Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
MTU mmoja alifariki na kwenda
jehanamu. Kufika huko akakuta
kuna jehanamu tofauti tofauti
kwa kila nchi. Akaamua
kuzunguka zunguka ili aweze
kuipata jehanamu yenye maumivu
kidogo zaidi.
Akaiendea jehanamu ya
Ujerumani. Akamwuliza mtu
aliyemkuta mlangoni.
"Wanakufanyaje ukiingia humu?"
Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka
kwenye kiti cha umeme kwa saa
moja, kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha mizumari kwa saa
moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kijerumani
anakucharaza bakora kutwa
nzima."
Mtu huyo hakuipenda kabisa
jehanamu hiyo. Akaamua kujaribu
jehanamu za Marekani, Uingereza,
Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini
akagundua kuwa zote zina
adhabu sawa tu na jehanamu ya
Ujerumani.
Kisha akaifikia jehanamu ya
Tanzania. Akastaajabu kuona
kuna foleni ndefu kweli ya watu
wakisubiri kuingia humo. Kwa
mshangao usiosemekana
akauliza, "Jamani kwani humu
wanawafanyaje?"
Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka
kwenye kiti cha umeme kwa saa
moja, kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha mizumari kwa saa
moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kitanzania
anakucharaza bakora kutwa
nzima."
Akazidi kustaajabu. Akauliza,
"Lakini mbona kinachofanyika
humu ni sawa kabisa na
kinachofanyika kwenye jehanamu
zingine, sasa kwa nini hapa kuna
foleni kubwa sana watu wote
wanakimbilia huku?"
Jamaa mmoja akamshika mkono.
Akamvutia pembeni.
Akamnong'oneza, "Watu
wanakimbilia huku kwa kuwa
jehanamu ya Tanzania haina
umeme wa uhakika, unakatika
katika kila dakika kwa hiyo kiti
cha umeme hakifanyi kazi. Halafu
pia misumari ilishalipiwa lakini
wala haijaletwa na mzabuni kwa
hiyo kitanda cha humu ni raha tu
kukilalia. Na jambo jingine ni
kuwa shetani wa Kitanzania
alipokuwa duniani alikuwa
mtumishi wa umma. Kwa hiyo
ameshazowea kufika ofisini na
kusaini kitabu cha mahudhurio na
kisha kuondoka zake kwenda
kufanya shughuli zake binafsi."
jehanamu. Kufika huko akakuta
kuna jehanamu tofauti tofauti
kwa kila nchi. Akaamua
kuzunguka zunguka ili aweze
kuipata jehanamu yenye maumivu
kidogo zaidi.
Akaiendea jehanamu ya
Ujerumani. Akamwuliza mtu
aliyemkuta mlangoni.
"Wanakufanyaje ukiingia humu?"
Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka
kwenye kiti cha umeme kwa saa
moja, kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha mizumari kwa saa
moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kijerumani
anakucharaza bakora kutwa
nzima."
Mtu huyo hakuipenda kabisa
jehanamu hiyo. Akaamua kujaribu
jehanamu za Marekani, Uingereza,
Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini
akagundua kuwa zote zina
adhabu sawa tu na jehanamu ya
Ujerumani.
Kisha akaifikia jehanamu ya
Tanzania. Akastaajabu kuona
kuna foleni ndefu kweli ya watu
wakisubiri kuingia humo. Kwa
mshangao usiosemekana
akauliza, "Jamani kwani humu
wanawafanyaje?"
Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka
kwenye kiti cha umeme kwa saa
moja, kisha wanakulaza kwenye
kitanda cha mizumari kwa saa
moja nyingine. Kisha anakuja
shetani wa Kitanzania
anakucharaza bakora kutwa
nzima."
Akazidi kustaajabu. Akauliza,
"Lakini mbona kinachofanyika
humu ni sawa kabisa na
kinachofanyika kwenye jehanamu
zingine, sasa kwa nini hapa kuna
foleni kubwa sana watu wote
wanakimbilia huku?"
Jamaa mmoja akamshika mkono.
Akamvutia pembeni.
Akamnong'oneza, "Watu
wanakimbilia huku kwa kuwa
jehanamu ya Tanzania haina
umeme wa uhakika, unakatika
katika kila dakika kwa hiyo kiti
cha umeme hakifanyi kazi. Halafu
pia misumari ilishalipiwa lakini
wala haijaletwa na mzabuni kwa
hiyo kitanda cha humu ni raha tu
kukilalia. Na jambo jingine ni
kuwa shetani wa Kitanzania
alipokuwa duniani alikuwa
mtumishi wa umma. Kwa hiyo
ameshazowea kufika ofisini na
kusaini kitabu cha mahudhurio na
kisha kuondoka zake kwenda
kufanya shughuli zake binafsi."