BAK,Naam kwa maoni yangu kuna priorities ambazo zina umuhimu mkubwa zaidi ya kujenga ofisi ya ubalozi DC. Kwa mfano majengo ya shule zetu ambazo nyingi hayana hata hadhi ya kuitwa shule. Wanafunzi wa shule nyingi bado wanakaa chini au kuboresha drainage system ya Dar ambayo kwa sasa ni hovyo kabisa maana mvua kubwaya dakika 20 tu basi mafuriko kila kona ya jiji. Hizo bilioni 10 zingeelekezwa huko nadhani zingekuwa na matokeo mazuri sana badala ya kujenga jengo ambalo lazima gharama zake zitagubikwa na ufisadi wa hali ya juu. Tusubiri kama hizo gharama tunazoambiwa sasa hazitaongezeka mara tatu au hata zaidi jengo hilo litakapokwisha.
Jengo lilishajengwa zamani. Limenunuliwa limeshamalizika.