Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
38,860
Points
2,000

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
38,860 2,000
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

1125671


1125673


1125675
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2013
Messages
5,519
Points
2,000

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2013
5,519 2,000
Kibongo bongo baada ya kujua kusoma na kuandika na kupanga panga baadhi ya namba hakuna kingine chochote itakachokusaidia elimu ya Tanzania.ila nae ali-made some mistake,hakutakiwa kurudi kijiji angepambana kutafuta chumba cha kupanga town alikokuwa na hayo mashirika yaliyompa deiwaka madogo wakasomee huko.

Sasa mpo wote kijiji maisha haya yalivyokuwa magumu nani atamsaidia mwenzake?Mnajikuta wewe uliyesoma unadumaa huku yule asiyesoma kabisa ambae lengo lako ulikuwa umsaidie naye anadumaa zaidi basi mkikaa mnafarijiana tu kimaskini.
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2013
Messages
5,519
Points
2,000

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2013
5,519 2,000
Elimu ya kujitemegea inahitajika sana hasa kipind hiki cha maendeleo ya technology
.................Yah na watu kuelewa hawataki,huko tuendako ile mnakaa office moja kila mtu na kazi yake itaisha itafikia kipindi inabidi akae mtu mmoja tu machine zizibe nafasi za watu kumi sasa hapo pana usalama kweli?

Ni hatari sana hii.
 

Arovera

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Messages
2,960
Points
2,000

Arovera

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2013
2,960 2,000
Mfumo wa elimu hii tuliyorithi kutoka kwa mkoloni inachangia nchi zetu kuzidi kua masikini, nchi ambazo wameendelea walishahama kutoka kwenye theoretical edution na walishahamia kwenye talent based education na specialised education miaka mingi sana. Leo hii Cristiano Ronaldo ana msaada mkubwa kwa nchi yake kuliko mchango wa maprofesa wetu na madaktari wetu wa falsafa kiasi ya kwamba ukiona wanavoargue hao tittled learners wetu doctors na proffessors utaona mapungufu ya elimu yetu
 

Forum statistics

Threads 1,352,689
Members 518,178
Posts 33,066,239
Top