Jengo la Maalim Seif Makao Makuu ya ACT Wazalendo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
Siku moja jioni moja miaka sita iliyopita nilipata bahati ya kumfikia Maalim nyumbani kwake Sharif Shamba nje na mbali na matarumbeta na shamrashamra za mikutano na mengineyo.

Ilikuwa starehe kubwa kwangu kunywa kahawa na Maalim na kuchekanae mfano tuko barzani tunapumzika.

Lakini tabu kukutana na mtu kama Maalim Seif ukaacha kumdodosa lau kwa mbali kwa namna ya maskhara.

Nikaanza kumchokoza, ''Maalim tupate basi kitabu makhsusi ulipokuwa kifungoni.''

Kacheka kidogo.
Nilikuwa nimemkumbusha mbali.

Jibu lake lilikuwa, ''In Shaallah.''

Sikumuacha karibu nikaongeza na ''Memoirs...'' yaani kumbukumbu za maisha yake.

Mara ya mwisho kuwa jirani sana na Maalim ilikuwa mwaka wa 2012 Bwawani Hotel nikiwa na TV Imaan tulikokwenda kumsikiliza Maalim akizungumza kuhusu hali ya Zanzibar na mategemeo ya wananchi.

Maalim alikuwa sasa yuko serikalini.

Wazanzibari kwa umoja wao wakiongozwa na Maalim Seif waliamua mwaka wa 2010 kupiga kura kutaka maaridhiano na kuleta Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kurejesha amani na utangamano visiwani.

Ismail Jussa amepata kuandika maneno haya:

''Kwa kupiga kura ya NDIYO, Wazanzibari tulichagua maridhiano na kukataa mfarakano, tulichagua umoja na kukataa mgawanyiko, tulichagua upendo na kukataa chuki, tulichagua matumaini na kukataa khofu, tulichagua amani na kukataa fujo.''

Hii ilikuwa hatua kubwa sana katika siasa za Zanzibar na ndiyo tunaweza kusema iliyofikisha Zanzibar hapa ilipo hivi sasa kiasi tunamtunuku na kumwadhimisha Maalim.

Namkumbuka Maalim na shida niliyowapa walinzi pale nilipoingia Bwawani Hotel katika chumba cha faragha alipokuwa Maalim Seif, Mzee Hassan Nasoro Moyo na viongozi wengine.

Mimi nilikuwa nje na wala sikuwa na nia ya kuingia ndani ya chumba kile kwani mtangazaji na mtu wa kamera tayari walikuwa ndani ya chumba kile wakishughulika.

Hawa vijana wote wana vitambulisho shingoni vinaning'inia na watu wa usalama weshawaruhusu.

Siku ile Maalim alikuwa anazungumza kuhusu hali ya Zanzibar.

Mimi si chochote lakini Ismail Jussa ndiye kanishika mkono tunazunguma basi hadi mle chumbani nikawa sasa uso kwa uso na Maalim.

Ikawa tunazungumza hili na lile, ''easy.''

Sasa nimefungua ''tablet,'' yangu nampiga picha Maalim na wakati mwingine kumwelekeza ''pose,'' niitakayo.

Nilimjua Maalim mwaka wa 1992 na baina yetu tulikuwa na mengi ambayo si wengi wakifahamu.

Hawa walinzi wake rasmi hawakuwa wananijua.

Kumbe jamaa wa Usalama kwa kutonifahamu kidogo wakafanya wasiwasi wa kutaka kunijua.

Mara niko kwa Mzee Moyo tunazunguza na kucheka. Lakini jamaa wa Usalama bado hawajanijua mie nani.

Mara nimemrukia Eddy Riyami basi ikawa kwao wao ni tafrani kidogo.

Nilipotoka nje tu wakanifikia kwa maswali...

Watafiti wa historia mpya ya Zanzibar bila shaka watakapokuja kuandika historia ya visiwa hivi itatoa umuhimu wa pekee kwa Maalim katika uchaguzi wa mwaka 1995 na chaguzi nyingine zilizofuatia.

Kwa mara ya kwanza wananchi wa Zanzibar walitikisa na pengine mtu unaweza kusema walivunja ngome ya dhana ya, ''Mapinduzi Daima.''

Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 hayakuwa na nguvu kama ilivyodhaniwa.

CCM Zanzibar walishindwa uchaguzi ule.

Imewezekana vipi kwa kipindi cha miaka mitatu tu ya Maalim kuwa katika upinzani kuwa na nguvu ya kupambana na kushinda uchaguzi?

Yaliyobakia ni historia.

Uchaguzi baada ya uchaguzi baada ya uchaguzi na matatizo yote yaliyotokea Maalim hakuacha kujaribu kuiongoza Zanzibar katika njia ya maelewano na utangamano baina ya Wazanzibari akisisitiza katika uhuru, amani na utambulisho wa Zanzibar kama nchi.

Zanzibar leo imetulia na inapendeza sawa na msemo maarufu, ''Zanzibar ni njema atakae aje.''

Maalim jina lake limepewa Jengo la Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Tanzania Bara jengo ambalo litafunguliwa rasmi Jumapili ijayo.

Kitendo hiki kimebeba mengi katika historia ya Tanzania.

1667019451466.png
 
Ccm haijawahi kushinda uchaguzi wowote wa Urais Zanzibar tangu mwaka 1995 mpaka leo, hili mliandike waziwazi kwenye historian bila khofu yoyote.

Tena imagine Ccm imepekeka Watanganyika Zanzibar wakiwemo wanajeshi ili kuboost kura za Ccm lakini imeshindikana kwa miaka yote.

Ukitafuta ukweli wa Wazanzibar wenyewe sidhani kama Ccm inaungwa mkono hata na watu laki moja tu sidhani.
 
Ccm haijawahi kushinda uchaguzi wowote wa Urais Zanzibar tangu mwaka 1995 mpaka leo, hili mliandike waziwazi kwenye historian bila khofu yoyote...
CCM ina hali mbaya sana Zanzibar, Hata hao wafuasi laki moja hawana, ni nguvu ya Dola tu inayowaweka mjini.
 
Jengo la Maalim Seif sio mali ya ACT Wazalendo, ni mali ya Maalim Seif.

Enzi za JPM jengo hilo liliporwa kutoka kwa Naalim wakapewa CUF ya Lipumba. Mama Samia amerudisha kwa Maalim, ambaye alishahamia ACT.

Kwa sasa jengo lipo chini ya Maalim Seif Foundation, na chama cha Maalim Seif (ACT) kimeweka ofisi kuu hapo.
 
Jengo la Maalim Seif sio mali ya ACT Wazalendo, ni mali ya Maalim Seif.
Enzi za JPM jengo hilo liliporwa kutoka kwa Naalim wakapewa CUF ya Lipumba. Mama Samia amerudisha kwa Maalim, ambaye alishahamia ACT. Kwa sasa jengo lipo chini ya Maalim Seif Foundation, na chama cha Maalim Seif (ACT) kimeweka ofisi kuu hapo.
Huyu JPM kama hayupo Jehenamu basi hata Jehenamu yenyewe itakuwa ni myths tu haipo.
 
Back
Top Bottom