Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,460
- 860,327
Hofu ni kitu kibaya sana.. Inaua kimwili na kiroho pia, inafubaza akili na kufisha ndoto nyingi sana.. Ukiweza kuishinda hofu umewin maisha katika nyanja nyingi sana
Ni wazi kuna upande haukufurahishwa kabisa na mafanikio ya SIMBA day jana, kuanzia mpangilio wa shughuli, mahudhurio mpaka ushindi mnono wa goli mbili dhidi ya waalikwa
Wenye kutafuta sababu wanaojifanya ni wana SIMBA wanajaribu kutengeneza dosari mbalimbali kama hizi
. Ni bonanza tu
. Tumealika timu mbovu
. SIMBA eti ilibebwa
. Na kali kuliko yote ambayo ndio imefanikiwa kuzua mjadala ni 'jeneza'
Kwamba mafanikio ya SIMBA day yametiwa dosari na hilo jeneza ! HOFU!... Nimejaribu kujiuliza dosari ni ipi kati ya mtani aliyepigwa mbili bila ama SIMBA aliyeshinda mbili bila?[emoji23]
Jeneza ni kiashiria cha umauti ama kifo, ni kiwakilishi cha huzuni na majonzi na simanzi... Msanii anapotumia jeneza kama nyenzo ya kufikisha ujumbe tarajiwa hana maana nyingine zaidi ya hizo hapo juu
Waandishi hutumia neno KUUA inapotokea timu moja imeshinda... Kwenye lahaja za lugha kuna viwakilishi vya maneno na kuna viwakilishi vya alama na kuna viwakilishi vya vikaragosi ama michoro picha
Mfungaji anapofunga goli hutumia vidole vya mikono yake kuonesha alama ya kukata shingo.. Tafsiri yake hapa ni kuua..lakini si kwa maana ile ya kuondosha uhai
Juzi kati hapa mwana masumbwi Madongo aliyepoteza pambano round ya nne alijaribu vilivyo kupeleka hofu kwa mpinzani wake kwa tambo mbalimbali na hata kutumia neno kuua.. Lakini mpinzani wake hakubabaika na kilichotokea wote tulikiona.
Mifano ni mingi lakini itoshe tu kusema 'jeneza' la SIMBA ilikuwa ni sehemu ya sanaa na kunogesha shughuli nzima..hakuna dosari iliyotiwa wala hakuna kanuni iliyovunjwa...