Kwa kubadilisha nickname, kazi tunayo!
Tuseme tunaitisha kura ya maoni bila ya kwanza kuuvunja muungano huu ... itakuwaje ikiwa waZanzibari wataukataa na waTanganyika wakaukubali ??
Yakhe si vyema kuchokoana.
Muungano ulitengezwa na watu wawili, Sheikh Karume na Mwalimu Nyerere ambao ndo walikuwa viongozi wetu miaka hiyo. Sasa ishapita miaka kibao na twishajichanganya kiasi kikubwa hivo si vyema kuanza chokochoko kwa shauri la muungano kwani tushakuwa ndugu, hata tukifiliwa, ndugu zetu wa mlima huja kutufariji nasi hivo hivo. Tukianza kudai kujitenga twaweza pata visiwa vyetu lakini tutaanza kubaguana kwa misingi ya uunguja na upemba. Sasa hivi twajifanya tu wamoja kudai tunachoita uhuru lakini hatucheki kwa dhati bali ni vijino pembe. Ndugu zangu, tusitafute mkwamo, tutatue kasoro zilizopo na tuendelee kupiga kasia, bandari bado i mbali.