Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Usimlaumu sana, hakuna mtu anayebadili maisha ila maisha yana mbadili mtu
Mkuu, wakati mwingine maisha yanatubadili kwa uzembe! Sasa huyu ndugu alikuwa na kazi yake mjini kwenye makampuni ya mawasiliano akamua kuacha kazi ili aje akae na wadogo zake. Ilishindikana nini kuwachukua hao madogo akakaa nao huko mjini kwa hicho kidogo alikuwa anapata?
 
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.
Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa.
SIJAJUA LENGO LA HUU UZI. NIMESOMA MARA MBILI MBILI LAKINI BADO SIJAJUA MAANA YA HUU KUWEPO HUU UZI HUMU. DIWANI KAENDA KUMUONA. KAENDA KUMUONA ILI IWEJE? HII HABARI UMEKUTA WAPI?
HUYO DIWANI HANA AKILI. HUU NI ZAIDI YA UDHALILISHAJI MAANA KAMA MTU HUTAKI KUMSAIDIA NI BORA UKAMUACHA NA MAISHA YAKE NA SIYO KUMUWEKA KWENYE MEDIA ILI WAPATE SIFA.
HUU UZI NIMEUSOMA ILA SIJAFURAHISHWA NAO KABISA. DADA YANGU UMEFANYA JAMBO JEMA LAKINI UMEFANYA UDHALILISHAJI PAMOJA NA HUYO DIWANI. MTU ANAHANGAIKA NA MAISHA YAKE AMEKONDEANA. WEWE UNARUSHA HUMU SIJUI UPATE LIKE AU NDIYO UJULIKANE ZAIDI?
KIUFUPI
WEWE, DIWANI NA HAO WALIOCHAPISHA HIYO HABARI WAMEFANYA TUKIO LA UDHALILISHAJI. KAMA MTU HUWEZI KUMSAIDIA ACHANA NAYE NA SIYO KWENDA KAMERA UPATE SIFA.
 
Geofrey Samson Mkuki (katikati) ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, katika fani ya uhandisi wa Mawasiliano (BSc. in Telecommunication Engineering) mwaka 2013. Kidato cha 4 na cha 6 alifaulu vizuri kwa kupata daraja la kwanza (division 1).
_
Lakini anaishi maisha ya ufukara na ukiwa kijijini kwao Mkiwa, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida. Geofrey hana wazazi (baba na mama yake walishafariki). Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia hiyo ya watoto watatu, hivyo anawajibika kuwalea na kuwatunza wadogo zake.

Tangu amalize elimu yake amekua akihangaika kupata kazi maeneo mbalimbali bila mafanikio. Mwaka 2013 aliajiriwa kama kibarua katika kampuni moja ya mawasiliano lakini baada ya mkataba wake kuisha alirudi nyumbani Ikungi. Baadae alipata ajira ya muda shule ya sekondari Chifu Senge kama mwalimu wa Physics na Hesabu. Baadae serikali ilipiga marufuku waalimu wa 'part time' akaamua kurudi kijiji kwao Mkiwa.

Kwa sasa anajishughulisha na vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza-Dar ili aweze kujikimu kimaisha na kuhudumia wadogo zake.

Kiongozi wa Oparesheni ya Chadema, jimbo la Singida Mashariki Francis Garatwa na Diwani wa Kata hiyo John Siuhi wamemtembelea Geofrey nyumbani kwake leo.

Licha ya kujishughulisha na vibarua vya kubeba mizigo, Geofrey ni mtaalam mzuri wa Computer na uhandisi wa mawasiliano, na amekua akisaidia kutengeneza computer za baadhi ya watu kijijini hapo.

Geofrey anatamani kutoka katika lindi la umaskini lililomvaa lakini haoni njia. Geofrey ni mfano halisi wa tatizo la ajira kwa vijana wengi nchini. Wapo vijana wenye elimu nzuri lakini kutokana na changamoto ya ajira wameshindwa kutumia ujuzi wao kulisaidia taifa na kujisaidia wao wenyewe.

Kama umeguswa na maisha ya Geofrey kwa namna yoyote na unadhani unayo nafasi ya kumsaidia (either kumtafutia kazi au mtaji wa biashara) unaweza kupiga Simu yake ya mkononi kwa nambari 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Credit: Francis M. Garatwa
FB_IMG_1560362749769.jpg
 
Tatizo letu wabongo lipo hapa tunapopata shahada za vyuo tumemaliza kusoma huwa! Hatutaki kujifunza tena.
Unadhani ukiwa na elimu ya Telecommunications engineering pekee unaweza kuishi kwa amani mtaani?

Kuna wakati unaweza pewa ushauri na watu wengu sana, lakini hawatakuja kukusaidia ili lazima tulifahamu ndugu zangu.

Magumu unayopitia wewe katika maisha tambua wazi kuna watu wamepitia magumu zaidi yako.

Kuna wakati tukae chini tusome na vitabu vya Art of living ili kupanua uwezo wetu wa kufikiri na namna ya kufikiri.

Mtu ana degree moja kichwani jobless, lakini bado anakaa anailaumu serikali kuwa anaishi maisha magumu kwa sababu hawajampa ajira.

Huu ni upumbavu! Tanzania ina watu wangapi waliosoma fani kama yako mpaka wewe pekee ulilie kuajiriwa? Je Tanzania itaajiri watu wangapi mpaka wote waishe mtaani?

Huyu ndugu yetu alikata tamaa mapema, huenda kazi aliyofanya haikuwa na maslahi kama alivyotarajia.

Lakini alipaswa kutumia nadharia hii ya Napoleon

The Habit of working more than you paid.

Wito wangu kwa vijana kama mimi, ambao mna elimu, tengeni muda msome vitabu vya art of living kubadili fikra mlizonazo. Walio wengi wameharibiwa kifikra tangu vyuoni, na sasa hawajui cha kufikiri zaidi ya kulaumu serikali.

Ukipenda anza kusoma kitabu hiki hapa cha Napoleon Hill. The sixteen Laws of Success. Kitabu hiki kimebadili maisha yangu, hata nikiwa kwenye kundi la watu lazima wanishangae,

Change your thinking, change your life.
 
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Aliwambia ndugu waache tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba la ana panda mahindi, mabamia yanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
Kwa hiyo hata wewe Ulishindwa kumpa elimu mpwa wako badala yake unanunua bando la JF?
 
Mwenyewe amehojiwa akasema alipata ajira lakini akaona arudi kijijini(hayo ni maamuzi yake binafsi angeweza kufanya chaguzi ya kuwaleta wadogo zake mjini),
Nyongeza, hizi elimu zetu za IT na communication engineering zinahitaji angalau internship ya mwaka 1 kabla haujapata ajira rasmi.
Mwenyezi Mungu ampe wepesi.
 
Sio udhalilishaji ila funzo kwa wengine ndugu,

Kuna wakati jicho lako likiingia mchanga linakuwa fundisho kwa watu wengine
SIJAJUA LENGO LA HUU UZI. NIMESOMA MARA MBILI MBILI LAKINI BADO SIJAJUA MAANA YA HUU KUWEPO HUU UZI HUMU. DIWANI KAENDA KUMUONA. KAENDA KUMUONA ILI IWEJE? HII HABARI UMEKUTA WAPI?
HUYO DIWANI HANA AKILI. HUU NI ZAIDI YA UDHALILISHAJI MAANA KAMA MTU HUTAKI KUMSAIDIA NI BORA UKAMUACHA NA MAISHA YAKE NA SIYO KUMUWEKA KWENYE MEDIA ILI WAPATE SIFA.
HUU UZI NIMEUSOMA ILA SIJAFURAHISHWA NAO KABISA. DADA YANGU UMEFANYA JAMBO JEMA LAKINI UMEFANYA UDHALILISHAJI PAMOJA NA HUYO DIWANI. MTU ANAHANGAIKA NA MAISHA YAKE AMEKONDEANA. WEWE UNARUSHA HUMU SIJUI UPATE LIKE AU NDIYO UJULIKANE ZAIDI?
KIUFUPI
WEWE, DIWANI NA HAO WALIOCHAPISHA HIYO HABARI WAMEFANYA TUKIO LA UDHALILISHAJI. KAMA MTU HUWEZI KUMSAIDIA ACHANA NAYE NA SIYO KWENDA KAMERA UPATE SIFA.
 
Mkuu, wakati mwingine maisha yanatubadili kwa uzembe! Sasa huyu ndugu alikuwa na kazi yake mjini kwenye makampuni ya mawasiliano akamua kuacha kazi ili aje akae na wadogo zake. Ilishindikana nini kuwachukua hao madogo akakaa nao huko mjini kwa hicho kidogo alikuwa anapata?
Ni ukweli mzee, elimu yake ina mapungufu. Zero Art of Living.
 
SIJAJUA LENGO LA HUU UZI. NIMESOMA MARA MBILI MBILI LAKINI BADO SIJAJUA MAANA YA HUU KUWEPO HUU UZI HUMU. DIWANI KAENDA KUMUONA. KAENDA KUMUONA ILI IWEJE? HII HABARI UMEKUTA WAPI?
HUYO DIWANI HANA AKILI. HUU NI ZAIDI YA UDHALILISHAJI MAANA KAMA MTU HUTAKI KUMSAIDIA NI BORA UKAMUACHA NA MAISHA YAKE NA SIYO KUMUWEKA KWENYE MEDIA ILI WAPATE SIFA.
HUU UZI NIMEUSOMA ILA SIJAFURAHISHWA NAO KABISA. DADA YANGU UMEFANYA JAMBO JEMA LAKINI UMEFANYA UDHALILISHAJI PAMOJA NA HUYO DIWANI. MTU ANAHANGAIKA NA MAISHA YAKE AMEKONDEANA. WEWE UNARUSHA HUMU SIJUI UPATE LIKE AU NDIYO UJULIKANE ZAIDI?
KIUFUPI
WEWE, DIWANI NA HAO WALIOCHAPISHA HIYO HABARI WAMEFANYA TUKIO LA UDHALILISHAJI. KAMA MTU HUWEZI KUMSAIDIA ACHANA NAYE NA SIYO KWENDA KAMERA UPATE SIFA.
Lengo la huu uzi ni ku expose the issue. JF inasomwa na watu tofauti. Msaada unaweza kupatikana kupitia kwenye uzi huu
 
Inaumiza Sana...unasoma kwa tabu ukiamini baadae mambo yatakua nafuu usaidie ndugu zako lakini inakua kinyume..Na huyu ni sample ya vijana wengi walioko mtaani.

Hakuna anayependa kuwa masikini,lakini wanasema jitihada nazo hazishindi kudra..kazi zimekua kizungumkuti siku hizi...kampuni nyingi zinapunguza watu..Bado hizo ajira chache zilizopo Kuna kujuana kwingi na rushwa za kila aina..dah Lord have mercy on us!
 
Daaaa nimesoma huku machozi yakinivizia.
Hasa nikikumbuka mwaka 2012 nilimaliza chuo July na Desemba mwaka huohuo nikapata ajira mpaka leo maisha yanasonga.
Hee mwenyezi mungu waangalie viumbe wako hawa wanaohangaika mtaani na vyeti vyao vizuri.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom