Ndugu yangu we,
Mbona unataka kuwahusisha wananchi kwa mambo yaliyofanywa na viongozi? Ni Mtanganyika gani wa kawaida aliyehusika katika kuusimika muungano? Watu si wameletewa muungano tu? Mimi naona Tanganyika ina muungano mkubwa na Kenya na the rest of Africa kuliko na Zanzibar, maana hapa hatuna a natural boundary, ni mambo ya wakoloni walichora mistari tu, lakini huko Zenj kuna a natural boundary.
Mimi napenda kusisitiza msimamo wangu wa kila siku, muungano huu haujawahi kupitishwa kihalali na wananchi, na kwa hiyo tuitishe kura ya maoni pande zote mbili, swali simple "Unataka muungano uendelee au uvunjwe?" Ndiyo uendelee kama ulivyo, Uvunjwe.
Ili muungano uendelee itabidi kura ya maoni ipate simple majority pande zote.Matokeo yoyote yaheshimiwe.Waangalizi wa kimataifa wawe bwerere kuhakikisha hamna usanii.
Iwapo wananchi japo 50.1 % kutoka kila pande ya muungano watasema wanataka muungano uendelee basi hii ndiyo iwe mandate ya kuendeleza muungano, yeyote atakayeleta fyokofyoko apewe tamu ya rungu la dola kwa kuwa seditious.
Iwapo wananchi japo 50.1% kutoka pande yoyote ya muungano wataukataa, muungano uvunjwe, na mbinu yoyote ya kuudumisha muungano ichukuliwe hatua kama uhaini against the will of the people.
Kwani kuna kazi gani kuongeza hili swali moja katika ballot ya uchaguzi wa rais 2010?
Binafsi, ingawa naweza kusema mengi kuhusu historia, na jinsi gani "Wazanzibari" ni Wamakua, Wazaramo na Wanyamwezi pamoja na Wangazija wachache waliovuka bahari, nimechoka na hizi kelele za muungano na ningepiga kura kuukataa, if only ili tuanze kuwatoza kodi properly "wazanzibari" wanaofanya biashara Dar properly na kuwadai work permit and all that.