Jembe la mkono sasa basi - Mh. Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jembe la mkono sasa basi - Mh. Pinda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngambo Ngali, May 13, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Pinda: Jembe la mkono sasa basi


  Thursday, 13 May 2010 05:46
  Na Mwandishi Wetu

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Kilimo cha jembe la mkono nchini sasa basi kwa vile kimeshindwa kuleta Mapinduzi ya Kilimo na badala yake lazima kutumia zana za kisasa na utalaamu.

  Alikuwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mirumba, Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Mpimbwe baada ya kukabidhi matrekta kwa vikundi vya wakulima katika siku yake ya nne ya ziara yake ya jimbo.

  “Jembe la Mkono siyo zana ya kutegemea kubadili maisha yetu… Wenzetu wanalima kwa matrekata madogo na makubwa, wanapanda na kuvuna kwa matrekta… majembe ya mkono yalitumika zaidi ya miaka 2,000 iliyopita,” alisema.

  Alikabidhi trekta moja kubwa kwa kikundi cha mbugani cha Kijiji cha Itenka; moja dogo kwa kikundi cha Jitume cha Kijiji cha Magamba na jingine dogo kwa kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Kijiji cha Uruira.

  Trekta kubwa aina ya Tafe, liliotengenezwa India, lina thamani ya sh. milioni 51 na wakulima wanatakiwa kuilipa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda sh. milioni 10 ambayo ni asilimia 20 ya gharama ambazo halmashauri hiyo iliingia kulinunua.

  Trekta dogo aina ya Kubota la Japan wakulima hutakiwa kulipia sh. milioni 1.5, ikiwa ni Asilimia 10 tu ya bei yake.

  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda tangu mwaka 2007/2008 imekuwa ikitekeleza agizo la serikali la kununua matrekta na kuyasambaza kwa wakulima kwa bei ya chini, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza kilimo cha zana na cha kisasa.

  Kwa mwaka huu wa fedha unaomalizika Mwezi ujao (2009/2010), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilipanga kununua matrekta madogo 36, kwa gharama ya sh. milioni 284 na matrekta makubwa matano ya sh milioni 258, ikiwa ni utekelezaji wa Mpango huo.  Napenda ndoto zake, seriously!!!!!!!!
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa mkulima kwa hili la kutumia matrekta ya Tafe na Kubota linaniingia akilini lakini hili la Power tiller aghaaaaaaa ulichemka. Ki ukweli power tiller ni mzigo kwa wakulima kwani hili linafaa sana kwenye maeneo ambayo ni soaked land na sio yenye dry/hard land kama dodoma nk na pia si mazuri kwenye milima kama lushoto. Cha kushangaza sasa wakurugenzi wa halmashauri wameyanunua bila kuomba ushauri wa maofisa kilimo wao wakisema ni agizo la waziri mkuu na bei ya power tiller moja ni kama tsh 5 mil ila limenunuliwa kwa 12mil na hizi halimashauri. Matokeo yake sasa wananchi wameshindwa kuyatumia baada ya kuona wenzao wanaoyatumia hayawasidii zaidi ya kuwaletea magonjwa kama kifua kikuu kutokana na vumbi na pia kuwanyong'onyeza kiafya kwani ili lilime linahitaji mkulima atumie nguvu nyingi, kama ukifika kwenye bohari au maeneo mengi ya ofisi za ujenzi Tanzania utayakuta haya matreka madogo yakiwa yamepark, ukiuliza utaambiwa kuwa wakulima hawaji kuyakopesha.Maswali Je ilikuwa agizo toka kwa Waziri mkuu kuwa kila wilaya ni lazima inunue power tiller? Je wataalamu wa kilimo na udongo walihusishwa kikamilifu kutoa ushauri wao kama power tiller zinunuliwe au la au wakurugenzi walinunua kisiasa zaidi, Je azimio la kilimo kwanza litaleta mapinduzi ya kijani au litapindisha migongo wakulima?. Ushauri wataalamu wa kilimo wasikilizwe, serikali itenge hela ya kutosha uli kuweza kuagiza mbolea na matrekta kama kubota ambayo yana uwezo wa kulima hekta nyingi kwa siku bila kuadhili afya ya mkulima, swala la siasa lisiingie kwenye vitu muhimu kama kilimo nk na wakurugenzi waache nidhamu ya woga wafanye kazi kutokana na ushauri mzuri wa maofisa wao walio chini kama DALDO, Waziri mkuu awachukulie hatua za kisheria wale wote ambao wamenunua mapoer tiller kwa bei za juu ikiwa hali bei zake si kubwa kivile kwani hapo kuna chembe chembe za rushwa na ufisadi Mwisho Haiwezekani kilimo kuwa kwanza kinadhalia tu wakati katika bajeti ya nchi kimepewa kipaumbele cha nne, ni vema kuwa makini kwa kila jambo sio kushika hili na lile baadae moja lazima lituponyoke tu.

  Mkereketwa
   
 3. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  To be honest napenda kuwauliza Hivi mrisha fanya research ya hizo tender za wanao leta ma trecktor yao na Je yanahimili mbuga zetu za huko kilosa na ardhi za kuho kanda ya ziwa na kaskazini? tusije jaribu jaribu vitu hapa na baaada tukaanza point finger to each of us, kabisa nawambieni ngojeni mtaniambia kuhusu izo pembejeo zitakapo fika maana naona watu wanakimbilia tu kuchukua tender za kuuza hizo pembe jeo.me namashaka nazo sana ipo ziku zitakuja kutupotezea mwelekeo wa maendeleo yetu kama hatuto simamia hizi (a.k.a Kauli mbiu),sera na sheria tuzianzishazo wandugu

  Kipindi cha nyuma kuna company moja kubwa dunia ya tracktor waliomba kibari cha kufanya assemble ya hayo ma tracktor lakini ndani ya serikali yetu kwa sababu haojamaa walikuwa hawana mtu na wakapingwa vibaya basi ile kambuni ilishuka kusini mwa africa na wakapewa kibali cha ku assemble tracktor sasa sijui hawa viongozi wetu hawakujua kuwa kuna kilimo kwanza au ndio wame implement juzi juzi? tu basi mjue hata kuendelea kwake kutatuchukuwa miaka ku reach hizo goals za kilimo kwanza kwa wakulima i mean kwa watanzania watakao penda kuwa wakulima
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Asante sana mkereketwa, kama ulikuwa kichwani mwangu
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Naona Pinda anawanga khe khe ati trekta moja kubwa .... imbecile.
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Pinda anaongea kufurahisha wapiga kura wake, hilo haliwezekani kwa Tanzania hii, na serikali haina nia ya kumsadia mkulima kwa hali ya chini kabisa, this is political statement - haina ukweli wowote na hali halisi.
   
 7. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani, ni wakulima gani wadogo wa Tanzania ambao wanaweza kuwa na Sh. 10m kununua trekta kubwa au hata hiyo 1.5m kuweza kununua trekta dogo? Nadhani wananchi wenye uwezo na wenye matrekta waombwe kuwasaidia wakulima wadogo kwa kuwalimia mashamba bure ama kwa kuchangia mafuta maana wao tayari uwezo wanao.

  Yupo Mbunge mmoja ambaye amejihakikishia kura za wananchi wa jimbo lake kwa sababu yeye baada ya kupata kiinua mgongo chake bungeni aliamua kununua trekta na kila msimu wa kilimo baada ya kumaliza kulima shamba lake amekuwa akitoa trekta hilo wananchi walitumie bureee mradi tu wachange fedha za mafuta na wakati mwingine mbunge huyo hujitolea kuwanunulia wananchi mafuta pale anapoona hawana uwezo wa kununua. Huo ni mfano bora wa kiongozi. Wananchi hao wameweza kulima mashamba makubwa na kujipatia kipato zaidi kutokana na kujitolea kwa mbunge wao kuwasaidia.
   
 8. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hapa sijamuelewa mweshimiwa waziri. Ilo jembe moja ndo basi?

  Halafu yeye akiongea kwa sababu ni waziri mkuu lazima awe specific aseme na aongeze kama anaongelea katika ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa au Taifa.

  Maana akiongea waziri Mkuu tunamtazama sana sana aongee kitaifa. Hivyo tunaomba achague maneno ya kusema vizuri.
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu kumbe nawe umeliona? yaani anaongelea kaeneo kadogo ndani ya Tz, afu ana generalise eti jembe la mkono basi!
  Huyu naye nimemstukia ni mzee wa maneno ya kufurahisha baraza tu, utekelezajikiduchuu!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hawa watu wana matatizo; hivi wanakumbuka mara ya mwisho kusema "kuondokana na jembe la mkono" ilikuwa lini?
   
 11. m

  magee Senior Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hesabu rahisi........hivi zile bilioni 40 za kampeini tunanunua matrecta mangapi???fanya hesabu hii rahisi then unipe jibu........
  40,000,000,000/1,500,000 au
  40,000,000,000/10,000,000
  ni sawa na mangapi?????
   
 12. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  what a pipe dream...! :angry:
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  POLITICIAN, ONE WHO SHAKES YOUR HAND BEFORE ELECTION AND YOUR CONFIDENCE LATER


  Silent whisper kwa hii nitapendekeza waongezee kabatani
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wanatambua kauli zao hazina uhalisiaa ila wanafurahiaa tunapozijadilii tena kwa pumzii kubwaa..

  Kwa ujumla pinda hana kauli iliyowahi kutekelezekaaa au yenye mantiki..
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni maneno tu hata kwenye kanga yapo, hizi zana za kisasa zitamfikia lini mkulima wa Biharamulo, hizi trekta ziko Dar tu na vijijini wanaendelea na sera ya KILIMO NI UGONJWA WA UTI WA MGONGO!
   
 16. k

  kisikichampingo Senior Member

  #16
  May 14, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Elnino umeongea. Pinda anaongea ili kukamilisha ratiba ya ziara yake huko kwao. Ni polotical statement.
   
 17. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mi nilifikiri anakwenda kugawa kila kijiji kumbe Mpanda, sasa hizo milioni kweli huyu mkulima wa jembe anazo? Mfanyakazi tu kumlipa KCC ya laki 3 ngumu, sasa huyu mkulima mwenye akiba ya 1.5m to start with..... kweli hawa viongozi wetu huwa wanajisahau wanafikiri wote tunapata mamilioni yasiyokatwa kama wao.
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siku sema thanks kufurahia maneno ya Mheshimiwa Pinda! La hasha! Hii ni kwa kuwa katika hali halisi mheshimiwa Pinda anaongea kufurahisha wananchi wake ambao ndio mtaji wa kura kwake. Nasema hivyo kwa udhati mkubwa kwani kwa hali halisi swala hilo haliwezekani kirahisi kwa mazingira ya Tanzania hii ambayo hata watoto wanafaulu darasa la saba wazazi wao wanashindwa kuwapeleka shule. Si kwakuwa hawapendi bali umaskini umekithiri. Pia kwa hali halisi serikali haina nia ya kumsadia mkulima kwa hali ya chini kabisa,kwa kuwa tunaona jinsi malighafi zinavyopanda.bei
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  PINDA na Serikali ya awamu ya JK,wamesema KILIMO KWANZA ,maana yake kuwa kilimo kitapewa kipaumbele na siyo MKULIMA KWANZA,hapa namaanisha kuwa kilimo kitafanyika na mfanyabiashara yeyote,na siyo lazima uwe mtanzania.tusipoteze muda kujadili kauli mbiu za viongozi,tuangalie je Wameweka mikakati ipi kuboresha maisha ya wakulima.
  Gazeti la New African IC Publications | African Business | Home
  limekuwa likitoa habari kuhusu mikataba ya kilimo kati ya nchi za uarabuni, mfano Mfalme wa Saudi amevuna mahindi aliyopanda ETHOPIA ,hivyo analo shamba kubwa ethopia wakati wakulima wa ethopia wana njaa kali.
  nchi ya Madagascar,imepewa eneo la kulima mpunga nchi ya Mozambiki/Msumbiji.
  kuna kitu kinaitwa FOOD SECURITY,waarabu wameanza kujipanga kwa kuja East Africa kununua maeneo ya mashamba kwa kilimo kwanza,Jana wamefika na uongozi wa nchi umeshawapokea ,
  IN SHORT, ni KILIMO KWANZA na Mkulima wa Tanzania AtaJijua mwenyewe after elections.
   
Loading...