Jengeni kwenu

Sema mkuu kuna sehemu ukijenga kiboya,wanakuondoa fasta. Kuna vijiji havifai hata wenyeji wakienda kusalimia anaingia usiku sana na kutoka alfajiri sana
Ni kama tu kule kwetu "Tukuyu".....

Kuna ndugu ni washirikina, inaweza kuwa (shangazi, bamdogo, mjomba na wengineo)

Ukikakarabati tu maskani lazima upigwe juju maana wanataka muwe katika hali sawa...lakini hizo tabia zilishamiri sana miaka ya nyuma tofauti na sasa...

Unyakyusani ukiskia nduguzo wanasema "Bhatengene" jihadhari na juju
 
Tupeane mbinu wajuba namna ya kujenga home kwanza.Maana wakati mwingine unakuta una familia yako huna kiwanja wala nyumba na upande wa pili maskani pia kunahitajika nyumba ya hadhi

Endapo uliomba kuzaliwa basi kajenge kwenu, ikiwa ulizaliwa pasi ya utashi wako basi jenga kwako ikitokea na wewe umeleta kiumbe bila utashi kikute kwao kumejengwa. Ukifa zikwa kwako.

Kujenga kwenu! Wazazi wako walishindwa nini kujenga kwao? Inamaanisha hawakuona umuhimu.
 
Nimeona picha hii sijui alikuwa kiongozi ila mpaka kifo kimemfikia naona kwao alikuwa kashindwa kupaendeleza.
Hivi hawa watu wapo
View attachment 1763679
Bhoke Munanka alijenga kwao Tarime jumba kubwa sana ambalo kila aliyekuwa akiingia tarime mjini lazima ataliona kwa vile lilikuwa kilimani; nadhani lilikuwa na vyumba karibu 10. Lakini lakini yeye mwenyewe alikuwa anaishi Dar na familia yake mpka jumba lile likawa maskani ya nyoka wakazaliana mle. Alipofariki alizikwa Kinondoni, hakupelekwa kwenye jumba hilo.
 
Ni kota za polis mkoani mara wilayani bunda ,huyu polis alijiuwa mwaka 2017
2017 barakoa walikuwa wanaovaa Hospital Tu. Hii kitu ni ya 2020- 2021 Ila sidhani kama ni TZ. Hatuna utamaduni WA kubebesha Wanawake majeneza.
 
Yaani wajenge siku wakifa au,!?sijaelewa heading ya uzi..
Home ni alama, panabaki kama makumbusho mkuu. Hata kama umetokea kwenye nyumba za tembe zinafakiwa kubaki hivyo kama ukumbusho.. tunajenga huku bahari beach , na home katika maeneo mapya ila sio kitovuni 🙄🙄🙄🙄
 
Huu mjadala ni mpana hadi nataka niutungie kitabu, kuna changamoto nyingi sana nimejifunza katika maisha yangu niliyoshiriki mazishi mbalimbali vijijini.

Kuna wakati tuliwahi kwenda kijiji kimoja hadi wakataka turudi na mwili tuje tuzike huku mjini.

Pengine tulifika mchana tukitarajia tuzike saa kumi ndugu wakagoma kuchimba kaburi kwamba hao wanaokuja kutoka mjini waje wachimbe wenyewe.

Mambo mengi yanasababishwa na koo zetu sio ya msingi na ukiwa kwenye vikao ukasema huu ni upuuzi yani na wewe lazima utaingia kwa hii crisis.
 
Vijana wa kiume huwa hamkumbuki kutengeneza kwenu
Hivi nani anapaswa kuyengeneza nyumbani kwenu baba au wewe?je nani atatengeza kwako au utasubiri mtoto wako aje akutengenezee na wewe,na kwanini ukazikwe kwenu ambako baba yako hajatengeneza?

Baba yako atazikwa kwake ambapo hajateneza kwani ukiumwa huwa unaenda kutibiwa kwenu?

Sera za extended family hizo zimepitwa na wakati
 
Naunga mkono hoja, haina haja ya kujenga bangaloo kijijini kwenu ila angalau weka hata nyumba ya Vyumba viwili, sebule na bati juu, siku ukipumzika kwa amani au ukitembelea na familia kijijini upate pa kufikia. Wengi wanajenga majumba ya kifahari mjini na kupasahau kwao, cha msingi jenga hata ya kawaida tu sio lazima iwe na matiles au sliding windows ila itakusitiri siku utakaporudi kwenye chimbuko lako.
 
Luna vijiji vingine unatakiwa uchaguw moja. Kufa au kujenga nyumba. Kwenye msingi tuu wanakuondoa.
 
Napingana na kujenga mahali ambapo utakaa kwa juma moja na kuacha kujenga mahali ambapo unakaa kwa majuma 51. Juzi kna kijana alikuwa anajichanga akajenge kwao. Eti baba ake kamwambia aanze kujenga home. Nikamwambia hiyo ni ajenda ya kibinafsi. Hao lengo lao ni kuwajengea wao wapate sehemu ya kuishi huku wewe na mkeo mkibaki kuteseka kwenye nyumba za kupanga! Kifupi, anza kujenga pale shughuli zako za kiuchumi zilipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…