Jehanamu ya Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jehanamu ya Tanzania.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bavaria, Sep 30, 2012.

 1. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,248
  Trophy Points: 280
  MTU mmoja alifariki na kwenda
  jehanamu. Kufika huko akakuta
  kuna jehanamu tofauti tofauti
  kwa kila nchi. Akaamua
  kuzunguka zunguka ili aweze
  kuipata jehanamu yenye maumivu
  kidogo zaidi.
  Akaiendea jehanamu ya
  Ujerumani. Akamwuliza mtu
  aliyemkuta mlangoni.
  "Wanakufanyaje ukiingia humu?"
  Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka
  kwenye kiti cha umeme kwa saa
  moja, kisha wanakulaza kwenye
  kitanda cha mizumari kwa saa
  moja nyingine. Kisha anakuja
  shetani wa Kijerumani
  anakucharaza bakora kutwa
  nzima."
  Mtu huyo hakuipenda kabisa
  jehanamu hiyo. Akaamua kujaribu
  jehanamu za Marekani, Uingereza,
  Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini
  akagundua kuwa zote zina
  adhabu sawa tu na jehanamu ya
  Ujerumani.
  Kisha akaifikia jehanamu ya
  Tanzania. Akastaajabu kuona
  kuna foleni ndefu kweli ya watu
  wakisubiri kuingia humo. Kwa
  mshangao usiosemekana
  akauliza, "Jamani kwani humu
  wanawafanyaje?"
  Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka
  kwenye kiti cha umeme kwa saa
  moja, kisha wanakulaza kwenye
  kitanda cha mizumari kwa saa
  moja nyingine. Kisha anakuja
  shetani wa Kitanzania
  anakucharaza bakora kutwa
  nzima."
  Akazidi kustaajabu. Akauliza,
  "Lakini mbona kinachofanyika
  humu ni sawa kabisa na
  kinachofanyika kwenye jehanamu
  zingine, sasa kwa nini hapa kuna
  foleni kubwa sana watu wote
  wanakimbilia huku?"
  Jamaa mmoja akamshika mkono.
  Akamvutia pembeni.
  Akamnong'oneza, "Watu
  wanakimbilia huku kwa kuwa
  jehanamu ya Tanzania haina
  umeme wa uhakika, unakatika
  katika kila dakika kwa hiyo kiti
  cha umeme hakifanyi kazi. Halafu
  pia misumari ilishalipiwa lakini
  wala haijaletwa na mzabuni kwa
  hiyo kitanda cha humu ni raha tu
  kukilalia. Na jambo jingine ni
  kuwa shetani wa Kitanzania
  alipokuwa duniani alikuwa
  mtumishi wa umma. Kwa hiyo
  ameshazowea kufika ofisini na
  kusaini kitabu cha mahudhurio na
  kisha kuondoka zake kwenda
  kufanya shughuli zake binafsi."
   
 2. d

  dy/dx JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 622
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hahahaha kama kweli vile...
   
 3. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  awesome joke bulldozzer xorry bulldog
   
 4. Kertel

  Kertel JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 2,431
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  Hu hu hu huuuuuuu
  kwa
  kwa
  kwa kwi kwi kwiiiiiiiiiiii
   
 5. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Dah Mtumishi wa Umma kama yule wa pale magogoni yeye ni kuishi kwenye ndege tu... bakora atawacharaza saa ngapi
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Na huyo mcharaza viboko mwenyewe ni kutoka pemba!!saaasaa nyiee,kawaambieni mfanye dhambi nani? Si nnawauliza nyie atiii?sasa mwanipa mikazi miye hataa sikuizoweaga mieee,sasa mi ntawaacha mkome atiii.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii ni nzuri sana aisee.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,774
  Trophy Points: 280
  ahhahaha display reality
   
 9. S

  SILVANUS NJENGA Senior Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umetisha kwa utunzi mzuri
   
 10. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,248
  Trophy Points: 280
  angekua mzaramo awaseme hadi wafe.
   
 11. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ha ha haaa, its the best joke of the day actually....!
   
 12. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda..hahah
   
 13. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Daah umefanya nipaliwe na serengeti kwa kicheko chenye huzuni ndani yake.
   
 14. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Daah huyu mpemba ni mvivu over my ritered wife !!!
   
 15. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh, kazi kwelikweli..mbinguni hamna tanesco ati...
   
 16. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Ushaambiwa ni jehanamu kwanza lazima utofautishe hizo sehemu mbili.... Mbinguni ni kwa wale waliotenda mema na jehanamu ni kuzimu huko ni kwa wale waliofanya maovu kama haya wanayofanya ccm na viongozi wake...

  Na hayo mateso yanaweza kufanyikia sehemu ulipozikiwa... yasemekana ni chini ya ardhi tuishiyo huko ambapo moto huwaka bila kuzimika tizama milima ya volcano au chemichemi za maji moto tokea karne na karne moto tu....

  Tanzania Tanesco ipo...
   
 17. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  hahahahahahahahahha!!hii kali kama ya maprof na mwanafunzi wao aliyetengeneza ndege!
   
 18. Lucy Godfrey

  Lucy Godfrey JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  teh teh teh teh teh te teh
   
 19. ThePromise

  ThePromise JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha haaaa!kumbe kuwa wababaishaji sometimes kuna faida ati!
   
 20. M

  Man soul Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wap ww?
   
Loading...