorofa kama lile la Machinga Complex.

John Mwakyoma alisema wamachinga wengi waliokuwa wamelengwa kufanya biashara katika jengo hilo wameachwa nje.
Alisema mbali ya kuachwa nje na kukosa nafasi katika jengo hilo, lakini pia wamachinga waliopewa vizimba wameshindwa kufanya biashara vizuri kwa kuwa ni vidogo pamoja na eneo hilo kutokuwa na wateja.
Mkopo wa NSSF kwa ajili ya Machinga Complex ni moja ya mikopo iliyotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2010/11 kuwa ya utatanishi inayoweza kusababisha fedha za wanachama kupotea.

CHANZO: NIPASHE

My Take:
Well..what can I say...

Well,..I say its high time you change your job and take every dime u got outstanding with nssf..coz these morons are busy giving away our hard-earned money,while they sit their asses in office like nothing is happening...why do they have to finance every silly project without givin a second of thought?kiwira coal,machinga complex..etc..WHY??
Get me a gun..I need to see this stupid fund managing director..he needs to understand its people's money hez dealing with..
 
Back
Top Bottom