Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la Machinga: NSSF imekula hasara ya bilioni 30

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sakata la jengo la Machinga Complex lililoko Ilala, Dar es Salaam limebainika kuendesha biashara ambayo hailipi na imeshindikana kulipa deni la mkopo wa ujenzi wake.

  Jengo hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lilijengwa kwa mkopo kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sh. bilioni 12.9.

  Kutokana na kufanya biashara isiyolipa na kushindwa kulipa deni la mkopo huo, NSSF imesema kuwa jengo la Machinga Complex limeshindwa kurudisha fedha hizo ambazo lilizitoa kwa Jiji la Dar es Salaam kama mkopo.

  Jengo hilo la ghorofa lilijengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapatia wamachinga waliozagaa jijini sehemu ya kufanyia biashara zao.

  Hadi sasa Jiji limeshindwa kulipa mkopo huo wa NSSF, ambalo kwa sasa deni linakadiriwa kufikia Sh. bilioni 30 kutokana na ongezeko la riba. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya NSSF, Manispaa ya Ilala na Jiji la Dar es Salaam, fedha za kulipia deni hilo zilitarajiwa zitokane na kodi ya jengo hilo ambalo kwa sasa lina idadi ya wamachinga 5,000 waliopanga kwenye vizimba vya kufanyia biashara.

  Ofisa Uhusiano Mkuu wa NSSF, Eunice Chiume, amethibitisha kwamba shirika lake mpaka sasa halijalipwa fedha zozote kama sehemu ya kulipia mkopo walioutoa kwa Jiji la Dar es Salaam.

  Chiume alilihakikishia NIPASHE kwamba Jiji halijaanza kulipa fedha hizo, huku akikataa kuingia kiundani katika suala hilo ambalo hivi karibuni limekuwa likizua maswali mengi.

  Awali wakati wa ujenzi huo unaanza, serikali ilijigamba kwamba ungekuwa na tija ikiwemo kujiendesha kwa faida na kuwahudumia wamachinga wanaozagaa hovyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

  Hata hivyo, mradi huo hivi sasa umeshindwa kutekeleza malengo hayo sambamba na kushindwa kulipa deni la NSSF.

  KAULI YA ZUNGU
  Mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu, ambaye alikuwa katika bodi ya ujenzi wa jengo hilo, aliliambia NIPASHE kuwa kazi aliyokuwa amepewa ni kuwakusanya wamachinga na kuwaingiza katika jengo hilo ili wafanye biashara.

  Zungu alisema kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi na kufanikiwa kupata wamachinga 5,000 ambapo kila mmoja alitakiwa kulipia kizimba chake Sh. 60,000 kwa mwezi kama kodi.

  "Mimi kazi yangu ilimalizika baada ya kuingiza wamachinga 5,000 ili wafanye biashara katika jengo hilo, lakini kazi ya kuhakikisha wanadumu hapo bila kuhama pamoja na kulipa kodi hilo siyo suala langu tena," alisema Zungu.

  Hata hivyo, taarifa kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema kuwa baadhi ya watalaamu wamekuwa wakishauri yawekwe mabango ya matangazo juu ya jengo hilo ili kusaidia kulipa deni hilo, lakini suala hilo linakwamishwa kutokana na vitendo vya ufisadi.

  Taarifa hizo zinasema kuwa kama ushauri huo ungekubalika na kutekelezwa, jiji lingeweza kupata zaidi ya Sh. milioni 30 kwa mwezi kutokana na mabango ya matangazo ambazo zingesaidia kulipia mkopo wa NSSF.

  MEYA MASABURI
  Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alipotafutwa hivi karibuni kuzungumzia sakata hilo, aliitupia lawama Manispaa ya Ilala kwa maelezo kuwa ndiyo ilikuwa inashughulika na utaratibu wa kuwaingiza wamachinga katika jengo hilo.

  MKURUGENZI ILALA AKOSOA

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, alipotafutwa na NIPASHE ili kutoa ufafanuzi wa sakata hilo, alithibitisha kuwa mradi huo haulipi kama ilivyotarajiwa na waliotoa wazo la kuuanzisha.

  Aidha, Fuime alithibitisha kwamba mabilioni ya fedha yalitumika katika kujenga jengo hilo, lakini akaweka bayana kwamba ni mradi ambao hauna faida.

  Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ilala aliongeza kwamba mapato kutoka kwa wamachinga hayatoshi kulipia deni la NSSF ambalo kwa sasa linazidi kuongezeka kutokana na riba.
  Fuime alithibitisha kuwa Manispaa ya Ilala ilishirikishwa katika kuanzisha mradi huo, lakini alisema walioingia katika mkataba ni Ofisi ya jiji la Dar es Salaam pamoja na NSSF.

  "NSSF walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo huku jiji likitoa ardhi kama dhamana yake katika kukamilisha mradi huu," alisema Fuime.

  Alisema mradi wa jengo hilo haulipi kwa kuwa wafanyabishara ndogondogo waliokuwa wamekusudiwa kupewa hawana uwezo wa kulipa fedha ili NSSF warudishe mtaji wao pamoja na riba.

  Kwa mujibu wa Fuime, ujenzi wa jengo hilo ulifanyika bila kufanyika utafiti wa kina kubaini aina ya jengo lililotakiwa kujengwa pamoja na eneo lilipotakiwa kuwekwa.

  Fuime alisema kuwa kutokana na mambo hayo kutozingatiwa, ndiyo maana NSSF inacheleweshwa kulipwa deni lake na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa shirika hilo kuchelewa kupata fedha hizo.
  "Mmachinga anatakiwa kujengewa jengo la kawaida ambalo siyo ghorofa na kama likiwa ghorofa basi iwe ghorofa moja, lakini sio kama lile jengo la sasa la Machinga Complex ambalo lina ghorofa zaidi ya mbili," alisema Fuime.

  Aidha, Fuime aliliambia NIPASHE kuwa jengo la aina ile lilitakiwa kuweka soko la wamachinga pamoja na kuwa katika kituo cha daladala ili kuvutia wateja.

  Fuime alikiri kuwa siasa ni miongoni mwa vitu vinavyochangia kukwamisha juhudi za watalaamu wanaotaka kubuni njia mbadala za kuwavuta wamachinga wengi ili waingie katika jengo hilo na kufanya biashara.

  "Mtalaamu akisema hivi anakuja mwanasiasa anasema acheni watu wangu msiwaguse kwa hiyo mnajikuta mnashindwa kufanikisha miradi mbalimbali inayobuniwa kitalaamu," alisema.

  Aidha, alisema wamachinga waliopewa vizimba katika jengo hilo wengi wao hawakustahili na kwamba waliostahili hawakupata fursa hiyo.

  Alifafanua kuwa utaratibu uliotumika kuwaingiza wamachinga hao ni kuwatumia viongozi vya vyama vya wafanyabishara hao na kwamba taratibu kadhaa zilikiukwa.

  "Kutokana na makosa hayo yote niliyosema, ni vigumu jengo la Machinga Complex kutengeneza faida hata kama lingekuwepo miaka mingapi kwa kuwa wapangaji wake ambao ni wafanyabiasha ndogo ndogo hawana uwezo wa kulipa mapato ya kutosha," alisema.

  MAONI YA WAMACHINGA
  Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo waliozungumza na NIPASHE walisema wakati ujenzi wa jengo hilo unaanza waliamini watapata sehemu nzuri ya kufanyia biashara zao, lakini bahati mbaya eneo hilo limekuwa halilipi kwa kuwa hakuna wateja.
  Said Haule, alisema watu waliopewa vizimba vya kufanyia biashara siyo wenzao kwa kuwa walichukuliwa watu wengine na kugawiwa huku wao wakibakia katika soko la Karume.

  Haule alisema hakuna mmachinga mwenye mtaji mdogo wa mashati matano ambaye anahitaji kuwa mpangaji katika ghorofa kama lile la Machinga Complex.

  John Mwakyoma alisema wamachinga wengi waliokuwa wamelengwa kufanya biashara katika jengo hilo wameachwa nje.
  Alisema mbali ya kuachwa nje na kukosa nafasi katika jengo hilo, lakini pia wamachinga waliopewa vizimba wameshindwa kufanya biashara vizuri kwa kuwa ni vidogo pamoja na eneo hilo kutokuwa na wateja.
  Mkopo wa NSSF kwa ajili ya Machinga Complex ni moja ya mikopo iliyotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2010/11 kuwa ya utatanishi inayoweza kusababisha fedha za wanachama kupotea.


  CHANZO: NIPASHE

  My Take:
  Well..what can I say...
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  naumwa aisee

  what is left sasa??
   
 3. t

  toby ziegler Senior Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji na wengine humu mimi naomba kuuliza:

  Hivi yule kijana wake Dau hapa JF yuko wapi siku hizi?
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  here we go again .... mwanakijiji vs NSSF ... Dr. Dau kakufanya nini..?
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sera mbovu za ccm utazijua tu. Bilioni 12 si zilitosha kuboresha miundombinu katika baadhi ya vijiji na kuwafanya vijana kubaki huko wajiajiri? Hata hivyo bado hawajachelewa wala kupata hasara. Lile jengo walibadili kwa kuliwekea parking za kukodisha pamoja na ofisi na kumbi za kukodisha. Hiyyo biashara ya machinga haitakaa ifanyike hapo kwa ufanisi.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kha!.. umeona jina langu kwenye hiyo taarifa au natakiwa nikiona kitu cha NSSF nikikimbie kwa sababu fulani? Tofauti na wengine wanavyomuona Dau kwangu hana tofauti na mtendaji mwingine wa shirika la umma au taasisi ya umma - ni sawa na David Mataka au Willim Urio au mtendaji mwingine yeyote. Wote nawashuku! Na utaona hili halihusiani na Dau ni NSSF unless unataka watu waamini kuwa NSSF ni Dau.

  Unatakiwa kuangalia hii hoja; tumeona issue ya uwekezaji wa NSSF Dodoma na huku kwingine; nadhani watu wanatakiwa kuwa waangalifu hasa mifuko hii inaposukumizwa kuwekeza
   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Discuss the issue that has been brought on the table, don't personalize the issue. Mzee Mwanakijiji amenukuu tu hiyo habari na yeye si chanzo chake, so what is your point here? Further more, kilichoandikwa ndio hali halisi na kielelezo cha uwekezaji usio makini unaofanywa na NSSF na mifuko mingine ya penshion. Ulitaka isijadiliwe?
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Yupo sana tu
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  mkuu that is not the way to go.... ameleta hoja, wewe unaleta viroja
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  walaji wamepatikana
  wanakula hadi 'bone marrow' za nchi

  ngoja tuone nini kitafuata, ila hapa tunapena presha tu kwa kuyafahamu mad.udu ya nchi hii.
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu mwanakijiji hebu niambie kama kwenye hiyo hasara michango yangu inahusika...


  NSSF ni shirika la hifadhi la jamii but siasa zimekuwa too much ndani yake..

  nimehamia ppf.

  Hivi zile milioni 50 alizokopaga Sumaye hapo NSSF alirudisha? na ilikuwaje NSSF ikamkopesha mtu asiye mwanachama?
   
 12. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwa vision ya waliobuni mradi huo majengo kama hayo yatajengwa kila manispaa dar na majiji mengine nchini
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.
   
 14. c

  collezione JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Umeongea point ndugu. Vijana wanatakiwa wabaki uko walipo ili wajiajiri. Na sio kukimbilia dar es Salaam.

  Swali linakuja: watabakije uko walipo, wakati hapalipi??? Miundo mbinu mibovu, na hakuna huduma za afya??

  Ndo maana tunataka states gvt. Kila state iwe na vipaumbele vyake. Sio kupangiwa na waziri anayeishi Dar es Salaam. Kila state iwe na Dar es Salaam yake. Ikuze miji yake, na kuleta internal investment bila kupangiwa na waziri au Rais anayeishi Dar es Salaam.

  Utashangaa watu wa Geita wanakimbilia Dar es Salaam, wakati Geita wameacha madini. Utashangaa watu wa Musoma wanakimbilia Dar es Salaam, wakati Musoma wameacha Dhahabu.

  Turudishe madaraka kwa wananchi, ili wanafaike na rasili mali zao. Tuacha mfumo wa waziri mmoja kuwapangia wanaGeita wafanye nini? WanaGeita wajipangie wenyewe nini cha kufanya kwa maslahi yao, na taifa kwa ujumla.

  Kwa hili la Machinga complex, ni mfano dhahiri kwamba. Serikali inataka Tanzania yote iamie Dar es salaam. Vijana watoke uko vijijini waje kuuza mitumba Dar. Na ni kweli, kutokana na maisha magumu uko vijijini. Kila kijana anataka kuja Dar es Salaam
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,171
  Trophy Points: 280
  Bilioni 30 zimetumika kujenga jengo lililo chini ya viwango, hii ni dhuluma kwa wachangiaji wa mfuko, serikali na mfuko wenyewe.
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,408
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Na tukumbuka si hii tu... kuna zile machinga complex nyingine za ahadi za JK. Sijui nazo zitajengwa na hela gani. JAMANI... Polepole naanza kuamini maneno ya Masaburi... Si ajabu wanaofiti kwenye maneno ya Masaburi ni wengi sana hapa nchini kuliko hata idadi ya wabunge wa Dar.
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wakati Wa kampeni za urais baba mwanaasha aliahidi machinga complex kila wilaya hapa dsm nikafikiri wanachazo cha hela Kumbe wanategemea hela za mifuko ya jamii du!!!!!!
   
 18. T

  Thesi JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi MMK cku hizi amekuwa mmiliki wa gazeti la nipashe? Nikirudi kwenye hoja hizi ni athari za maaumuzi ya kisiasa, yanayoleta biashara za siasa. Yaani Utafikiri watu hawajasoma. NSSF shirika la wafanyakazi wanaingia kwenye biashara za siasa. Ni biashara ngapi mbovu wameweka rehani fedha za wanachama? Hivi vitu hawakuangalia kabla ya kuanza mradi? Angalia watendaji wanavorushiana mpira. Ni aibu tupu.
  Lakini nnachotaka kuuliza hivi hakuna pesa hata kidogo inayopatikana hapa kuanza kurudisha huo mkopo? Hapa kuna mchwa wanaangusha nyumba.
   
 19. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kwa upuuzi huu wa watanzania kudhania kila kitu ni personal tutachelewa sana kupata maendeleo. Kila kitu kimewekwa hadharani nikajua utatetea kwa kusema Dr Dau anasingiziwa lakini wewe unaondoa watu kwenye mada ili wadhanie kuwa ni bifu then waache kujadili mabilioni yaliyopotea. Kwa wanachama wa NSSF hii si habari njema kwani michango yao imejenga nyumba ya bundi na popo. Wapuuzi wachache mnaotetea ufisadi kwa kututoa nje ya mada ili tusijadili dhuluma mnastahili kupigwa ban
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?
   
Loading...