Geofrey Samson Mkuki (katikati) ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, katika fani ya uhandisi wa Mawasiliano (BSc. in Telecommunication Engineering) mwaka 2013. Kidato cha 4 na cha 6 alifaulu vizuri kwa kupata daraja la kwanza (division 1).
_
Lakini anaishi maisha ya ufukara na ukiwa kijijini kwao Mkiwa, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida. Geofrey hana wazazi (baba na mama yake walishafariki). Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia hiyo ya watoto watatu, hivyo anawajibika kuwalea na kuwatunza wadogo zake.
Tangu amalize elimu yake amekua akihangaika kupata kazi maeneo mbalimbali bila mafanikio. Mwaka 2013 aliajiriwa kama kibarua katika kampuni moja ya mawasiliano lakini baada ya mkataba wake kuisha alirudi nyumbani Ikungi. Baadae alipata ajira ya muda shule ya sekondari Chifu Senge kama mwalimu wa Physics na Hesabu. Baadae serikali ilipiga marufuku waalimu wa 'part time' akaamua kurudi kijiji kwao Mkiwa.
Kwa sasa anajishughulisha na vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza-Dar ili aweze kujikimu kimaisha na kuhudumia wadogo zake.
Kiongozi wa Oparesheni ya Chadema, jimbo la Singida Mashariki Francis Garatwa na Diwani wa Kata hiyo John Siuhi wamemtembelea Geofrey nyumbani kwake leo.
Licha ya kujishughulisha na vibarua vya kubeba mizigo, Geofrey ni mtaalam mzuri wa Computer na uhandisi wa mawasiliano, na amekua akisaidia kutengeneza computer za baadhi ya watu kijijini hapo.
Geofrey anatamani kutoka katika lindi la umaskini lililomvaa lakini haoni njia. Geofrey ni mfano halisi wa tatizo la ajira kwa vijana wengi nchini. Wapo vijana wenye elimu nzuri lakini kutokana na changamoto ya ajira wameshindwa kutumia ujuzi wao kulisaidia taifa na kujisaidia wao wenyewe.
Kama umeguswa na maisha ya Geofrey kwa namna yoyote na unadhani unayo nafasi ya kumsaidia (either kumtafutia kazi au mtaji wa biashara) unaweza kupiga Simu yake ya mkononi kwa nambari 0746440462 au Email:
mkukijs@gmail.com
Credit: Francis M. Garatwa